Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimepata taarifa zisizo rasmi,kama mdau wa elimu Tanzania,kuwa kuna mabadiliko makubwa katika elimu ya msingi yatafanyika hivi karibuni. Mabadiliko hayo yatahusu mitaala,masomo husika na muda wa elimu ya msingi. Kwanza,elimu ya msingi itaishia darasa la sita. Madarasa ya kutahini yatakuwa ni la nne na la sita. Baada ya hapo ni masomo ya sekondari.
Pili,yapo masomo yatakayofutwa na yapo yatakayoanzishwa. Mfano wa masomo yatakayofutwa ni masomo ya Teknolojia,Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Mfano wa somo jipya ni lile la Maadili litakalofundishwa pamoja na somo la Uraia. Litaitwa Uraia na Maadili.
Kwa miaka sita ya Shule ya Msingi,ni dhahiri kuwa wanafunzi watafika vyuo vikuu wakiwa bado wadogo. Itakuwaje huko Vyuoni? Dunia inategemea mawasiliano na teknolojia,TEHAMA kwanini isiendelee kuwepo? Nini hasa lengo la mabadiliko haya kwa mustakabali wa taifa letu? Natamani zibaki kuwa tetesi tu
Sijui wanafunzi wa Loyola labda unielezee mwenyeweSomo la maadili lina umuhimu wa pekee, we watafute wanafunzi waliosoma Sekondari ya Loyola ndiyo utajua ninacho maanisha hapa.
TEHAMA ianze kufundishwa Sekondary sio shule ya msingi.
Eti eeeeInawezekana sana kwa sasa lakini waweke msisitizo kwenye elimu ya awali kwa watoto wote.
"Enzi" zetu tulijua kusoma, kuandika na hesabu tukiwa darasa la kwanza na la pili na kiingereza tulianza kujifunza darasa la tatu (na kwa kweli mpaka tunafika la saba baadhi yetu hatukuwa na uwezo wa kufanya meaningful conversation kwa lugha ya kiingereza).
Sasa hivi watoto wetu wadogo tu wa chekechea (miaka 4+) wanahesabu vizuri, wanajua kusoma na kuandika (haya wengine tulijifunza darasa la kwanza na la pili) na wanaongea kiingereza katika level ambayo wengine tuliifikia tukiwa kidato cha kwanza au pili. Kwa hivyo nikitizama yote haya, sioni sababu ya watoto hawa wa sasa kusoma shule ya msingi kwa miaka saba....hakuna sababu!
suala la kuishia std six lilianzishwa last year utekelezaji wake uliamuliwa uanze kwa darasa la pili la mwaka huu kwa maana ya kua mwaka 2020 wakimaliza std six wanaletwa secondary straight yaani from std one to form four ni primary school education.Ndalichako ni mzuri, lakini kwa utawala huu atakuja kuwa kituko cha milenia! Atafute ushauri kwa wataalamu wasiojikomba!
wala hakuna jungu wala funiko ukweli mtupu kasema labda waraka wafute Leo!Majungu kutoka kwa wambea wa ufipa at work.
Kila siku mnaleta tetesi kuhusu utawala Wa Magufuli na mambo yao.
Tunaomba mtuletee na tetesi kuhusu kuondolewa uenyekiti mfalme Mbowe
Sisi zamani hatukusoka hiyo TEHAMA tunawezaje kusavivu buana?Nimepata taarifa zisizo rasmi,kama mdau wa elimu Tanzania,kuwa kuna mabadiliko makubwa katika elimu ya msingi yatafanyika hivi karibuni. Mabadiliko hayo yatahusu mitaala,masomo husika na muda wa elimu ya msingi. Kwanza,elimu ya msingi itaishia darasa la sita. Madarasa ya kutahini yatakuwa ni la nne na la sita. Baada ya hapo ni masomo ya sekondari.
Pili,yapo masomo yatakayofutwa na yapo yatakayoanzishwa. Mfano wa masomo yatakayofutwa ni masomo ya Teknolojia,Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Mfano wa somo jipya ni lile la Maadili litakalofundishwa pamoja na somo la Uraia. Litaitwa Uraia na Maadili.
Kwa miaka sita ya Shule ya Msingi,ni dhahiri kuwa wanafunzi watafika vyuo vikuu wakiwa bado wadogo. Itakuwaje huko Vyuoni? Dunia inategemea mawasiliano na teknolojia,TEHAMA kwanini isiendelee kuwepo? Nini hasa lengo la mabadiliko haya kwa mustakabali wa taifa letu? Natamani zibaki kuwa tetesi tu
Binamu hakuna elimu buree!Najiuliza kulikua na haja gani ya kuifanya elimu iwe bure ilhali serikali sasa inakwepa mzigo wa gharama kwa kupunguza huduma? Ni kweli hiki ndicho watanzania walikihitaji?
Ni kweli watanzania walichoshwa na mzigo wa elimu bora waliyogharamia angalau na kuletewa elimu bure ya bana matumizi isiyo na tija? Mwanafunzi kufanya mitihani miwili tu yakuchapwa kwa mwaka ndicho hiki watanzania walihitaji?
YETU MACHO!!!
Sisi zamani hatukusoka hiyo TEHAMA tunawezaje kusavivu buana?
Tehama haifundishwi isipokuwa shule chache sana, kwa sababu nadhani zaidi ya 75% ya shule hazina mazingira na vifaa vya kufundisha somo hilo, kwa hiyo wala usicomplain kwa hilo!!Elimu ya msingi kuishia la sita si mbaya ni hatua nzuri maana itapunguza miaka ya kuwa masomoni na sioni adhari yeyote hapo ila kuhusiana na TEHAMA kufutwa this isn't fair....tuna wanyima wadogo zetu na watoto zetu nafasi nzuri maishani ukizingatia ulimwengu wa sasa ulivyo wahusika walitizame hili kwa umakini..