Darasa la Saba na Ubunge

Darasa la Saba na Ubunge

Natilia shaka sana elimu yako na ufahamu ulio nao.
Kama elimu tunazo soma siyo guarantee ya efficiency kazini kwanini Serikali inahangaika kujenga Shule, Vyuo vya Kati, Vyuo Vikuu n.k ili Taifa liwe na Wasomi/Wataalamu hatimae nchi iwe na maendeleo na kujikomboa kiuchumi?

Kuwa na Rais mwenye PhD ya sayansi na kukataa chanjo na barakoa ni hulka au ujinga wake tu! Fikiria kama huyu PhD holder ya Sayansi angelikuwa ni PhD holder "ya MEDICINE things could've been quite different! Asingelichukua huo uamzi wa kijinga na very likely angelikuwa hai leo!

Jiulize huyu PhD wa sayansi ya Kemia na Hesabu alichagua Madaktari kwenye lile Jopo la Kamati iliyofuatilia ISSUE YA MAKINIKIA? Kwanini hatukuwaona hao kina kibajaj na Musukuma kwenye hizo Kamati???
Tuacheni kuspotosha maswala nyeti kama haya please!

Wewe unayejinasibu na elimu hata huelewi level ya elimu ya Ph.D ni nini, ndiyo maana unaandika habari za kumtetea mtu mwenye Ph.D ya Kemia kushindwa kujua mambo ya medicine kwa sababu hana Ph.D ya medicine.

Hujui kwamba kwa level ya Ph.D hata ya literature tu, kujua umuhimu wa chanjo na barakoa ni jambo basic.

Sasa unahoji elimu yangu wakati wewe mwenyewe hujui elimu ni nini na Ph.D ni nini.

Halafu unaji contradict, inaonekana bila kujua. Kwa sababu huwezi kutumia mantiki katika kufikiri.

Kimsingi umekubali kwamba mtu mwenye Ph.D ya sayansi anaweza kuwa na hulka ya ujinga.

Hivyo Ph.D si guarantee ya kuzuia hulka ya ujinga.

Na hivyo, hoja ya kudhibiti ujinga kwenye bunge kwa kupandisha kiwango cha elimu ni hoja mufilisi.

Nakwambia hivi, bila kuongeza kiwango cha elimu kwa jamii, unaweza kuwa na bunge limejaa wasomi likaona wananchi wajinga hakuna wa kuwafuatilia wakiiba.

Bunge la wabunge wasomi watupu likakubaliana kuiba na kudanganya wananchi wajinga.

Hapo bunge lako la wasomi halijakusaidia.

Kinachotakiwa ni kuongeza level ya elimu kwa jamii nzima.

Ukifanya hivyo, automatically wabunge wasio na elimu watatoweka.

Marekani hawana kiwango cha elimu bunge lao.

Lakini hawana mbunge wa darasa la saba.

Kwa nini?

Wananchi wanajua kuchuja wabunge wasio na elimu. Wanawachuja. Mbunge asiye na elimu hata kupata nomination ya chama tu hapati.

Wewe unataka nchi ambayo imejaa wananchi walioishia darasa la saba isiwe na mbunge aliyeishia darasa la saba?

Halafu useme hilo bunge lina uwakilishi halisi wa wananchi?

Unataka kuponya ugonjwa kwa kutibu dalili.

Udhaifu wa wabunge wetu kielimu si ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa.

Ugonjwa ni udhaifu wa elimu katika jamii.

Sasa, hapa unachofanya ni kutaka kumtibu mgonjwa wa kifua kikuu kwa kumoa dawa ya kikohozi ya Cofta.

Huwezi kutibu kifua kikuu kwa dawa ya kupoza kikohozi ya Cofta.
 
Habari wanajukwaa,

Nimekuwa nikijiuliza Maswali mengi sana juu ya utumishi wa wabunge ambao ni darasa la saba. Muongozo wa ajira Serikalini ni kwamba wanaajiri kuanzia kidato cha nne na kuendelea, kama huna cheti cha form four huna sifa ya kuwa mtumishi wa umma.

Ninavyoelewa mimi inawezekana isiwe hivyo, mtumishi wa umma ni yule anayelipwa mshahara wake na serikali (kupitia kodi za wananchi). Kama serkali iliamua kuwatoa kwenye ajira watumishi wake ambao walikuwa na elimu ya darasa la saba, kwa nini wabunge wa darasa la saba hawakuguswa ili hali nao ni watumishi wa umma.

Mtumishi aliyekuwa dereva au mfanya usafi akaondolewa kwenye ajira kwa sababu ya darasa la saba, serikali haioni kuwa ilimuonea mtu huyo wakati kuna mbunge ambaye ana majukumu makubwa ya kitaifa ikiwamo kutunga sheria na kuishauri serikali. Utampate kazi mtu wa darasa la saba ya kutunga sheria na kushauri serkali wakati huohuo mfanya usafi na dreva ambaye anatolewa kwenye ajira kwa elimu ileile ya darasa la saba.

Serikali ipitie upya hii mifumo na ikiwezekana waongeze ufaulu wa elimu kuwa na sifa ya kugombea ubunge angalau iende mpaka kidato cha sita au stashahada (Diploma).
Nani alikudanganya kama mbunge ni mtumishi wa umma ? Kwa taarifa yako mbunge hayumo katika mfumo wa utumishi wa umma bali ni mwakilishi wa wananchi katika Bunge. Yeye ni mwanasiasa hafungwi na taratibu za utumishi wa umma ambao ukifikisha miaka 60 lazima ustaafu. Mbunge anaweza hata akawa na umri wa miaka 80 bado akawa mbunge. Ninaunga mkono hoja kwamba kutokana na maendeleo makubwa katika ulimwengu wa leo kuna haja ya kupitisha sheria angalau mbunge awe na elimu ya kidato cha nne.
 
Wewe unayejinasibu na elimu hata huelewi level ya elimu ya Ph.D ni nini, ndiyo maana unaandika habari za kumtetea mtu mwenye Ph.D ya Kemia kushindwa kujua mambo ya medicine kwa sababu hana Ph.D ya medicine.

Hujui kwamba kwa level ya Ph.D hata ya literature tu, kujua umuhimu wa chanjo na barakoa ni jambo basic.

Sasa unahoji elimu yangu wakati wewe mwenyewe hujui elimu ni nini na Ph.D ni nini.

Halafu unaji contradict, inaonekana bila kujua. Kwa sababu huwezi kutumia mantiki katika kufikiri.

Kimsingi umekubali kwamba mtu mwenye Ph.D ya sayansi anaweza kuwa na hulka ya ujinga.

Hivyo Ph.D si guarantee ya kuzuia hulka ya ujinga.

Na hivyo, hoja ya kudhibiti ujinga kwenye bunge kwa kupandisha kiwango cha elimu ni hoja mufilisi.

Nakwambia hivi, bila kuongeza kiwango cha elimu kwa jamii, unaweza kuwa na bunge limejaa wasomi likaona wananchi wajinga hakuna wa kuwafuatilia wakiiba.

Bunge la wabunge wasomi watupu likakubaliana kuiba na kudanganya wananchi wajinga.

Hapo bunge lako la wasomi halijakusaidia.

Kinachotakiwa ni kuongeza level ya elimu kwa jamii nzima.

Ukifanya hivyo, automatically wabunge wasio na elimu watatoweka.

Marekani hawana kiwango cha elimu bunge lao.

Lakini hawana mbunge wa darasa la saba.

Kwa nini?

Wananchi wanajua kuchuja wabunge wasio na elimu. Wanawachuja. Mbunge asiye na elimu hata kupata nomination ya chama tu hapati.

Wewe unataka nchi ambayo imejaa wananchi walioishia darasa la saba isiwe na mbunge aliyeishia darasa la saba?

Halafu useme hilo bunge lina uwakilishi halisi wa wananchi?

Unataka kuponya ugonjwa kwa kutibu dalili.

Udhaifu wa wabunge wetu kielimu si ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa.

Ugonjwa ni udhaifu wa elimu katika jamii.

Sasa, hapa unachofanya ni kutaka kumtibu mgonjwa wa kifua kikuu kwa kumoa dawa ya kikohozi ya Cofta.

Huwezi kutibu kifua kikuu kwa dawa ya kupoza kikohozi ya Cofta.
Hueleweki!
Wewe ndo unaji contradict! Uko upande upi sasa? Upande unatetea la 7 na upande unatetea PhD....!!!
Kama ugonjwa ni UDHAIFU wa Elimu katika jamii unataka kutuambia Wasomi wote Tanzania Doctors na PhD holder Elimu yao Ni questionable? Kumbuka kuna Watz wamesoma nje ya Tanzania na Wana perform wonders!
Ningekubaliana na wewe kama ungelisema UDHAIFU WA TANZANIA NI CCM NA KATIBA MBOVU YA NJI HII.
Ndiyo maana PhD holder akishakuwa Mwanasiasa PhD anaweka pembeni anaanza kucheza ngoma ya CCM na KUDEMKA KWA SANA.
Ndo maana Watz wanasema tumeruhusu AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA...!
Maana Serikali ya CCM inawaruhusu Darasa la Saba kuingia Bungeni kuwatukana Professors na Spika Ndugai mwenye Digrii ya 1&2 anawaruhusu na kuwaongezea dakika. Shame!!
 
Umenifurahisha sana namna ulivyo 'react' nadhani jamaa kakuita hivyo kutokana na 'umri' wa id yako hapa jukwaani.
Yaani jamaa ananiita dogo wakati hatufahamiani. Kwamba yeye ni senior kwa sababu account yake ina umri mkubwa?
 
Nafasiza kuchaguliwa katika sanduku la kura mara nyingi wanaochaguliwa wanachaguliwa si kwa sababu ya elimu zao ni jinsi ambavyohawa wanaochaguliwa wa anamchamgo katika hio jamii, Usidhani kwamba ukiwa na Elimu ya chuo kikuu basi ukienda mahali popote utachaguliwa, Hapana, Hali ya mtaani wanaijua wanaokaa huko ndio maana hao darasa la saba wanachaguliwa halafu wewe na vyeti vyako unaibuka ziro.
 
Hueleweki!
Wewe ndo unaji contradict! Uko upande upi sasa? Upande unatetea la 7 na upande unatetea PhD....!!!
Kama ugonjwa ni UDHAIFU wa Elimu katika jamii unataka kutuambia Wasomi wote Tanzania Doctors na PhD holder Elimu yao Ni questionable? Kumbuka kuna Watz wamesoma nje ya Tanzania na Wana perform wonders!
Ningekubaliana na wewe kama ungelisema UDHAIFU WA TANZANIA NI CCM NA KATIBA MBOVU YA NJI HII.
Ndiyo maana PhD holder akishakuwa Mwanasiasa PhD anaweka pembeni anaanza kucheza ngoma ya CCM na KUDEMKA KWA SANA.
Ndo maana Watz wanasema tumeruhusu AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA...!
Maana Serikali ya CCM inawaruhusu Darasa la Saba kuingia Bungeni kuwatukana Professors na Spika Ndugai mwenye Digrii ya 1&2 anawaruhusu na kuwaongezea dakika. Shame!!
Wewe unaandika kama simpleton.

Hata kuelewa set theory tu tofauti ya union, intersection, compliment, kuelewa abstract tu huelewi.

Kwani nikisema darasa la saba anaruhusiwa kugombea ubunge ndiyo nimemkataza huyo Ph.D aliyesoma nje asigombee ubunge?

Mbona reasoning yako ni poor sana kwa mtu anayetetea elimu?

Nilitegemea mtu anayetetea elimu atuoe rrason ya kielimu yenye mantiki, siyo hii yako inayoprotest kitu ambacho hakina merit ya ku protest.

Unajua kufikiri kwa mantiki?

Unaelewa kwamba darasa la saba wakiruhusiwa kugombea ubunge wenye Ph.D hawajakatazwa?

Unaelewa kwamba mimi sijaleta hoja ya kusema "zuieni watu wenye Ph.D kuwa wabunge, wabunge wawe walioishia darasa la saba tu". Ninasema walioishia darasa la saba wapewe uhuru wa kugombea ubunge sawa na Ph.D, wananchi waamue nani anafaa?

Sasa mbona unanipa mzigo usio wangu kama vike nimesema Ph.D wasigombee ubunge, wagombee darasa la saba tu?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Ngoja nijaribu tena kukueleza.

1. Kwanza kabisa naomba uelewe kwamba mimi si mpinga elimu. Mimi ni mpenda elimu. Ila naelewa kitu kinaitwa "the law of unintended consequences" na "the road to hell is paved with good intentions". Jaribu kusoma hizo habari kama una uwezo.

Things are counterintuitive sometimes.

Ma korti ya Wafalme wa Ulaya tulikogeza hii elimu rasmi ya vyeti walihitaji "Court Jesters". Hawa si wasomi. Hawa ni wasanii wa kuchekesha tu. Na katika korti hizo, mtu yeyote alikuwa hatakiwi kumsema Mfalme vibaya, wasomi wote wakimsema Mfalme vibaya walikuwa wanauawa.

Ila huyo mchekeshaji ambaye si msomi ndiye mtu aliyekuwa anaruhusiwa kumsema mfalme kwa lolote.

Kwa sababu huyo ndiye alikuwa ana uwezo wa kumuambia mfalme mabaya yake, halafu mfalme akayafanyia kazi bila kujisikia vibaya kwamba amekosolewa na wasomi.

Kwa hiyo hawa "court jesters" wana sehemu zao katika jamii toka huko tulikogeza haya mabunge yetu.

Nimekuuliza swali hujalijibu

Ukipewa bunge lililojaa wasomi wa Ph.D, wanaojua wananchi ni wajinga na hawawezi kuwafuatilia, wasomi wakaiba na kudanganya watu, bunge hilo la wasomi litakufaidisha vipi? Hujajibu.

2. Elimu haiishii kwenye elimu rasmi. Kuna watu wana elimu rasmi na hawajaelimika, na pia kuna watu hawana elimu rasmi ila wameelimika.

Hawa wengine kiingereza wanaitwa "autodidact". Watu wanaojifunza wenyewe.

3. Kuwa na elimu rasmi kubwa mara nyingine si alama ya kuwa na akili au uwezo sana. Inawezekana ni alama ya kuwa na access ya elimu (mtu wa kukulipia ada, kutoka familia iliyowahi kusoma etc).

Rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva hana degree.Ila watu wanampenda sana kwa uongozi wake mpaka wanamtaka arudi kuwa rais agombee tena.

Akiulizwa, kwa nini yeye hana degree, atajibu mimi familia yetu haikuwa na uwezo, nikianza kufanya kazi nikiwa mdogo, huko kazini nikaonekana kipaji changu cha uongozi nikapanda kwenye kuongoza vyama vya wafanyakazi.

Atasema elimu niliyoipata kwenye kuongiza vyama vya wafanyakazi haifundishwi katika degree yoyote. Mitihani niliyopambana nayo katika figusu za siasa za vyama vya wafanyakazi ni mitihani practical ambayo haina shule popote.

Ukimnyima ubunge au urais mtu kama huyu, ukampa mtu mwenye Ph.D na hulka ya ujinga, utakuwa umeji shortchange mwenyewe.

4. Hakuna shortcut ya kutatua tatizo la elimu bungeni. Kitu kinachotakiwa kufanywa nibkuongeza elimunkwa jamii nzima, ili jamii ijue kuwachekecha wagombea. Hili kitafanya tupate kile kinachoitwa "the best of both worlds.

5. Demokrasia ya kweli ninike ambayo haiweki vizingiti vingi kwa watu wanaotakq kuongiza. Kizingiti cha kweli kinatakiwa kiwe kukubalika na wananchi.

Unaweza kuwaletea watu kiongozi msomi sana wa elimubrasmi, lakini hajui lugha yao hao watu, akashindwa kuwasiliana nao, kwa sababu yuko tofauti sana nao.

Wakati kuna mtu mwingine hajasima sana kwa elimu rasmi, ika anawaelewa wale watu na matatizo yao na anaweza kuwasikiana nao na kuwaongoza vizuri zaidi.

Nasema kwamba, ikiwa kuna mtu ana kipaji cha uongozi, ila kwa sababu ya masahibu ya maisha tu hakupata vyeti vikubwa, labda alifiwa na wazazi mapema akakosa wa kumsomesha, au aliumwa macho siku ya mtihani wa mwisho akafeli, basi wananchi waweze kuujua uwezo wake na kumchagua awawakilishe. Kusiwe na vigezo vikubwa vya elimu kwenye ubunge kumnyanyapaa huyu.

Vivyo hivyo, kukiwa na mtu ana Ph.D, lakini maneno yake hayaendani na Ph.D, anasema amneno ya ovyo ovyo tu, mara awaqmbue watu wabaki na mavi yao majumbani mwao wasichqfue vyoo vya serikali, mara anakataa chanjo na barakoa, wananchi waweze kujua huyu hamnazo, na labda Ph.D yake kasaidiwa tu, wamkatae.

Ukitaka kazi ya wananchi ya kuchekecha viongozi ifanywe na vyeti vya elimu rasmi unaweza kukosea katika sehemu mbili hizi.

Unaweza kumkataa mtu ambaye ana uwezo wa kuongoza, ila, kutokana na matatizo fulani tu hakusoma kupata vyeti. Labda kasoma kwa uzoefu wa kazini au kujisomea vitabu mwenyewe.

Hili moja.

Lakini la pili, ukiangalia elimu kama ni vyeti, kilimbukeni, matokeo yake ndiyo hayo utaishia kumchagua mtu mwenye Ph.D kwa kufikiri Ph.D ndiyo guarantee ya uongozi bora, halafu huyo mwenye Ph.D akashindwa hata kuongea kwa staha, akakwambia baki nyumbani na mqvi yako usichqfue vyoo vya serikali.

Watanzania wengi wanasumbukiwa nanukimbukeninwa elimu.

Ulimbukeni wa elimu ndio unawafanya watu waone kwamba elimu maananyake ni vyeti.

Wakati kuna elimu kubwa sana isiyo na vyeti.
 
Nafasiza kuchaguliwa katika sanduku la kura mara nyingi wanaochaguliwa wanachaguliwa si kwa sababu ya elimu zao ni jinsi ambavyohawa wanaochaguliwa wa anamchamgo katika hio jamii, Usidhani kwamba ukiwa na Elimu ya chuo kikuu basi ukienda mahali popote utachaguliwa, Hapana, Hali ya mtaani wanaijua wanaokaa huko ndio maana hao darasa la saba wanachaguliwa halafu wewe na vyeti vyako unaibuka ziro.
Watanzania wengine bado wana haya

1.Wana ulimbukeni fulani wa elimu wa kufikiri kwamba elimu rasmi ndiyo mwisho wa elimu.

2. Wananapenda kurahisisha mambo complex yenye sura mbalimbali tofauti. Suala complex la elimu ni nini wamelitafutia convenient shortcut kwamba"elimu ni vyeti, ukifanikiwa kununua vyeti vikakubalika wewe una elimu" na hata kama umegundua nini, kama huna vyeti wewe huna elimu.

3. Hatujifunzi kwa watu walioelimika. Bunge la Senate Marekani, nchi iliyotuzidi sana kielimu kwa hii elimu rasmi, halina sharti lolote la kielimu kuwa mbunge. Masharti ni kufikisha miaka 30, kuwa raia wa Marekani kwa miaka 9 na kuwa mkazi wa jimbo unalotaka kuwakilisha wakati wa uchaguzi. Sasa sie tulioanza kupata elimu rasmi juzi hapa tunataka kujifanya tunaijua sana kuliko huko kwa wenzetu walioianzisha?

4. Hawako sensitive katika suala zima la kunyanyapaa watu. Kuna watu wengi hawajasoma sana lakini wana uwezo mkubwa, tatizo mfumo uliopo hauwafai watu waadilifu, unawafaa watu wasio na maadili, wezi wezi, wanaotumia rushwa na uongo. Sasa hapo mtu aliyeishia darasa la saba na Chenge aliyesoma Harvard wote watapata ubunge, Chenge atafanya mambo ambayo ni kinyume na usomi, atawaibia wananchi na kuweka vijisenti visiwa vya Jersey, na kusema hivyo ni vijisenti tu. Wananchi watamuogopa kwa kuwa ni msomi, wengine watamsifia. Lakini mtu wa darasa la saba akichemsha kwenye kuchangia, hata kabla hajaiba, ataumbuliwa kwa kuwa ni darasa la saba.Hapo unamuonea tu huyu darasa la saba, bunge zima linanuka, huyu anashindwa kuwa kiongozi mzuri si kwa sababu ni mtu wa darasa la saba, anashindwa kuwa kiongozi mzuri kwa sababu mfumo wetu wa uongozi hauruhusu mtu mwenye maadili kupanda ngazi. Ukiwa hutaki rushwa na uongo hata chama hakiwezi kukupendekeza kuwa mbunge. Sasa wabunge wakifeli, wanaoonekana wamefeli ni darasa la saba, kwa sababu ya elimu yao.Kumbe bunge zima linanuka, kwa sababu kuanzia wasomi wa elimu rasmi mpaka darasa la saba wote wame kuwa compromised na process nzima ya kupata ubunge.

5. Hawaelewi kuwa tatizo letu ni kuwa nchi haina inclusivity, nchi ina exclusivity, hatuna diversity of thought.Hao wasomi wanaosemwa wamejaa kwenye cabinet na Ph.Ds zao, lakini waliishia kuimba sifa na pambio kwa msomi kichaa Magufuli. Hakuna msomi hata mmoja aliyejiuzulu kazi yake kwa kutetea kanuni zake za kisomi zilizoharibiwa na Magufuli.

Sasa hao ni wasomi au wanaigiza kuwa wasomi?

Tuongeze elimu kwa wote, tuongeze demokrasia halisi. Tusiongeze vikwazo vya watu kuwa wabunge.

Marekani hakuna kikwazo cha elimu kwa mtu kuw mbunge, na hawana mbunge aliyeishia primary school as far as I know.

Kwa nini?

Kwa sababu wananchi wana muamko, usomi wa formal education ni kitu cha kawaida tu, wananchi wanajua kuchuja viongozi, na hata kiongozi mwenye uzoefu tribal leader wa Indigenous Indians ambaye hajasoma formal education, lakini ana uzoefu mzuri kutoka kabila lake anaweza kuchangia bungeni, akigombea ubunge, wanawez akumpa nafasi.

Kwa nini tuna ji limit? Kwa nini tunataka demokrasia itakayowabagua sehemu kubwa ya Watanzania? Kwa nini hatuelimishi watu ili wajue kuchuja wenyewe kiasi kwamba mtu mzugaji yeyote, awe na Ph.D au darasa la saba, asipate nafasi?

Kwa nini tunataka kutumia vyeti kama shortcut ya kujua nani anafaa na nani hafai wakati vyeti vyenyewe vingi ni vya kununua na kusaidiwa tu?
 
Nani alikudanganya kama mbunge ni mtumishi wa umma ? Kwa taarifa yako mbunge hayumo katika mfumo wa utumishi wa umma bali ni mwakilishi wa wananchi katika Bunge. Yeye ni mwanasiasa hafungwi na taratibu za utumishi wa umma ambao ukifikisha miaka 60 lazima ustaafu. Mbunge anaweza hata akawa na umri wa miaka 80 bado akawa mbunge. Ninaunga mkono hoja kwamba kutokana na maendeleo makubwa katika ulimwengu wa leo kuna haja ya kupitisha sheria angalau mbunge awe na elimu ya kidato cha nne.
Hata kama si watumishi wa umma kwa kuwa wanalipwa mshahara na serikali wanatakiwa kwenda sambamba na sera za utumishi
 
mheshimiwa rais tunakuomba hili swala uliongelee katika hotuba yako bungeni,hii ni aibu mbunge anatakiwa atleast awe na shahada ya diploma na kuendelea ,form 4(basic education) unafanya nn bungeni ?sitaki kuamini story ya darasa la 7 karne hii ya 21.
 
Ninavyojua hili hawezi kuliongelea hata kuligusia, hata wabunge wenyewe hawawezi, vinginevyo wanaharakati waanzishe mada hii
 
Ubunge ni uwakilishi wa wananchi, tatizo watu waliosoma wameona ubunge kqma fursa ya ajira. Hivi jama umesoma unashindwa nini kushawishi wananchi wakuchague hadi utegemee huruma ya serikali.
Kqma ni hivyo hata wapiga kura elimu yao ianzie kidato cha sita na kuendelea. Pia mnajisahau kuwa kwa mujibu wa katiba kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa
 
Hao Wabunge Darasa la Saba Walitakiwa wawe Wachunge Ng'ombe au Kufuga Kuku wa Kianyeji maana wa Kisasa Wangewapa Hasara as they are not risk takers, basi tu Umbumbu wa Watanzania Umewabeba.
Kama Yule wa Geita sio risk taker kabisa wakati Prof Muongo ni Risk taker
 
Hivi kwani ni kweli wapo wabunge walioishia darasa la saba?
 
Nani alikudanganya kama mbunge ni mtumishi wa umma ? Kwa taarifa yako mbunge hayumo katika mfumo wa utumishi wa umma bali ni mwakilishi wa wananchi katika Bunge. Yeye ni mwanasiasa hafungwi na taratibu za utumishi wa umma ambao ukifikisha miaka 60 lazima ustaafu. Mbunge anaweza hata akawa na umri wa miaka 80 bado akawa mbunge. Ninaunga mkono hoja kwamba kutokana na maendeleo makubwa katika ulimwengu wa leo kuna haja ya kupitisha sheria angalau mbunge awe na elimu ya kidato cha nne.
Kama sio watumishi wa umma mbona wanajaza form za maadili ya utumishi wa Umma?
 
Back
Top Bottom