Ufisadi uliotamalaki nchini ww kama mzalendo unauongeleaje? Tunaosema mambo hayako poa unatuona sisi si wazalendo
Mbona haya yote nimeshayaongelea labda kwa mtazamo wako hukunielewa, nimeshasema sana hata kama siyo hapa kwamba watu wameacha misingi ya mwanzo wanawaza pesa,rushwa, wizi,nikashauri waache wawe na utu na kuwaonea huruma wananchi.
Kama nimewasema nyinyi mnaouchukia ufisadi sikumbuki kwa kweli nilisemaje, au nilisema kwa lugha ambayo haikueleweka. Lakini nipo pamoja na nyinyi katika kupinga ufisadi.
Uzalendo una mapana yake mengi, kuna wakati hata kama umechukia kuna namna ya kuongea na kufikisha ujumbe.
Pia kuisema serikali si kwa matusi, kejeli, ugomvi au kutoa siri za ndani na kuzianika nje halafu useme tayari nimemuweza.
Hivi umewahi kujiuliza, kwa mfano ndg yako amekukosea halafu ukaamua kupeleka siri zake nje ukamuanika hadharani mambo yake yote, aibu zake zote na kumuacha uchi.
Hapa unakuwa umemkomoa nani?
Uchi wa nduguyo ni wako pia, aibu ya nduguyo ni yako pia. Mahali penye uwezo wa kumsaidia kumvika nguo mvike na kumsitiri.
Kama una suruali mbili mpe moja, kama huna mshonee kiraka uyafiche makalio yake, kama huna kiraka cha nguo mvishe cha gunia, nacho kama hakipo mpatie kiraka cha bati hiki ataishi nacho muda mrefu na aibu yake haitaonekana.
Watu watakuona wewe kupitia ndg yako. Watanzania wenzangu nawaomba sana kwa yeyote anayesoma ujumbe huu tusitiriane, tuonyane kwa hekima na busara pale tunapokoseana.
Tuvumiliane sote tu wadhaifu, tunatofautiana katika kuwaza na kutenda. Sijakusudia kumkwaza mtu,mawazo yangu yanaweza kuwa si sawa, ila nimeongelea katika misingi ya uzalendo. Penye kuzungumza kwa hoja na iwe hivyo.
Kuishi kwa kuviziana, visasi, na mauaji si sawa mbele za Mungu. Haya ni mawazo yangu siyo sheria, sitarajii kumkwaza mtu au kumuhukumu.
Mahali palipo na diplomasia hapaharibiki neno.Mambo mengine tunaweza kuyamaliza kwa mazungumzo pasipo ugomvi.
Huu ndio Uzalendo.