Dar yakusanya Tsh. Trilioni 13 kati ya 16.5 zilizokusanywa na TRA. Ni aibu kwa Tanzania kutegemea 80% ya Mapato kutoka Mkoa mmoja

Dar yakusanya Tsh. Trilioni 13 kati ya 16.5 zilizokusanywa na TRA. Ni aibu kwa Tanzania kutegemea 80% ya Mapato kutoka Mkoa mmoja

Hawana akili hawawezi elewa ubaya wa kurundika Rasilimali kwenye Mji mmja.
Hilo la kurundika rasilimali za nchi sehemu moja ni tatizo la viongozi wa ccm ambao hawana maono kama samia.

Siku Dar nayo ikawaka moto kama moto wa jehanamu California ukateketeza kila kitu kilichoko Dar , Tanganyika itapoteza vitu vingapi vya muhimu ?
 
Sababu kuu Bandari ya Dar

Viwanda

Uwanja wa ndege wa kimataifa
Dar pekee ndio Ina Bahari hapa Tanzania? Unaelewa hoja iliyoko.mezani lakini?

Kuanzia Mtwara Hadi Tanga kote huko Kuna Bandari shida ni hazijawekewa miundombinu kama Dar na ndio hoja yenyewe,why Kila kitu kiwe Dar?

Kwa nini kiwanja Cha ndege chenye Huduma zote kijengwe Dar pekee?

Hivyo viwanda vinafuata Huduma zilizojazana Dar pekee
 
Yaani mikoa yote iliyobaki ikiungaishwa bado haiifukuzi Dar hata kwa mbali! Hii haijakaa sawa!
Harafu hata Mamlaka hata hazishangai.

Ngoja ije itokee siku Moja Dar iwe paralysed ndio akili zitawakaa sawa.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo Mikoa 25 haifikii hata robo ya Mapato ya Mkoa mmja.

Mambo ya ajabu sana haya.
 
Kwani mada yangu inamlajmi.nani?
Tajiri mi napenda open minded dialogues, penye nyeusi iwe nyeusi blue iwe blue sio kusema unajua hii ni kama pinki...

Kimsingi serikali yetu imefeli toka zamani kujikuta wanaifanya Dar ndio hub ya uchumi kwa Tanzania. Angalau Magufuli kafanya jambo kwa kuinyanyua Dodoma, na mama nayeye anajitahidi kuinyanyua Zanzibar. Ili mikoa yote ichangie pato la taifa.

Bahati mbaya sana hakuna kiongozi ameiangazia Mwanza au Arusha kwa ukaribu wakati resources ambazo zipo kule zina nafasi kubwa sana ya kuchangia pato la taifa kwa wastani wa kufanana kabisa.

Samaki waliopo ziwa Victoria na madini yaliyopo Geita kama tungeweka utaratibu mzuri naamini leo tusingeandika hivi. Kana utalii na horticulture vilivyopo Arusha tungevitangaza kiuhakika na kuweka uwazi na uwajibikaji kwa watendaji leo hii tusingeandika hivi..

Serikali inabidi kwanza ibadilishe mindset za watanzania tulio wengi, kwa vitendo. Naamini inawezekana kabisa mapato yakawa yanaingia mengi sana toka pande zingine zozote lakini wengi tunaamini yanapigwa...

Kwa mantiki hiyo, kuwe na uwazi wa mapato katika sekta zote hasa hasa mapato yatakanayo na foreign investment, hasa hasa sekta ya madini na utalii... Leo hii huko Geita wametapakaa wachina kila kona wanachimba dhahabu, je mapato yao yapo wazi, wana impact kwa uchumi wetu??? Hawana janja janja ya kukwepa kodi?? Wana'adhere kwa CSR???

Naamini serikali ikiamua kuweka vitu wazi watu wakahoji na kutoa maoni, trust me Dar itakua ya pili kwa kuchangia pato la taifa. Inaweza kuongoza Zanzibar au Arusha (nightmare) kutokana na mapato ya utalii...

My case is rested!!
 
Mambo mengi yameelekezwa Dar , kiufupi hakuna mtanzania anaweza kuweka mpango wa kutawanya uchumi kwa sababu wanafuata utaratibu walioukuta ...Chuo cha mafunzo ya ndege kipya kinajengwa Dar , karibia projects zote kubwa zinafanyika hapo .
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema Mkoa wa Dar es Salaam ni wa kipekee katika ukusanyaji wa mapato nchini.

Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda alisema hayo Dar es Salaam juzi usiku wakati wa hafla ya kuwapa tuzo walipa kodi bora wa mikoa ya kikodi ya Dar es Salaam kwa mwaka 2023/2024.

Mwenda alisema Dar es Salaam ni mkoa wa kipekee kwa kuwa kuna mikoa mitano ya kikodi: Ilala, Temeke, Kinondoni, Tegeta na Kariakoo. “Licha ya kuwa na mikoa mitano ipo Idara ya Forodha na ina mikoa mitatu mikubwa, kuna Kituo cha Huduma Maalumu, Kituo cha Kukusanya Kodi za Mafuta na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambako tunakusanya kodi,” alisema.

Mwenda alisema sababu hizo na nyinginezo ziliwezesha TRA ikusanye Sh trilioni 16.5 kuanzia Julai hadi Desemba mwaka 2024 na kati ya fedha hizo trilioni 13 zilikusanywa katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Habari Leo

===

MY TAKE

Kitendo cha Nchi kutegemea asilimia 80% ya Mapato Kwa Mkoa mmja wa Dar ni jambo la ajabu na la kushangaza na inaonesha jinsi Nchi Ina uneven distribution of resources. Pia soma Miaka Zaidi ya 60 Baada ya Uhuru,Tanzania Imeshindwa Kuondoa Mizizi ya Ukoloni Kwa Nchi kuwa tegemezi wa Uchumi na Mapato Kwa Jiji Moja tuu la Dar

Hatuwezi kuendelea na utaratibu huu,ni muda muafaka sasa Kwa Serikali kutawanya maendeleo na economic centres kwenye Kila Kanda.

Kwamba Mikoa 25 inakusanya Trilioni 3.5 yaani hata nusu ya Mapato ya Dar hayafiki harafu Walioko kwenye Utawala wanaona sawa tuu.

Ngoja ije itokee Dar kuwa paralysed siku Moja Kwa tukio.loloye ndipo akili zitawajia maana Mtu mweusi Huwa hajifunzi na hana akili za kesho Hadi apigwe tukio.
Trilioni zaidi ya 12 ni Bandari, mtu wa mkoani akitoa mzigo wake Bandari basi unahesabiwa kama ni mapato ya Dar,

Sina uhakika ila sitashangaa pia kampuni kubwa kulipa kodi zao dar hata kama mzigo umeuzwa mkoani.

GDP za mikoa ni indicator nzuri kuliko hii.
 
Mambo mengi yameelekezwa Dar , kiufupi hakuna mtanzania anaweza kuweka mpango wa kutawanya uchumi kwa sababu wanafuata utaratibu walioukuta ...Chuo cha mafunzo ya ndege kipya kinajengwa Dar , karibia projects zote kubwa zinafanyika hapo .
Mtu mweusi ana akili fupi sana ,hapo wanasubiria labda ngozi nyeupe ndio uwaambie sio sawa ndio watakuwa sio sawa ila mweusi mwenzao aliwaambia Huwa hawaelewi.
 
Trilioni zaidi ya 12 ni Bandari, mtu wa mkoani akitoa mzigo wake Bandari basi unahesabiwa kama ni mapato ya Dar,

Sina uhakika ila sitashangaa pia kampuni kubwa kulipa kodi zao dar hata kama mzigo umeuzwa mkoani.

GDP za mikoa ni indicator nzuri kuliko hii.
Dar ndio sehemu pekee ambayo Ina Bahari na Bandari pekee? Kwa nini Bandari zingine zisiwe developed?

Harafu GDP sio hela na Wala haileti au.kuingiza hela.

Dar ikiwa paralysed hata kama mnazalisha huko ila mlango wa kuizia au.ku exports uko Dar Haina maana.
 
Back
Top Bottom