Darasa la saba kuweza kuwa spika wa Bunge: Haiwezekani chombo nyeti kinachopitisha sheria na bajeti ya nchi kiwe na kiongozi la 7

Darasa la saba kuweza kuwa spika wa Bunge: Haiwezekani chombo nyeti kinachopitisha sheria na bajeti ya nchi kiwe na kiongozi la 7

Lady Mwali

Senior Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
147
Reaction score
333
Inakuaje hata mtu mwenye elimu ya Darasa la 7 vigezo vinamruhusu awe spika? Eti ajue kusoma na kuandika tu. Hivi watunga sheria walikuwa wamelewa au?

Bunge ni kiungo muhimu sana kikiwa muhimili mmojawapo wa serikali baada ya Rais+ baraza la mawaziri na Mahakama, iweje mihimili mingine viongozi wake wawe na elimu kubwa huku spika wa Bunge aweze kuwa la 7?

Mbona Jaji mkuu hawezi kuwa na Elimu ya la 7? Hii sheria ya ajabu sana katika sheria za Tanzania.

Haiwezekani chombo nyeti kinachopitisha sheria na bajeti ya nchi kiwe na kiongozi la 7 ukizingatia spika anaweza kuwa Rais wa JMT.

Wanasiasa acheni unafiki wa kutunga sheria zinazowabeba.
 
Mwenye kujua kusoma na kuandika siyo Darasa la saba... ni binadamu yeyote...
 
Katiba yetu ni 1977 kipindi ambacho mhitimu wa darasa la saba alikuwa msomi tu mzuri wa kiwango cha lami.

Ndio maana tumewahi kuwa hata na rais mwenye diploma ya kishikaji ukiachilia mbali mawaziri kama akina SAS, na wafanyakazi wengi wa umma wenye elimu ya la tano, saba, 12 (form iv) na baadae form six na vyuo tena masters.

Tukubali kuwa tumetoka mbali na tuko mbali ila katiba mpya inahitajika ili iendane na wakati tulio nao na hata level ya elimu waliyonayo watu wetu.
 
Maajabu zaidi ni kwamba. Serikalini ili upate nafasi ya u'dereva lazima uwe na cheti cha form four.
Halafu madereva hawana ofisi za kukaa wanapokuwa eneo lao la kazi wanakaa kwenye magari....haya ni matumizi mabaya sana ya akili na shule pia. dereva form four anaenda kukaa kwenye gari mbunge darasa la saba anajengewa ofisi na eneo "maalum la makazi ya viongozi"

Ukweli hapa hivi vipengele inabidi wavipitie upya watirudishie madereva wetu wakongwe na wajuzi haswaa wa kazi zao.

Wanasiasa baada ya shetani motoni anayefata ni wao.....alisikika mzee mmoja mtandaoni
 
Anatakiwa awe na cheti cha chekechea au PHD?

Bunge sio la wasomi tu kwani nchi hii sio ya wasomi tu.Nafikir kigezo cha kusoma na kuandika ni sahihi kabisa.Kutokuwa na PHD kusiwe sababu ya kubaguana maana hata hizo PhD nazo kuna siku zitakuwa sawa na Darasa la saba.Hata hivyo tuhamasishane tusome ili tusibaguane.
 
Unafahamu Chief Adam Sapi alikuwa na elimu gani?

Sheria ilitungwa hivyo ili kum-accomodate soika aliyekuwepo wakati huo.

Ukweli ni kuwa sifa ya kujua tu kusoma na kuandika ili kuwa mbunge, ni uwendawazimu wa hali ya juu.
 
Kama wasomi wana maana tusingekuwa hapa kwa mikataba ya ovyo. Tumeshuhudia ma Prof, Dr hasa kipindi cha Covid 12 wakisema na kutenda ovyo.

Bora awe na akili timamu tu, hata asijue kusoma watamsomea. Ova
 
Inakuaje hata mtu mwenye elimu ya Darasa la 7 vigezo vinamruhusu awe spika? Eti ajue kusoma na kuandika tu. Hivi watunga sheria walikuwa wamelewa au ?

Bunge ni kiungo muhimu sana kikiwa muhimili mmojawapo wa serikali baada ya Rais+ baraza la mawaziri na Mahakama, iweje mihimili mingine viongozi wake wawe na elimu kubwa huku spika wa Bunge aweze kuwa la 7?

Mbona Jaji mkuu hawezi kuwa na Elimu ya la 7? Hii sheria ya ajabu sana katika sheria za Tanzania.

Haiwezekani chombo nyeti kinachopitisha sheria na bajeti ya nchi kiwe na kiongozi la 7 ukizingatia spika anaweza kuwa Rais wa JMT.

Wanasiasa acheni unafiki wa kutunga sheria zinazowabeba.
Kwani hapo cha ajabu nini?
Cha msingi ajue kusoma na kuandika kiswahili basi mengine awe tayari kupokea maagizo kutoka juu
 
Inakuaje hata mtu mwenye elimu ya Darasa la 7 vigezo vinamruhusu awe spika? Eti ajue kusoma na kuandika tu. Hivi watunga sheria walikuwa wamelewa au ?

Bunge ni kiungo muhimu sana kikiwa muhimili mmojawapo wa serikali baada ya Rais+ baraza la mawaziri na Mahakama, iweje mihimili mingine viongozi wake wawe na elimu kubwa huku spika wa Bunge aweze kuwa la 7?

Mbona Jaji mkuu hawezi kuwa na Elimu ya la 7? Hii sheria ya ajabu sana katika sheria za Tanzania.

Haiwezekani chombo nyeti kinachopitisha sheria na bajeti ya nchi kiwe na kiongozi la 7 ukizingatia spika anaweza kuwa Rais wa JMT.

Wanasiasa acheni unafiki wa kutunga sheria zinazowabeba.
Kwa hiyo darasa la 7 kazi yao ni kuchagua tu, wakitaka kuchaguliwa hapana. Huuu ni ubaguzi na kwa taarifa siasa sio TAALUMA
Kama tunawazuia darasa la saba kuchaguliwa basi tutunge sheria kwa vigezo hivyo hivyo vinavyomnyima haki kuchaguliwa vilevile wasiwe na haki ya chagua.
 
Halafu madereva hawana ofisi za kukaa wanapokuwa eneo lao la kazi wanakaa kwenye magari....haya ni matumizi mabaya sana ya akili na shule pia. dereva form four anaenda kukaa kwenye gari mbunge darasa la saba anajengewa ofisi na eneo "maalum la makazi ya viongozi"

ukweli hapa hivi vipengele inabidi wavipitie upya watirudishie madereva wetu wakongwe na wajuzi haswaa wa kazi zao.

wanasiasa baada ya shetani motoni anayefata ni wao.....alisikika mzee mmoja mtandaoni
Yaani we acha tuu. Bala zito hili
Anatakiwa awe na cheti cha chekechea au PHD?

Bunge sio la wasomi tu kwani nchi hii sio ya wasomi tu.Nafikir kigezo cha kusoma na kuandika ni sahihi kabisa.Kutokuwa na PHD kusiwe sababu ya kubaguana maana hata hizo PhD nazo kuna siku zitakuwa sawa na Darasa la saba.Hata hivyo tuhamasishane tusome ili tusibaguane.
Tunalazimika tuwe na wawakilishi wenye uelewa mkubwa ni kwa sababu humo ndio kuna 'Vision' ya taifa. Kwa elimu ya darasa la saba literally haina mchango mkubwa kwa individual kuwa na uelewa mkubwa, Ubunifu, Exposure na mengine yanayo husiqna na akili. ijapokuwa wapo wachache wa darasa la saba walio 'Smart minded' kutokana na mazingira, genes nk. Lakini commonly elimu ndio measures nzuri katika hilo

So angalau level ya Elimu kuanzia degree inafaa kama kigezo cha kuwa muwakilishi au mtunga sheria wa taifa na kutarajia mazuri. Lakini We 'blacks' factors kama unafiki,njaa, nk hazitatuacha salama haijalishi ni muelevu kiasi gani mfano msosi wenu wa havard
 
Tuanzishe bunge lingine la wataalam na wasomi wabobezi ili miswada ikipita bungeni nao waiangelie na kuridhia au la, pia iangalie na kusimamia katiba na maadili ya viongozi ili liweze kuonya Rais, majaji, spika kama Ndugai akiendesha bunge ovyo. Haiwezekani hadi leo eti hamna Rais aliyevunja katiba au haki za binadamu, wakati mitaani inaonesha Rais anaponda katiba na kukiuka haki za binadamu!
 
Back
Top Bottom