Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Nimepata taarifa zisizo rasmi,kama mdau wa elimu Tanzania,kuwa kuna mabadiliko makubwa katika elimu ya msingi yatafanyika hivi karibuni. Mabadiliko hayo yatahusu mitaala,masomo husika na muda wa elimu ya msingi. Kwanza,elimu ya msingi itaishia darasa la sita. Madarasa ya kutahini yatakuwa ni la nne na la sita. Baada ya hapo ni masomo ya sekondari.
Pili,yapo masomo yatakayofutwa na yapo yatakayoanzishwa. Mfano wa masomo yatakayofutwa ni masomo ya Teknolojia,Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Mfano wa somo jipya ni lile la Maadili litakalofundishwa pamoja na somo la Uraia. Litaitwa Uraia na Maadili.
Kwa miaka sita ya Shule ya Msingi,ni dhahiri kuwa wanafunzi watafika vyuo vikuu wakiwa bado wadogo. Itakuwaje huko Vyuoni? Dunia inategemea mawasiliano na teknolojia,TEHAMA kwanini isiendelee kuwepo? Nini hasa lengo la mabadiliko haya kwa mustakabali wa taifa letu? Natamani zibaki kuwa tetesi tu