Serikali kujihusisha na biashara za mafuta ni nia ya viongozi kutafuta rushwa badala ya kujali wananchi. Serikali inashidwa kutatua tatizo la umeme la kununua Generator lakini badala yake inataka kujiingiza kwenye biashara za rushwa kwa kukataza na kuchagua ni nani alete mafuta Tanzania. Je ni lini viongozi wetu wataanza kujali watanzania badala ya matumbo yao, ni lini tutakuwa na viongozi wazalendo. Nani kasema kwamba tu kampuni zikijiunga zitaleta mafuta kwa bei rahisi wakati tanzania inatumia 0.0002% ya mafuta !!. Serikali ijitoe kwenye biashara na hao mawaziri hasa wa nishati hawajui biashara wala wanachofanya bali wanawasikiliza hao wanawapa rushwa wanavyowaambia. Mimi niko hapa Houston, TX kwenye kiini cha kampuni zote za biashara za mafuta duniani na nasema hii ni rushwa na si ukweli kwamba utapunguza bei kwa kuchagua kampuni moja kuleta mafuta!!!