Darasa: Jinsi ya kudownload (Kupakua) series za Netflix

Darasa: Jinsi ya kudownload (Kupakua) series za Netflix

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kudownload vitu kuna faida nyingi hasa katika nchi kama yetu

1. Endapo unakaa sehemu ambayo haina network nzuri ni vigumu kustream series za netflix maana itakua inaganda ganda kwasababu ya network.

2. Kustream series kwa vifurushi ni gharama kwa watu wa vipato vya chini, Hivyo wengi wanaweza kutumia vifurushi vya bei chee vya usiku ili kudownload na kucheki series mda wowote.

3. Hutasumbuka na torrents, Mfano Money Heist ilipotoka binafsi nliishusha hapo hapo wakatu bado haijapandishwa kwenye torrents, Pia kuna series ambazo hazipo torrent, wewe utaweza kuzshusha, Hutakuwa tena mtumwa wa hizi torrents

Haya turudi kwenye mada.

1. Ili kudownload series za netflix inabidi uwe na software inaitwa "FLIXGRAB", binafsi naitumia kwenye windows, sijajua kama ipo kwa android ama ios ya iphone na macbook.

2. Software utaipakua hapa >>> Flixgrab - free downloader for Netflix

3. Ukitaka kudownload series utaingia kwenye account yako ya netflix, utachagua series unayopenda na utaenda sehemu ya episodes

4. Uta right click kwenye episode unayoitaka na utaminya copy link location

View attachment 1478350

5. Utafungua flix grab na utaminya paste url
View attachment 1478351

Kumbuka kabla hujadownload unaweza kuchagua quality ya video, lugha ya audio na subtitles utazohitaji.

Pia unaweza kudownload season nzima au kuchagua episode unazotaka kushusha

Kitu cha muhimu ni kwamba kuna toleo la bure na toleo premium la elf 17 kwa miezi mitatu.

Toleo la bure hutaweza kudownload HD, utapata quality ya kawaida sana, ni kam 360 p ndio mwisho

Kama utahitaji kununua njia rahisi ni kutumia mpesa visa card, utaminya *150*00# >>4 >> 6 hapo uatengeneza kadi na utatumiwa meseji yenye taarifa za kadi zako utazotumia kufanyia muamala...Jaza kama elf 18 ndio ufanye muamala.

NAAJUA KUNA BAADHI WATATAFUTA NJIA MBADALA YA PREMIUM VERSION ZILIZOVUNJWA, KUFANYA HIVI NI KUHATARISHA USALAMA WA PC YAKO MAANA VIRUS HAWA WANAWEZA KUKUFUNGIA MAFAILI YOTE (NMESHUDIA KWA WATU WATATU), HERI UNUNUE TU MAANA INARUSU WATUMIAJI WATATU KWAHIO MNAWEZA KUJICHANGA
 
Kwa wale ambao hawaijui pirate bay na torrents
Kuna series kibao za netflix hazipo huko piratesbay, nyingi sana, mfano 3% ya brazil sijaiona nahat za wanaijeria zijaziona

Pia ile money heist ilipotoka tu mimi nilikuwa nina uwezo wa kuishusha mda huo huo bila kusibiria torents, Nakumbuka iliapandishwa kwenye torrents baada ya masaa kadhaa huku sisi tukiwa tushashusha kitambo
 
Wakuu msisumbuke sana,
Teatv, utapata kila kitu bora na series yoyote ile bure,
Kisha rudi unipe mrejesho.
Bila kusahau kwa ubora unaoutaka wewe.

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
Kuna series ama movie za wanaijeria ama wabrazil???
Kuna option za kuchagua lugha ya audio????
 
Kwenye hii app unachek muvi ya mb 250 ikiwa clear kabisa kama hd yan
Ubaya tu ni kwamba sio kila series ya netflix ipo huko, pia kama mdau moja wa juu hapo alivyosema, kuna matatizo ya subtitles mda mwengine.

Ila yote kwa yote nayo inasaidia
 
1. Si kweli kwamba netflix inahitaji internet yenye speed kustream, Netflix wana Hadi Av1 codecs nimestream movie kwa 0.5mbps internet. Mb 500 naangalia movie 2 na mb zinabaki. Na unlimited ya royal Halotel ilikuwa inastream kabla hawajapunguza speed.

2. App ya Netflix ina option ya kudownload huna hata haja ya kutumia 3rd party app, kama movie umeipenda unaidownload. Unless unataka kushare na watu hio movie.
 
Mkuu kuna sehemu kustream 1080P ni kazi mno maana networks zinasumbua, Wa mikoani yuna changamoto sana hapa, Pia kama nlivyosema mwanzono, mtu wa kipato cha kawaida huwa anavizia bando za usiku za bei nafuu GB Kibao, hapa ndipo flix grab husaidia wengi

Kwa kawaidia binafsi nina rafiki na ndugu wanaopendaga kubeba series kwenye flash, hapa ndipo flix grab inanisaidiaga, Pia hata mimi kazini network tunayotumia hairuhusu kuperuzi internet, huwa naziweka kwenye simu nazihamishia kwenye pc za kazini, kukiwa hakuna kazi nacheki
 
Wazee wa torrents hatujakuelewa kabisa
Nakukumbusha tu ya kwamba money heist ilipotoka punde tu nliweza kuishusha papo hapo na wenzangu watabe wa torrents walikuja na flasha zao, Hio money heist karibia kila chimbo kuanzia ettv, eztv, rarbg, kat, pirate bay, teatv n.k ilipandishwa huko baada ya masaa mengi kupita baada ya kuachiwa rasmi netflix, huo muda kuwa watu walikuwa wanakaribia kuimaliza nliowaingizia kwenye flash.

Na kitu kingine hizo torrents ni watu kama sisi tunao rip hizo series ndio zinawekwa, hazijipandishagi.
 
1. Si kweli kwamba netflix inahitaji internet yenye speed kustream, Netflix wana Hadi Av1 codecs nimestream movie kwa 0.5mbps internet. Mb 500 naangalia movie 2 na mb zinabaki. Na unlimited ya royal Halotel ilikuwa inastream kabla hawajapunguza speed.
Nakubaliana na wewe! Zamani mara kwa mara nilikuwa na-subscribe NetFlix lakini baada ya miezi miwili mitatu, nikawa najitoa! Kilichokuwa kinanishinda ni bundle manake episode moja ilikuwa inakula roughly 1GB!

Baadae kabisa, nikaona wacha nijaribu Basic Plan (awali nilikuwa natumia Premium)! Tangu nianze kutumia Basic Plan ni almost mwaka sasa na sijajitoa kwa sababu GB moja ile ile naangalia almost 4 episodes!

Hapo ndipo nikagundua mchawi wangu alikuwa HD anayepatikana kwenye Premium Plan, na hadi sasa sijaona tofauti ya maana in terms of video ya quality!
 
Nakukumbusha tu ya kwamba money heist ilipotoka punde tu nliweza kuishusha papo hapo na wenzangu watabe wa torrents walikuja na flasha zao, Hio money heist karibia kila chimbo kuanzia ettv, eztv, rarbg, kat, pirate bay, teatv n.k ilipandishwa huko baada ya masaa mengi kupita baada ya kuachiwa rasmi netflix, huo muda kuwa watu walikuwa wanakaribia kuimaliza nliowaingizia kwenye flash.

Na kitu kingine hizo torrents ni watu kama sisi tunao rip hizo series ndio zinawekwa, hazijipandishagi.
Muhimu wote tunaona
 
Back
Top Bottom