Habari wanajukwaa,
Nimekuwa nikijiuliza Maswali mengi sana juu ya utumishi wa wabunge ambao ni darasa la saba. Muongozo wa ajira Serikalini ni kwamba wanaajiri kuanzia kidato cha nne na kuendelea, kama huna cheti cha form four huna sifa ya kuwa mtumishi wa umma.
Ninavyoelewa mimi inawezekana isiwe hivyo, mtumishi wa umma ni yule anayelipwa mshahara wake na serikali (kupitia kodi za wananchi). Kama serkali iliamua kuwatoa kwenye ajira watumishi wake ambao walikuwa na elimu ya darasa la saba, kwa nini wabunge wa darasa la saba hawakuguswa ili hali nao ni watumishi wa umma.
Mtumishi aliyekuwa dreva au mfanya usafi akaondolewa kwenye ajira kwa sababu ya darasa la saba, serkali haioni kuwa ilimuonea mtu huyo wakati kuna mbunge ambaye ana majukumu makubwa ya kitaifa ikiwamo kutunga sheria na kuishauri serikali. Utampate kazi mtu wa darasa la saba ya kutunga sheria na kushauri serkali wakati huohuo mfanya usafi na dreva ambaye anatolewa kwenye ajira kwa elimu ileile ya darasa la saba.
Serikali ipitie upya hii mifumo na ikiwezekana waongeze ufaulu wa elimu kuwa na sifa ya kugombea ubunge angalau iende mpaka kidato cha sita au stashahada (Diploma).
Wabunge ni wanasiasa.Usilinganishe wanasiasa (politicians) na watumishi wa umma (civil servants). Hawa wawili wanawajibika tofauti. Wanasiasa wanawajibika kwenye vyama vyao na wapiga kura wao. Watumishi wa umma wanawajibika kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Hata sifa zao za kupata kazi ni tofauti.
Wanasiasa mtihani wao ni kutongoza wapiga kura wawapigie kura.
Katika demokrasia ya kweli, huo ni mtihani mkubwa kuliko Ph.D.
Tunachotakiwa kufanya ni.
1. Kuongeza wigo wa elimu kwa jamii.
2. Kuongeza demokrasia ya kweli.
Baada ya hapo, kama wabunge wa darasa la saba hawafai, wananchi watawachuja kwenye chaguzi.
Mimi nina tatizo unapomsakama mbunge wa darasa la saba kwamba hana uwezo wa kuwakilisha wananchi vizuri, wakati, in principle kachaguliwa na wananchi.
Naweza kusikiliza hoja hii zaidi kwenye wabunge wa kuteuliwa. Hawa hata wakiondolewa kabisa wote sina tatizo.
Tatizo la kuongeza kiwango cha elimu kwenye ubunge ni kuibana demokrasia.
Kwa sababu kimsingi kikatiba karibu watu wote wenye umri unaotakiwa wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa uongozi.
Sasa ukianza kuweka viwango vya elimu vya "diploma" ama form six kwenye ubunge, unawanyima wa darasa la saba uwakilishi.
Ni kama vile useme watu walioishia darasa la saba wasipige kura, kwa sababu hawana elimu ya kuchambua mambo. Haki ya kuchagua na kuchaguliwa uongozi zinashabihiana kwa mengi.Ukikataza darasa la saba wasiwe wabunge, utakataza darasa la saba wasipige kura pia?
Wamarekani bunge lao (Senate) halina kiwango cha elimu. Katiba inataja masharti ya umri (miaka 30), uraia wa Marekani kwa angalau miaka 9 na makazi katika jimbo wakati wa uchaguzi huo.
Hakuna sharti la elimu.
Kwa nini? Wananchi wenyewe wataamua kama huyu mtu ameelimika vya kutosha kuwa Senator ama la.
Pia, viwango hivi ni vitu ambavyo havina guarantee ya ufanisi, form six wakichemsha nao tutasema tupandishe tupate Ph.D, nao watashukuru kutoka jalalani na kuchemsha halafu itakuwaje?
Tuna tatizo lililozidi elimu rasmi. Tuna tatizo la utamaduni.
Ndiyo maana unaweza kukuta mtu ana Ph.D lakini maneno na matendo yake hayaendani na Ph.D.
Sasa ukishaelewa kwamba tuna matatizo ya utamaduni, kumnyima darasa la saba ubunge ni kutatua tatizo ambalo halipo.
Wabunge wetu wana underperform si kwa kukosa elimu rasmi. Wabunge wetu wana underperform kwa kufuata utamaduni wa kizamani wa hewala hewala.
Usomi ni zaidi ya usomi wa shule.
Na jamii isipoelimika, hata ukiweka wabunge wote wana elimu ya juu, kama hakuna wa kuwafuatilia na wa kuwashurutisha, wataishia kujipendelea wenyewe.
Tuna tatizo la utamaduni, tuna tatizo la elimu kwa jamii nzima.
Kama hatujaya address matatizo hayo, matatizo ya wabunhe dhaifu yataendelea tu.
Tukiya address matatizo hayo, matatizo ya wabunge dhaifu yataisha automatically, wabunge dhaifu hawataweza hata kupendekezwa na vyama vyao, vyama vitajua hawa hawatapata kura au approval ya wananchi.
Kwa sasa vyama vinaona wananchi wenyewe ni watu wa kupelekwapelekwa tu, wapewe wabunge wowote wale watawafaa tu.