Daraja la Jangwani litajengwa kwa billion 300 au billion 97?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Achana na kile kituko cha jana kwenye utambulisho wa mkandarasi wa kichina kupitia kampuni iitwayo CCC.. KItuko chenyewe ni kitu kipya nilichokisikia kwa mara ya kwanza pochi la mama/ pochi la mama limefunguka

Tafsiri yake ilikuwa ni rahisi sana.. Kwamba hiyo ni pesa ya mtu binafsi toka kwenye pochi lake na kaamua kufanya hisani.. Sikuwahi kudhani Bashungwa naye na usomi wake wote anaweza kuwa chawa promax

Mwaka jana November tuliambiwa serikali imetenga billion 300 za ujenzi wa daraja la Jangwani.. Hii maana yake ni kwamba yalishafanyika makisio yote kwa ajili ya hiyo Kazi.. Lakini kwa mshangao wa wengi jana kwenye utambulisho wa mkandarasi wa hilo daraja tuliambiwa litajengwa kwa billion 97 tuu.

Ninini kilitokea mwaka jana tulipoambiwa ni billion 300 na mwaka huu tunaambiwa ni billion 97?
Hiyo pungufu ama ziada ya billion 203 imekujaje kujaje?
Na VX V8?
Na Yutong?
Na Bodaboda?
Na Baiskeli? Ama na ungo?

Tanganyika..!
 
B
Bashungwa naye ni mmoja wa vijana wa hovyo
 
Hizo ni logistical issues za re allocation of funds ni za viongozi wajuu.
 
Kuna wakati natamani niwe mwana siasa halafu kuna wakati sitamani kabisa,naona tu wacha niendelee kupamabana na hivi vihela vidogo ninavyovipata......
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza katika mahojiano maalum na Ayo Tv ameeleza kuwa ili kumaliza kero na taabu zinazosababishwa na mafuriko yanayotokea mara kwa mara katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam tayari Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhusu Hassan ametafuta fedha za kujenga daraja kubwa la juu Magomeni - Fire ambalo litajengwa kwa zaidi ya Tsh. bilioni 300 na hadi April 2024 shughuli za kuanza ujenzi na Mkandarasi kuwa "site" zitaanza.

“Niwaase Wana Dar es Salaaam mvua bado zinanyesha tuendelee kuchukua tahadhari” Ameeleza Chalamila
November 12 2023
 
Pamoja na kushangaa je wewe unataka zitumike 300 au 97?
 
Acha porojo muhimu kwetu kero tajwa iishe.
 
Zilitengwa bil 300 sasa bil 97 tu. Zingine mama anajipa mwenyewe au zitaenda tumboni kwa wenye meno kula😂🤣
 

Change inapelekwa kwenye uchaguzi ...... Mama kakikamia sana hicho kiti.....!!
 
Kwanza swali muhimu ni je ramani ya mchoro wa mradi imebadilika? Kama imebadilika waliludia kufanya fixibility stuady upya au? Kama mchoro ni ule ule sababu za kushuka kiasi cha pesa ni zipi? Kama fedha ilikuwa imetengwa hapo mwanzoni billioni 300 je 203 itakayobaki itaenda wapi na je aliye idhinisha re allocation ya hzo pesa ni nani maana sina hakika kama bunge limepitisha ilo.
 
Hapo kulikuwa kuna mipango ya kuiba pesa,haiwezekani daraja la busisi - kigongo ambalo lina urefu wa zaidi ya km 3 na baadhi ya nguzo zake zikijengwa kwenye maji lijengwe kwa bilioni 800 halafu hiko kidaraja cha jangwani kijengwe kwa bilioni 300!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…