Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ikiwa ni Wiki ya Pili sasa mgao ukiendelea kimya kimya, hatimaye DAWASA yatoa ratiba ya Mgawo wa Maji.
Nanukuu kiongozi wa Mkoa: "Naomba niwaambie wananchi kuwa mgawo haupekuki kutokana na ukame ambao tayari TMA ilishatangaza kuwepo kwa hali hii muda mrefu kulikosababishwa na kunyesha kwa mvua chache msimu wa mvua uliopita na kuchelewa kunyesha kwa mvua katika msimu huu wa vuli.
"Pia watu waelewe hali hii haisababishwi na Serikali wala sera za CCM bali ni mipango ya Mungu, hivyo asitokee mtu huko akaanza kupotosha huko, kikubwa tuendelee kumuomba Mungu atuletee mvua za vuli na vyanzo vyetu vya maji viweze kujaa,” alisema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla siku ya Jumanne 25 Oktoba 2022 baada ya kutembelea vyanzo vya vya kuzalisha maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu.