Dark days 17/03/20...

Wewe ulikuwa na maono kama yangu.Ila tangu zamani huwa ninamuona Mr.Born town ni mtu makini sana kwenye suala la Kampuni na huwa anamuweza sana huyu Paka, kwahiyo pamoja na mambo yake ila kiukweli namkubali ile advertise aliyomfanyia kule kanda ziwa hasa Kagera na Kigoma ilitosha kusema jamaa yuko vizuri. Hii riwaya mpaka ifike mwisho Fanani atakuwa ametupatia mwisho mzuri na picha halisi ya nini kinaendelea. Tuendelee kuchambua pasipo mihemko maana huko mbele hatujui nini kinakuja.
 
Ohooooooo
 
Mi nadhani kumuua mr born town siyo suluhisho kabisa hata kidogo. Maana tunajitengenezea taifa lenye laana. Ni kama wao akina Mr born town walivyomuua late CEO. Nadhani system ni muhimu ziangalie namna ya kumtumia mr born town ktk maendeleo ya nchi maana bado tunamuhitaji, si mumeona leo timu ya wananchi tumewatandika 1 nunge vilaza simba hahahah (hapo nimechomekea mambo ya moyoni ya timu wananchi). Ila tuache utani mtindo wa kuuana ni mbaya sana ktk taifa lolote.
 
Kwa hyo tuendelee kuacha kikundi fulani cha watu wachache kiendelee kuinjoi keki ya taifa huku wananchi wakitaabika na lindi la umaskini?
 
Kwa hyo tuendelee kuacha kikundi fulani cha watu wachache kiendelee kuinjoi keki ya taifa huku wananchi wakitaabika na lindi la umaskini?
Kuna namna nyingi za kudeal naye ila kumuua haisaidii kabisa & I’m against hiyo move. Pamoja na machungu niliyonayo ya mr born town kumuua mtu wetu, kipenzi cha watanzania late CEO lakini kulipiza kwa kumuua yeye tunajiandalia taifa ya kuuana kama ilivyokuwa utawala wa roma na kwa huo uuani tutaandaa mfumo ambao siku ya kufeli nchi itabaki mikononi mwa mafia kama Italy ilivyo sasa kwa sababu tutafikia kuwa na vikundi ambavyo vitaamua nani vimuue ili fulani awe rais na hivyo vikundi vitajitwalia rasilimali. Tumuache kabia mr born town na asiguswe dhambi ya kushiriki kumuua late CEO iishie kwake tu. Please deep state walijue hili wasimuue mr born town wamuache kuepusha laana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…