Daraja la J.P.Magufuli (Kigongo-Busisi) ni la 1 kwa urefu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati. Litaondoa tabu ya wananchi kutumia dakika 120

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Daraja la J.P.Magufuli (Kigongo-Busisi) ni la 1 kwa urefu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati. Litaondoa tabu ya wananchi kutumia dakika 120 (masaa mawili) kusubiri kivuko hadi DAKIKA 4 tu kuvuka darajani ili maisha ya uzalishaji kiuchumi na kijamaa yaendelee.

Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza miradi yote kabambe iliyoasisiwa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ambaye wiki hii inafika miaka 3 tangu Mwenyezi Mungu amemuita. RIP uncle JPM.

Asante sana mhe. Rais wetu Mama Samia kwa malengo yako ya Kazi Iendelee. Kwamba mazuri yote ya Awamu Zote Serikali ya Awamu ya 6 itayaendeleza na kuongeza mengi mazuri zaidi. Wakati unaingia madarakani ujenzi wa daraja ulikuwa 25% na sasa umefika 85% na Disemba 2024 daraja linakamilika. Asante sana. @samia_suluhu_hassan.

 
Namwona Fred Lowassa kwenye meza hapo. Kijana anafuata nyayo kama walivyofanya watoto na wajukuu wa John Rockefeller siyo? 👍
 
Ni zamu ya mama Samia naye kukumbukwa Kwa kujenga daraja la KISORYA - UKEREWE
 



" Litaondoa tabu ya wananchi kutumia dakika 120 (masaa mawili) kusubiri kivuko hadi DAKIKA 4 tu kuvuka darajani ili maisha ya uzalishaji kiuchumi na kijamaa yaendelee"

Sijawahi kungoja kivuko kwa zaidi ya nusu saa
 
Kumbukumbu nzuri itakuwa Samia International Airport Mwanza, hii itafaa kwa legacy kanda ya ziwa,mfupa uliowashinda wengi
 
Kwanini siku hizi chawa wamekuwa wengi hivyo huku mtaani?
Hivi hii miradi anajenga mtu, au inajengwa kwa kodi wanazotozwa watanzania?
 
Hapa magu alifanya cha maana sana hili daraja atakumbukwa milele
 
Huyu mpuuzi jiwe alitapanya fedha za watanzania kwa kujenga daraja la mabilioni lisilo na tija. Eti lengo lake kubwa ni kurahisisha usafiri wa kwenda ukweni (kwa akina mama Janeth) Busisi. Pumbafu!
 
" Litaondoa tabu ya wananchi kutumia dakika 120 (masaa mawili) kusubiri kivuko hadi DAKIKA 4 tu kuvuka darajani ili maisha ya uzalishaji kiuchumi na kijamaa yaendelee"

Sijawahi kungoja kivuko kwa zaidi ya nusu saa
Kama MV Mwanza na MV Misungwi zikipiga kazi kwa kupishana kuvuka ni ndani ya saa moja. Sasa ukute ipo MV Misungwi au Mwanza pekee halafu kuna foleni ya malori!!
Kwa tunaosafiri mara kwa mara kupitia hicho kivuko tunaunga mkono ujenzi wa hilo daraja
 
Mwamba Magufuli kwenye miundombinu alikua vizuri sana apewe maua yake tuu
 
Japokuwa jamaa alikuwa mwehu, lakini hata wehu wakikusanya uchafu huwa wanasaidia usafi, hapa aliupiga mwingi sana japokuwa lengo lake ilikuwa kuwakosha ukweni kwake pale Bukumbi kwa mama Janeti, sasa sijui ile shule kubwa sana ya mama janeti kama imeanza kazi, ilikiwa inasimamiwa ujenzi na Mnyeti
 
Kama MV Mwanza na MV Misungwi zikipiga kazi kwa kupishana kuvuka ni ndani ya saa moja. Sasa ukute ipo MV Misungwi au Mwanza pekee halafu kuna foleni ya malori!!
Kwa tunaosafiri mara kwa mara kupitia hicho kivuko tunaunga mkono ujenzi wa hilo daraja


Okay, fair enough, kazi nzuri ya Magufuli kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…