Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
TAARIFA KWA UMMA
Uongozi wa Wilaya ya Kilolo unapenda kutoa ufafanuzi kwa Umma kufuatia taarifa potofu inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu ubovu wa daraja linalopatikana katika kijiji cha Kiwalamo kilichopo kata ya Idete.
Taarifa hiyo haina ukweli na ina nia ovu ya kuchonganisha Wananchi na Serikali yao pendwa. Hali halisi ni kwamba daraja hilo siyo bovu na linapitika vizuri kabisa, isipokuwa katika kipindi hiki cha mvua nyingi za masika maji yamekua mengi kiasi cha kufurika juu ya daraja na kupelekea kutokea kwa kadhia hiyo.
Hata hivyo daraja hilo lipo ndani ya mpango kazi wa utekelezaji wa upanuzi kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARU-RA) ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi kwenye daraja hilo na kuepuka hali hiyo kujirudia mara kwa mara hususani wakati wa mvua za masika.