Hueleweki!
Wewe ndo unaji contradict! Uko upande upi sasa? Upande unatetea la 7 na upande unatetea PhD....!!!
Kama ugonjwa ni UDHAIFU wa Elimu katika jamii unataka kutuambia Wasomi wote Tanzania Doctors na PhD holder Elimu yao Ni questionable? Kumbuka kuna Watz wamesoma nje ya Tanzania na Wana perform wonders!
Ningekubaliana na wewe kama ungelisema UDHAIFU WA TANZANIA NI CCM NA KATIBA MBOVU YA NJI HII.
Ndiyo maana PhD holder akishakuwa Mwanasiasa PhD anaweka pembeni anaanza kucheza ngoma ya CCM na KUDEMKA KWA SANA.
Ndo maana Watz wanasema tumeruhusu AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA...!
Maana Serikali ya CCM inawaruhusu Darasa la Saba kuingia Bungeni kuwatukana Professors na Spika Ndugai mwenye Digrii ya 1&2 anawaruhusu na kuwaongezea dakika. Shame!!
Wewe unaandika kama simpleton.
Hata kuelewa set theory tu tofauti ya union, intersection, compliment, kuelewa abstract tu huelewi.
Kwani nikisema darasa la saba anaruhusiwa kugombea ubunge ndiyo nimemkataza huyo Ph.D aliyesoma nje asigombee ubunge?
Mbona reasoning yako ni poor sana kwa mtu anayetetea elimu?
Nilitegemea mtu anayetetea elimu atuoe rrason ya kielimu yenye mantiki, siyo hii yako inayoprotest kitu ambacho hakina merit ya ku protest.
Unajua kufikiri kwa mantiki?
Unaelewa kwamba darasa la saba wakiruhusiwa kugombea ubunge wenye Ph.D hawajakatazwa?
Unaelewa kwamba mimi sijaleta hoja ya kusema "zuieni watu wenye Ph.D kuwa wabunge, wabunge wawe walioishia darasa la saba tu". Ninasema walioishia darasa la saba wapewe uhuru wa kugombea ubunge sawa na Ph.D, wananchi waamue nani anafaa?
Sasa mbona unanipa mzigo usio wangu kama vike nimesema Ph.D wasigombee ubunge, wagombee darasa la saba tu?
Unajua kusoma kwa ufahamu?
Ngoja nijaribu tena kukueleza.
1. Kwanza kabisa naomba uelewe kwamba mimi si mpinga elimu. Mimi ni mpenda elimu. Ila naelewa kitu kinaitwa "the law of unintended consequences" na "the road to hell is paved with good intentions". Jaribu kusoma hizo habari kama una uwezo.
Things are counterintuitive sometimes.
Ma korti ya Wafalme wa Ulaya tulikogeza hii elimu rasmi ya vyeti walihitaji "Court Jesters". Hawa si wasomi. Hawa ni wasanii wa kuchekesha tu. Na katika korti hizo, mtu yeyote alikuwa hatakiwi kumsema Mfalme vibaya, wasomi wote wakimsema Mfalme vibaya walikuwa wanauawa.
Ila huyo mchekeshaji ambaye si msomi ndiye mtu aliyekuwa anaruhusiwa kumsema mfalme kwa lolote.
Kwa sababu huyo ndiye alikuwa ana uwezo wa kumuambia mfalme mabaya yake, halafu mfalme akayafanyia kazi bila kujisikia vibaya kwamba amekosolewa na wasomi.
Kwa hiyo hawa "court jesters" wana sehemu zao katika jamii toka huko tulikogeza haya mabunge yetu.
Nimekuuliza swali hujalijibu
Ukipewa bunge lililojaa wasomi wa Ph.D, wanaojua wananchi ni wajinga na hawawezi kuwafuatilia, wasomi wakaiba na kudanganya watu, bunge hilo la wasomi litakufaidisha vipi? Hujajibu.
2. Elimu haiishii kwenye elimu rasmi. Kuna watu wana elimu rasmi na hawajaelimika, na pia kuna watu hawana elimu rasmi ila wameelimika.
Hawa wengine kiingereza wanaitwa "autodidact". Watu wanaojifunza wenyewe.
3. Kuwa na elimu rasmi kubwa mara nyingine si alama ya kuwa na akili au uwezo sana. Inawezekana ni alama ya kuwa na access ya elimu (mtu wa kukulipia ada, kutoka familia iliyowahi kusoma etc).
Rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva hana degree.Ila watu wanampenda sana kwa uongozi wake mpaka wanamtaka arudi kuwa rais agombee tena.
Akiulizwa, kwa nini yeye hana degree, atajibu mimi familia yetu haikuwa na uwezo, nikianza kufanya kazi nikiwa mdogo, huko kazini nikaonekana kipaji changu cha uongozi nikapanda kwenye kuongoza vyama vya wafanyakazi.
Atasema elimu niliyoipata kwenye kuongiza vyama vya wafanyakazi haifundishwi katika degree yoyote. Mitihani niliyopambana nayo katika figusu za siasa za vyama vya wafanyakazi ni mitihani practical ambayo haina shule popote.
Ukimnyima ubunge au urais mtu kama huyu, ukampa mtu mwenye Ph.D na hulka ya ujinga, utakuwa umeji shortchange mwenyewe.
4. Hakuna shortcut ya kutatua tatizo la elimu bungeni. Kitu kinachotakiwa kufanywa nibkuongeza elimunkwa jamii nzima, ili jamii ijue kuwachekecha wagombea. Hili kitafanya tupate kile kinachoitwa "the best of both worlds.
5. Demokrasia ya kweli ninike ambayo haiweki vizingiti vingi kwa watu wanaotakq kuongiza. Kizingiti cha kweli kinatakiwa kiwe kukubalika na wananchi.
Unaweza kuwaletea watu kiongozi msomi sana wa elimubrasmi, lakini hajui lugha yao hao watu, akashindwa kuwasiliana nao, kwa sababu yuko tofauti sana nao.
Wakati kuna mtu mwingine hajasima sana kwa elimu rasmi, ika anawaelewa wale watu na matatizo yao na anaweza kuwasikiana nao na kuwaongoza vizuri zaidi.
Nasema kwamba, ikiwa kuna mtu ana kipaji cha uongozi, ila kwa sababu ya masahibu ya maisha tu hakupata vyeti vikubwa, labda alifiwa na wazazi mapema akakosa wa kumsomesha, au aliumwa macho siku ya mtihani wa mwisho akafeli, basi wananchi waweze kuujua uwezo wake na kumchagua awawakilishe. Kusiwe na vigezo vikubwa vya elimu kwenye ubunge kumnyanyapaa huyu.
Vivyo hivyo, kukiwa na mtu ana Ph.D, lakini maneno yake hayaendani na Ph.D, anasema amneno ya ovyo ovyo tu, mara awaqmbue watu wabaki na mavi yao majumbani mwao wasichqfue vyoo vya serikali, mara anakataa chanjo na barakoa, wananchi waweze kujua huyu hamnazo, na labda Ph.D yake kasaidiwa tu, wamkatae.
Ukitaka kazi ya wananchi ya kuchekecha viongozi ifanywe na vyeti vya elimu rasmi unaweza kukosea katika sehemu mbili hizi.
Unaweza kumkataa mtu ambaye ana uwezo wa kuongoza, ila, kutokana na matatizo fulani tu hakusoma kupata vyeti. Labda kasoma kwa uzoefu wa kazini au kujisomea vitabu mwenyewe.
Hili moja.
Lakini la pili, ukiangalia elimu kama ni vyeti, kilimbukeni, matokeo yake ndiyo hayo utaishia kumchagua mtu mwenye Ph.D kwa kufikiri Ph.D ndiyo guarantee ya uongozi bora, halafu huyo mwenye Ph.D akashindwa hata kuongea kwa staha, akakwambia baki nyumbani na mqvi yako usichqfue vyoo vya serikali.
Watanzania wengi wanasumbukiwa nanukimbukeninwa elimu.
Ulimbukeni wa elimu ndio unawafanya watu waone kwamba elimu maananyake ni vyeti.
Wakati kuna elimu kubwa sana isiyo na vyeti.