Dar yakusanya Tsh. Trilioni 13 kati ya 16.5 zilizokusanywa na TRA. Ni aibu kwa Tanzania kutegemea 80% ya Mapato kutoka Mkoa mmoja

Lakini waoa Uchumi wao sio centrally planned kama huku Bongo.

Wana formula nzuri ya mgawanyo na mchango wa Kila states kwenye federal unlike hapa Tanzania

So huo sio mfano mzuri wa kulinganisha na Tanzania.
 
Sasa mada ni GDP au mapato ya kodi ...maana alicholeta mtoa uzi ni mapato ya kodi sio GDP ...sio ajabu kwa nchi kuwa na GDP kubwa kwenye eneo moja kuliko mengine ila ni ajabu kwa nchi kuwa na collection ya mapato kubwa eneo moja kuliko mikoa mingine
Sasa ukitaka kulete kodi nikuulize wewe bidhaa gani inaingia Tanzania bila kupitia bandari ya Dar? kila unacho kula wewe au kujaza mafuta yote yanalipiwa Dar mpaka kampuni zote za simu zinalipa Dar. Kipimo sahihi cha uchangiaji pato kwa mkoa ni uzalishaji.
 
Lakini waoa Uchumi wao sio centrally planned kama huku Bongo.

Wana formula nzuri ya mgawanyo na mchango wa Kila states kwenye federal unlike hapa Tanzania

So huo sio mfano mzuri wa kulinganisha na Tanzania.
Ndio maana inakuwa sio sawa pia kusema Dar inachangia 80% maana bidhaa zote zinapita Dar na zinalipiwa hapo. Kama tunataka kupima basi tungefanya kama Zanzibar wao wanakusanya chao na bidhaa hiyo ikifika Dar inapigwa tena kodi kwa maana kama ushindani. Kwa hapa tungesema kama umeleta mafuta na liter Mil 2 unapeleka soko la Arusha basi yanapita kama transit ikifika Arusha yanalipiwa. USA japo nchi moja ila ni states na mifumo ta Tax tofauti ushindani. Ndio maana kusema Dar 80% ni kwa sababu ya mfumo wetu wa kukusanya kodi unaipa hiyo 80%.
 
Wakati Dar pekee wanakusanya Trilioni 13 Kwa miezi 6 eti Hawa Kagera wamevuka malengo Kwa kukusanya Bilioni 92 😁😁👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DF-FqdGuhMw/?igsh=MWc1NzdqazZmcnJhNA==
 
Hiyo ni calculation na estimates ,GDP sio hela na kuthaminisha vitu Kwa bei
Kwenye income approach unathaminisha vitu gani ..GDP inajumlisha mapato ya serikali pamoja na halmashauri jumlisha mishahara ya wafanyakazi jumlisha mapato ghafi ya taasisi na kampuni jumlisha makisio ya mapato ya watu binafsi waliojiajiri ndio unapata GDP
 
Issue ya Dar kukusanya hela nyingi ni changa la macho la upuuzi wa TRA. Ukishakuwa na Biashara kubwa file lako linahamishiwa Large Taxpayers Department - ilala haijalishi uko mkoa gani. Migodi yote mikubwa nchini mafile yako ilala na kampuni zingine zote kubwa za mikoa mbali mbali hata billionea Mlokozi file lake lipo TRA - Dar ilala japo kiwanda kiko Babati - Manyara.
 
Bado ni uzembe kwanini wasiwekeze bandari ya Tanga kuioa nguvu nayo ikaribiane atleast na dar kupunguza mzigo na foleni bandari ya dar?
 
Bado ni uzembe kwanini wasiwekeze bandari ya Tanga kuioa nguvu nayo ikaribiane atleast na dar kupunguza mzigo na foleni bandari ya dar?
Bandari ya Tanga ngumu kuiendeleza, eneo lake ni strategic zaidi (Kivita), sema lipo eneo ambalo inaweza kujengwa Bandari mpya ya maana, Eneo ni natural lenye kina Kirefu. Mwambani.
 
Hayo hayo maeneo strategic ya kibita ndio wenye akili wanawekeza na kuyalinda kweli kweli.

Pili sio uzembe ni uzezeta wa kushikiliwa akili au muendelezo wa fikra z kikoloni na watu kuwa na akili ndogo.
 
Sasa mambo kama haya manake nini? TRA wanaweza leta sababu za msingi za kufanya huu ujinga?

By the way ni wachache sana wa hivyo,Kwa sababu hata kama faili.lako limehamishiwa huko Ilala kwani unatoka Geita kuja kufanya malipo Ilala? Si unalipa huko huko tuu ila control namba ndio inasoma ya Ilala.
 
Hoja ni Mapato directly yaliyokusanywa kutoka sources mbalimbali.

Habari ya GDP ni mada nyingine has nothing to do here
 
Hakuna kitu cha kulaumu hapo , ndio maana utafutaji wa Dar ukitumia akili ni rahisi kupata pesa. Vitu vingi vya kustimulate uchumi viko Dar huu ni ukweli mchungu
Alafu pesa za dar ni za mikoa yote si dar pekee. Ile business center kama hujui. Lakini pia population ya dar ni sawa mega city hivyo factor za kukusanya mapato mengi dar zipo nyingi kuliko ulinganishe na kigoma etc
 
Mkuu File lako lilipo ndio ofisi yako kikodi na ndipo utakapolipia na inaporipotiwa...
 
Hayo hayo maeneo strategic ya kibita ndio wenye akili wanawekeza na kuyalinda kweli kweli.

Pili sio uzembe ni uzezeta wa kushikiliwa akili au muendelezo wa fikra z kikoloni na watu kuwa na akili ndogo.
Kwa Hapo Tanga huwezi kujenga Bandari kubwa, sababu sio Bahari kuu bali ni Ghuba, kuna wakati inabidi meli kubwa ipaki mbali halafu vile vimeli vidogo vipakue na kuleta Bandarini.

Hio bandari ni strategy ya Vita ya wajerumani sababu hilo eneo ni rahisi kujilinda incase mnavamiwa toka Baharini, hio Ras unayoiona Raskazone ndio kuna makambi ya jeshi, Mizinga etc.

Ili upokee Meli kubwa za kisasa kuenda na wakati unahitaji sehemu kubwa kushinda hio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…