Darasa la Saba na Ubunge

Darasa la Saba na Ubunge

Hawa jamaaa hawana impact yoyote kwa wananchi , hivi kweli Babu tale na yeye Mbunge anatakiwa aishauri na kuikosoa Serikali kweli?
Batu Tale nimemsikia mara moja akiongea bungeni alikuwa akiuliza swali la nyongeza. Ongea yake unaweza kujiuliza aliwa convince vipi wajumbe mpaka wakampa kura? Au kwa sababu ni memeja wa msanii?
 
Hata kama kaishia darasa la 3
Kama sijakosea kwenye katiba hawajataja kiwango cha elimu, wameandika aweze kusoma na kuandika.
Kwa maana hiyo hata kama hukuenda shule ila ukafundishwa kwa njia unazojua wewe ukaweza kusoma na kuandika una sifa za kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Ni kweli kabisa maana wakati mwingine uongozi ni kipaji.
Nilichokuwa nahoji hapa kwa nini mfanya usafi au dreva wa darasa la saba hapaswi kupewa kazi serikalini wakati kazi yake haihitaji kujieleza au kuongoza?
Serikali ina sifa zake inazozitaka kulingana na kazi, mahitaji na wakati. Mimi nawalaumu sana watumishi wanaokaa tu bila kujiendeleza mwisho wa siku wanajikuta hawana sifa kutokana na mahitaji ya wakati. Kwa upande wa Bunge sifa zao Mara nyingi zinatakiwa zimbebe kila mtu.
 
Dogo Serikali na Bunge ni vitu viwili tofauti ila vinategemeana. Sio lazima sifa za utumishi Serikalini zifanane na Sifa za Ubunge.
Una maana umeridhika na vigezo vya wabunge kuingia bungeni?
Acha kupotosha. Bunge ni sehemu nyeti isiyotaka akili za akina msukuma wewe.

Dunia hii ya sayansi msukuma atachangia nini kwa manufaa ya taifa?

Mambo ya uchumi na siasa za kimataifa Tale atachangia nini.....?

Infact wabunge wenye elimu ndogo muda wenu unakaribia. Mnalikwamisha taifa letu kwa makelele yenu ya kuwakosoa bila staha wabunge wasomi wanapotoa maoni yao ya kitaalamu.
 
Kanuni za kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge zinataka mgombea ajue walau Kuandika, Kusoma na Kuhesabu. Basi!
Acha hoja mfu zisizo na mashiko!
Yawezekana unatetea utopolo kwa vile na wewe ni walewale LY...!!
Kama Serikali imeweka masharti kuwa ili uwe mtumishi wa Umma kwa maana ya ajira Serikalini wakiwemo Wabunge na Watumishi wengine,lazima angalao uwe umemaliza F4 na uwe na Cheti au Diploma kwenye Taaluma fulani. Kwanini Mbunge awe na masharti tafauti? Hivi mshahara anaolipwa Mbunge hautokani na Kodi za Watz ? Hii kama siyo double standards ni kitu gani?

Kama swala ni kujua Kusoma na Kuandika kwanini basi hata kada na sehemu zingine nao wasiruhusiwe kuomba ajira kwa KIGEZO CHA KUJUA NA KUSOMA TU? Kwanini nchi moja hii ya Tanzania iwe na vigezo tofauti? AJIRA BUNGENI MINIMUM REQUIREMENTS CLASS 7, AJIRA
SEHEMU ZINGINE ZOTE LAZIMA UWE NA ASTASHAHADA, SHAHADA NA KUENDELEA.....? What a double standard is this?
 
Habari wanajukwaa,

Nimekuwa nikijiuliza Maswali mengi sana juu ya utumishi wa wabunge ambao ni darasa la saba. Muongozo wa ajira Serikalini ni kwamba wanaajiri kuanzia kidato cha nne na kuendelea, kama huna cheti cha form four huna sifa ya kuwa mtumishi wa umma.

Ninavyoelewa mimi inawezekana isiwe hivyo, mtumishi wa umma ni yule anayelipwa mshahara wake na serikali (kupitia kodi za wananchi). Kama serkali iliamua kuwatoa kwenye ajira watumishi wake ambao walikuwa na elimu ya darasa la saba, kwa nini wabunge wa darasa la saba hawakuguswa ili hali nao ni watumishi wa umma.

Mtumishi aliyekuwa dreva au mfanya usafi akaondolewa kwenye ajira kwa sababu ya darasa la saba, serkali haioni kuwa ilimuonea mtu huyo wakati kuna mbunge ambaye ana majukumu makubwa ya kitaifa ikiwamo kutunga sheria na kuishauri serikali. Utampate kazi mtu wa darasa la saba ya kutunga sheria na kushauri serkali wakati huohuo mfanya usafi na dreva ambaye anatolewa kwenye ajira kwa elimu ileile ya darasa la saba.

Serikali ipitie upya hii mifumo na ikiwezekana waongeze ufaulu wa elimu kuwa na sifa ya kugombea ubunge angalau iende mpaka kidato cha sita au stashahada (Diploma).
Hata mimi nilikuwaga najiuliza hivi darasa la saba anaenda kufanya nini bungeni?
Lakini baada ya kuwa nafuatilia michango ya darasa la saba King Msukuma, Kishimba, Lusinde(Kibajaji) Vs michango ya wasomi kama kina Prof Muhongo ,Lisu, Lema, Msigwa etc

Nimegundua darasa la saba wanatakiwa wawe wengi bungeni ili wawe wanatoa maagizo alafu wasomi wanatekeleza.

Darasa la saba huwa wanazungumzia uhalisia wa maisha ya mtanzania na hata wakitoa solution huwa inaendana na maisha ya watanzania lakini wasomi huwa wako bize kutoa theories tu na hata wakitoa solution huwa haziendani na maisha ya mtanzania, mara nyingi huwa wanahisi wanaongoza taifa kama Sweden!!!

Ni bora ushinde ukisikiliza mchango wa Kishimba kuliko kutumia dakika moja ukisikiliza mchango wa Tundu Lisu.
 
Habari wanajukwaa,

Nimekuwa nikijiuliza Maswali mengi sana juu ya utumishi wa wabunge ambao ni darasa la saba. Muongozo wa ajira Serikalini ni kwamba wanaajiri kuanzia kidato cha nne na kuendelea, kama huna cheti cha form four huna sifa ya kuwa mtumishi wa umma.

Ninavyoelewa mimi inawezekana isiwe hivyo, mtumishi wa umma ni yule anayelipwa mshahara wake na serikali (kupitia kodi za wananchi). Kama serkali iliamua kuwatoa kwenye ajira watumishi wake ambao walikuwa na elimu ya darasa la saba, kwa nini wabunge wa darasa la saba hawakuguswa ili hali nao ni watumishi wa umma.

Mtumishi aliyekuwa dreva au mfanya usafi akaondolewa kwenye ajira kwa sababu ya darasa la saba, serkali haioni kuwa ilimuonea mtu huyo wakati kuna mbunge ambaye ana majukumu makubwa ya kitaifa ikiwamo kutunga sheria na kuishauri serikali. Utampate kazi mtu wa darasa la saba ya kutunga sheria na kushauri serkali wakati huohuo mfanya usafi na dreva ambaye anatolewa kwenye ajira kwa elimu ileile ya darasa la saba.

Serikali ipitie upya hii mifumo na ikiwezekana waongeze ufaulu wa elimu kuwa na sifa ya kugombea ubunge angalau iende mpaka kidato cha sita au stashahada (Diploma).
Wabunge ni wanasiasa.Usilinganishe wanasiasa (politicians) na watumishi wa umma (civil servants). Hawa wawili wanawajibika tofauti. Wanasiasa wanawajibika kwenye vyama vyao na wapiga kura wao. Watumishi wa umma wanawajibika kwa Katibu Mkuu Kiongozi. Hata sifa zao za kupata kazi ni tofauti.

Wanasiasa mtihani wao ni kutongoza wapiga kura wawapigie kura.

Katika demokrasia ya kweli, huo ni mtihani mkubwa kuliko Ph.D.

Tunachotakiwa kufanya ni.

1. Kuongeza wigo wa elimu kwa jamii.
2. Kuongeza demokrasia ya kweli.

Baada ya hapo, kama wabunge wa darasa la saba hawafai, wananchi watawachuja kwenye chaguzi.

Mimi nina tatizo unapomsakama mbunge wa darasa la saba kwamba hana uwezo wa kuwakilisha wananchi vizuri, wakati, in principle kachaguliwa na wananchi.

Naweza kusikiliza hoja hii zaidi kwenye wabunge wa kuteuliwa. Hawa hata wakiondolewa kabisa wote sina tatizo.

Tatizo la kuongeza kiwango cha elimu kwenye ubunge ni kuibana demokrasia.

Kwa sababu kimsingi kikatiba karibu watu wote wenye umri unaotakiwa wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa uongozi.

Sasa ukianza kuweka viwango vya elimu vya "diploma" ama form six kwenye ubunge, unawanyima wa darasa la saba uwakilishi.

Ni kama vile useme watu walioishia darasa la saba wasipige kura, kwa sababu hawana elimu ya kuchambua mambo. Haki ya kuchagua na kuchaguliwa uongozi zinashabihiana kwa mengi.Ukikataza darasa la saba wasiwe wabunge, utakataza darasa la saba wasipige kura pia?

Wamarekani bunge lao (Senate) halina kiwango cha elimu. Katiba inataja masharti ya umri (miaka 30), uraia wa Marekani kwa angalau miaka 9 na makazi katika jimbo wakati wa uchaguzi huo.

Hakuna sharti la elimu.

Kwa nini? Wananchi wenyewe wataamua kama huyu mtu ameelimika vya kutosha kuwa Senator ama la.

Pia, viwango hivi ni vitu ambavyo havina guarantee ya ufanisi, form six wakichemsha nao tutasema tupandishe tupate Ph.D, nao watashukuru kutoka jalalani na kuchemsha halafu itakuwaje?

Tuna tatizo lililozidi elimu rasmi. Tuna tatizo la utamaduni.

Ndiyo maana unaweza kukuta mtu ana Ph.D lakini maneno na matendo yake hayaendani na Ph.D.

Sasa ukishaelewa kwamba tuna matatizo ya utamaduni, kumnyima darasa la saba ubunge ni kutatua tatizo ambalo halipo.

Wabunge wetu wana underperform si kwa kukosa elimu rasmi. Wabunge wetu wana underperform kwa kufuata utamaduni wa kizamani wa hewala hewala.

Usomi ni zaidi ya usomi wa shule.

Na jamii isipoelimika, hata ukiweka wabunge wote wana elimu ya juu, kama hakuna wa kuwafuatilia na wa kuwashurutisha, wataishia kujipendelea wenyewe.

Tuna tatizo la utamaduni, tuna tatizo la elimu kwa jamii nzima.

Kama hatujaya address matatizo hayo, matatizo ya wabunhe dhaifu yataendelea tu.

Tukiya address matatizo hayo, matatizo ya wabunge dhaifu yataisha automatically, wabunge dhaifu hawataweza hata kupendekezwa na vyama vyao, vyama vitajua hawa hawatapata kura au approval ya wananchi.

Kwa sasa vyama vinaona wananchi wenyewe ni watu wa kupelekwapelekwa tu, wapewe wabunge wowote wale watawafaa tu.
 
Wamewaondoa darasa la saba kutoendelea na utumishi wa uma ilihali katiba iko vilevile kuwa mtu yeyote mwenyekujua kusoma na kuandika anafaa kuwaajiriwa katika utumishi wa uma sasa sielewi wametumia katiba ya wapi kuwafuta KAZI watumishi jaws wa darasa la saba
 
Serikali ina sifa zake inazozitaka kulingana na kazi, mahitaji na wakati. Mimi nawalaumu sana watumishi wanaokaa tu bila kujiendeleza mwisho wa siku wanajikuta hawana sifa kutokana na mahitaji ya wakati. Kwa upande wa Bunge sifa zao Mara nyingi zinatakiwa zimbebe kila mtu.
Ndo mpaka kwenye kufagia? wakati mtunga sheria hawekewi vigezo
 
Una maana umeridhika na vigezo vya wabunge kuingia bungeni?
Acha kupotosha. Bunge ni sehemu nyeti isiyotaka akili za akina msukuma wewe.

Dunia hii ya sayansi msukuma atachangia nini kwa manufaa ya taifa?

Mambo ya uchumi na siasa za kimataifa Tale atachangia nini.....?

Infact wabunge wenye elimu ndogo muda wenu unakaribia. Mnalikwamisha taifa letu kwa makelele yenu ya kuwakosoa bila staha wabunge wasomi wanapotoa maoni yao ya kitaalamu.
Watu bado hawajajua umuhimu wa kuwa mbunge. Kwa kuwa ipo hivyo acha tuendelee hivyohivyo
 
Habari wanajukwaa,

Nimekuwa nikijiuliza Maswali mengi sana juu ya utumishi wa wabunge ambao ni darasa la saba. Muongozo wa ajira Serikalini ni kwamba wanaajiri kuanzia kidato cha nne na kuendelea, kama huna cheti cha form four huna sifa ya kuwa mtumishi wa umma.

Ninavyoelewa mimi inawezekana isiwe hivyo, mtumishi wa umma ni yule anayelipwa mshahara wake na serikali (kupitia kodi za wananchi). Kama serkali iliamua kuwatoa kwenye ajira watumishi wake ambao walikuwa na elimu ya darasa la saba, kwa nini wabunge wa darasa la saba hawakuguswa ili hali nao ni watumishi wa umma.

Mtumishi aliyekuwa dreva au mfanya usafi akaondolewa kwenye ajira kwa sababu ya darasa la saba, serkali haioni kuwa ilimuonea mtu huyo wakati kuna mbunge ambaye ana majukumu makubwa ya kitaifa ikiwamo kutunga sheria na kuishauri serikali. Utampate kazi mtu wa darasa la saba ya kutunga sheria na kushauri serkali wakati huohuo mfanya usafi na dreva ambaye anatolewa kwenye ajira kwa elimu ileile ya darasa la saba.

Serikali ipitie upya hii mifumo na ikiwezekana waongeze ufaulu wa elimu kuwa na sifa ya kugombea ubunge angalau iende mpaka kidato cha sita au stashahada (Diploma).
Unaweza kuwa darasa la saba na ukaongea vizuri,mbona tabasamu mbunge wa sengerema ni darasa la 7 lakini anaongea vizuri sana
 
Kanuni zitabadilishwa na nani? Kama tutategemea mabadiliko kupitia Bunge itakuwa ni ndoto za Alinacha.
Tatizo siku hizi wanaharakati wamekuwa wapole sana, wana wajibu wa kuanzisha mijadala kama hii
 
Kanuni za kugombea nafasi za Udiwani na Ubunge zinataka mgombea ajue walau Kuandika, Kusoma na Kuhesabu. Basi!
Hii mbona ni sifa ya Elimu ya Vidudu yaani KKK(K-3)? Kusoma, Kuandika na Kuhesabu. Shame on you CCM Goverment!!
 
Kwamba wenye elimu wamefanya nini?,....huoni msukuma anavyoshauri kuliko wenye elimu
 
Unaweza kuwa darasa la saba na ukaongea vizuri,mbona tabasamu mbunge wa sengerema ni darasa la 7 lakini anaongea vizuri sana
Kuongea vizuri ndiyo kitu gani? Hujaona mtu anaongea vizuri lakini hajawahi kuchungulia hata darasani? Hoja hapa ni Elimu ya kuweza kudadavua maswala nyeti ya Kibunge, Kitaifa na Kimataifa. Hatutaki mbunge mwene Elimu ya kutukana Watu kwa vile tu wako Chama pinzani au wanao mzidi elimu!!!

Nashauri Wabunge wasomi wapeleke hoja binafsi na Serikali ilete muswada Bungeni mara moja ili kubadili Sheria ya kuomba kugombea Ubunge angalao minimum Qualificatoon iwe at least Certificate au Diploma kwene Taaluma yoyote kama ilivo kwa Ajira zote Serikalini.
A BIG NO TO CLASS 7.
 
Kuwa msomi wa elimu rasmi si guarantee ya ufanisi.

Mfano:-

Tumekuwa na Rais mwenye Ph.D ya sayansi lakini kakataa chanjo na barakoa.

Unataka kutatua tatizo ambalo halipo wakati tatizo lililopo hutatui.

Rejea post yangu namba 29 hapo juu.
 
Kwamba wenye elimu wamefanya nini?,....huoni msukuma anavyoshauri kuliko wenye elimu
Huyu msukuma anashauri vitu vinavyoonekanana papo kwa papo hasa kukosoa wenzake na kuchangia hoja general sio zile za kiutafiti, hana uwezo wa kujenga hoja au kuanzisha hoja binafsi yenye mashiko kwa taifa.
 
Kuwa msomi wa elimu rasmi si guarantee ya ufanisi.

Mfano:-

Tumekuwa na Rais mwenye Ph.D ya sayansi lakini kakataa chanjo na barakoa.

Unataka kutatua tatizo ambalo halipo wakati tatizo lililopo hutatui.

Rejea post yangu namba 29 hapo juu.
Natilia shaka sana elimu yako na ufahamu ulio nao.
Kama elimu tunazo soma siyo guarantee ya efficiency kazini kwanini Serikali inahangaika kujenga Shule, Vyuo vya Kati, Vyuo Vikuu n.k ili Taifa liwe na Wasomi/Wataalamu hatimae nchi iwe na maendeleo na kujikomboa kiuchumi?

Kuwa na Rais mwenye PhD ya sayansi na kukataa chanjo na barakoa ni hulka au ujinga wake tu! Fikiria kama huyu PhD holder ya Sayansi angelikuwa ni PhD holder "ya MEDICINE things could've been quite different! Asingelichukua huo uamzi wa kijinga na very likely angelikuwa hai leo!

Jiulize huyu PhD wa sayansi ya Kemia na Hesabu alichagua Madaktari kwenye lile Jopo la Kamati iliyofuatilia ISSUE YA MAKINIKIA? Kwanini hatukuwaona hao kina kibajaj na Musukuma kwenye hizo Kamati???
Tuacheni kuspotosha maswala nyeti kama haya please!
 
Back
Top Bottom