Habari yako mkuu..!
Kiukweli hata mimi ninampa pongezi sana Darasa, ameonesha uwezo mkubwa sana. Hilo limejithibitisha wazi kabisa hata mitaani kwetu, kila kona hiyo ngoma inachezwa, hata hapa ninatype nikiwa naisikia kwa earphones.
Mi kwa jinsi nilivyokuelewa hauna maana mbaya!
Ulichokisema hata mimi nimeshawahi kukihofia, KUDUMU KATIKA UBORA WAKO KATIKA MUDA MREFU ( CONSISTENCE )
Hilo ndio jambo ambalo ni changamoto kwa wasanii wengi sana.
Ila tumtakie mafanikio katika kazi yake, hilo ndio jambo la msingi. Mafinikio yake ni jambo la kufurahia na sio vinginevyo.