Darasa la 7 kuanza mitihani ya Taifa Oktoba 7, 2020 huku Kidato cha 4 wakianza Novemba 23, 2020

Darasa la 7 kuanza mitihani ya Taifa Oktoba 7, 2020 huku Kidato cha 4 wakianza Novemba 23, 2020

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756


"Darasa la 7 wataanza Mitihani Oktoba 7-8, Kidato cha 2 wataanza Nov 9 -20, wanaomaliza Kidato cha 4 na wa kujitegemea, wataanza Nov 23 hadi Disemba 11, na Darasa la Nne wataanza Novemba 25 - 26, 2020 " -Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako.

"Kidato cha 5 wataanza kufanya mitihani Julai 24, na Julai 27 wataanza rasmi masomo ya kidato cha 6 na wanafunzi wapya wanaojiunga na kidato cha 5 utaratibu wao utatangazwa majina yatakapotolewa" - Waziri wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako.

"Tangu tumefungua Shule na Vyuo Juni 1, tumekuwa tukifuatilia afya za wanafunzi wetu na mpaka Juni 16, hatujapokea kisa hata kimoja cha Mwanafunzi aliyepata Virusi vya Corona, hivyo muhimu sana kuendelea kuchukua tahadhari" - Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako.

EasapFrXsAAUsLp.jpg

EasapFqXQAAKEuA.jpg
 
BREAKING NEWS: Darasa la 7 wataanza Mitihani Oktoba 7-8, Kidato cha 2 wataanza Nov 9 -20, wanaomaliza Kidato cha 4 na wa kujitegemea, wataanza Nov 23 hadi Disemba 11, na Darasa la Nne wataanza Novemba 25 - 26, 2020 - Waziri wa Elimu, Prof Ndalichako.
EA RADIO
 
Sasa kama ratiba ni hiyo ule utaratibu wa kufidia muda haupo
Mkuu muda gani uliopotea,tatizo unakuta mtu siyo daktari ila anahoji mambo ya kidaktari

Shule zilifungwa tarehe 17 mwezi wa tatu,ambapo kama sikosei ilikuwa imebaki wiki moja watoto wafunge likizo ya mwezi wa NNE ambapo likizo hii ni wiki mbili,baada ya hapo shule zingefungulia tarehe 20 mwezi wa nne na baadae kufungwa mwezi wa sita tarehe 07 hadi tarehe 08 mwezi wa saba,

Ukipiga mahesabu hapo unaona kuwa kuna wiki 01 iliyopotea wakati wa kufunga na pia mwezi mmoja baada ya likizo ya pasaka,kumbuka kwenye likizo ya mwezi wa sita kuna wiki mmoja imekatwa kwani shule zilipaswa kufunguliwa tarehe 08,hivyo kuna upotevu wa mwezi na wiki mmoja ambayo itafidiwa na likizo ya mwezi wa Tisa kwani shule hazitafungwa,

lakini pia kidato cha nne walotakiwa kumaliza mitihani tarehe 23 mwezi wa 11 lakini kwa sasa itakuwa mwezi wa 12 hivyo hakuna muda uliopotea mkuu.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mbombo ingafu, naombea saikolojia ya walimu itulie. Wasipaniki kutaka watoto wafaulu, waende na watoto taratibu bila kuwastress na mi homework na kuwaweka darasani masaa 12 mfululizo kwa kisingizio wamepumzika miezi 3.

Wizara owe makini sana mitihani ya taifa isivuje maana kuna shule bado watakuwa na uchu wa kutaka kuonekana wanaongoza badala ya kuwekeza kwenye kuwafundisha watoto waelewe na si kuwakremisha.

Kuna muda natamani ningekuwa mwalimu na mmiliki wa shule moja ya binafsi nioneshe mfano kuwa inawezekana kuwafanya wanafunzi tangu darasa la kwanza ajitegemee kujisomea na kujiamini kufanya mtihani kwa kuelewa alichofundishwa bila kukaririshwa.

Kuna baadhi ya walimu watalalamika watoto wamesahau yote tuliofundisha January hadi March, as if wao hawasahau mambo sembuse watoto....

Saikolojia inahitajika sana, ndani ya huo muda mfupi watoto wakahitimu hata kwa ufaulu wa C kuliko afaulu A akienda form1 asipokutana na walimu wa kumkremisha anafeli...

Nakumbuka shule tulizosoma miaka ile.... Enzi za Kantalamba Secondary School.

Kila la kheri wazazi, mshirikiane na watoto wenu muongee nao kuwatia moyo.

Kila la kheri walimu, maisha yaendelee kuanzia hapa, hakika mtaweza mkishirikiana na wazazi na wanafunzi.

Kila la kheri wanafunzi wote wenye mtihani wa taifa, wekeza kwenye kuelewa na si kukremisha.

Bibi Matata.
 
Back
Top Bottom