Ulevi ni mbaya hasa ukisababisha kushindwa kutimiza wajibu wako.
Darasa anaonekana kabisa ni mwanji lakini sikudhani kama anaweza kunywa kufikia kushindwa kutimiza wajibu wake.
Nashukuru kwa kumwambia ukweli na huo ndio ushabiki wa kweli ikiwezekana ajitazame na kubadilika.
Najua Darasa anapendwa sana na wengine wanaweza wasikuamini kwakuwa wanampenda sana hata kama uliyo yasema ni ukweli lakini najua umetimiza wajibu wako.
Pengine wimbo wake umekuwa mkubwa sana hadi ameshindwa kuhimili kishindo cha wimbo wake.
Hapa ndio utajua umuhimu wa management....
Darasa kama kweli unakunywa hadi unashindwa kutimiza wajibun wako basi acha ulofa na ubadilike..huu ni wakati wako hakuna nafasi nyingine.