Yawezekana ni kweli ana watu kila sehemu au ndivyo sivyo,mimi na wewe hatuna uhakika.
Hii kampuni ina watu wengi sana wenye akili nyingi,kama wameweza kuyaona haya yote hawawezi kuwatrace na kuwatambua wote waliopo nyuma yake na kukata chain nzima?
Kwanini asiwekwe bench tu akanyimwa access ya kumuendesh current ceo, hivi akimulikwa kwa macho makali bado anaweza kuendelea kusumbua?
Kwani sasa hivi anajilinda, anayemlinda hajui nyendo zake? Ninachotaka kusema hapa tusitatue matatizo kwa kulipizana visasi vya mauaji. Damu hizi zinaweza kuja kuligharimu Taifa huko mbeleni sisi tukiwa hatupo.
Ninavyojua kampuni ilisema tuanze upya tusameheane, kwahiyo hata kumuacha tu kwamba sasa wewe mzee pumzika inatosha kwake.
Hivi watu wakiambiwa warudishe mali zote za umma zilizoibwa na kufichwa nje na ndani halafu zikatumika kwa maslahi ya Taifa haitoshi?
Mkimuwajibisha kwa execution bila kujua kama ana mali,zipo kiasi gani, wapi,taifa litafaidika vipi? Maana tunaambiwa anafanya biashara, kama kuna mikatab ya hovyo ivunjwe na kurejeshwa serikalini iangaliwe upya.
Kilichotokea kwa jiwe sikukipenda kiliumiza watu wengi, hata huyu kitaumiza watu wengi pia, Mr.New culture alichofanyiwa na Kijana msema sana vyote sikuvipenda. Haki haikutendeka kwao .
New ceo anayotaka kufanyiwa bado siungi mkono hoja. Kampuni hiii ina watu mahiri wa diplomasia na maono kwanini wasikae mezani wakazungumza?
Uzalendo wangu ninamaanisha naipenda nchi yangu Rais wangu, Watanzania wenzangu wote, wana JF wote, mwenye Uzi wake Yoga na wewe pia, na wote ninaojibizana nao.
Bado hatujachelewa tunaweza kuanza upya kuijenga Kampuni yetu katika Upendo, Haki na Amani huku tukihubiri neno Uzalendo Kwanza.
Siko upande wowote, sijatumwa na yeyote, sifaidiki na chochote wala mfumo wowote ule wa upigaji, mimi ni mkulima ila ninaipenda Kampuni yangu.
Nawapenda makamanda wote mnaotulinda tuko shwari ndio maana tunapata muda wa kuandika haya,hata Ukraine na Russia wanatamani kuwa kama sisi sasa hivi lakini je yanayoendelea huko wameyastahili hayo na ni haki yao na Uzalendo? Kazi yenu ni njema sana. I salute you commandas!!