Dark days 17/03/20...

Nimekumbuka maelezo yake. Wasiwasi wangu ulikuwa je Mungu ataadhibu na wale wamchao katika roho na kweli?

Kwa jinsi ulivyoelezea sidhani kama utakuwa mbali na yeye.

Ubarikiwe sana mkuu.
 
Nimekumbuka maelezo yake. Wasiwasi wangu ulikuwa je Mungu ataadhibu na wale wamchao katika roho na kweli?

Kwa jinsi ulivyoelezea sidhani kama utakuwa mbali na yeye.

Ubarikiwe sana mkuu.
Wale wamchao Katika roho na kweli watapona na MUNGU atawalinda na mabaya yote!
 
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere kundi kubwa la watu walionekana wakikimbia mara baada ya kuvunja geti, wakawa wanaelekea kwenda kushuhudia mwili wa Rais wao kipenzi ukiingizwa ndani ya ndege tayari kusafirishwa. Licha ya serikali kutoa siku mbili za kuuwaga mwili wa marehemu lakini hazikutusho kuwazuia maelfu wa Watanzania waliojitokeza hadi uwanja wa ndege kumsindikiza huku wakiimba na kulitaja jina la shujaa huyo.

Watu walifika uwanjani hapo walikuwa ni wengi mno, ikiacha idadi kubwa ya Watanzania waliojipanga pembeni ya barabara kutoka uwanja wa mpira wa uhuru hadi kufika uwanja wa ndege bado hawakufikia idada ya hawa waliofulika uwanjani hapo.
Licha ya kuwekwa utaratibu maalumu uwanjani hapo lakini ilikuwa ni ngumu kuwazuia Watanzania hao ambao baadae walivunja geti na kuanza kukimbia wakiingia ndani zaidi ya uwanja wa ndege. Hali hii ilipelekea wengine kuanguka na kuanza kukanyagana. Ilikuwa ni hatari sana hasa kwa wanawake na vijana wadogo walikuwa miongoni mwa waombolezaji hao.

David akiwa mmoja kati ya maelfu ya watu waliofika mahali hapo, alishuhudia kundi kubwa la watu likivunja geti na kuingia ndani ya uwanja wa ndege kwa kasi. David akiwa hatua kadhaa kutoka hapo, alijikuta akitabasamu na kuwaza moyoni.

"Huu ni upendo wa ajabu wanaouonyesha Watanzania kwa Rais wao, haijawahi tokea mahali popote Dunia, hakika walimpenda mno"
Aliwaza David na wakati akiwaza hayo ndipo alipoona tukio lingine la ajabu.

Katikati ya lile kundi kubwa la watu waliokuwa wakikimbia kwa mara nyingine tena alimuona yule binti mwenyewe gauni jekundu. David alitoa macho kwa mshangao baada ya kuona binti huyo akifanya mambo ya ajabu. Si kwamba alikuwa akikimbia kama wengine la hasha, yeye alikuwa bize akiwainua wale watu waliokuwa wakianguka chini kuwazuia wasikanyagwe. Alikuwa akiifanya kazi hiyo kwa kasi sana. Anaenda kushoto anamuinua huyu anarudi kulia, anakwenda mbele anarudi nyuma huku kasi yake ikionekana kutokuwa ya kawaida kabisa.
Yule binti aliendelea kuifanya kazi hiyo katikati ya ule umati mkubwa wa watu. Jambo la ajabu ni kwamba hakuna aliyekuwa akimuona zaidi ya David peke yake.
"Oo..oya mwanangu" Alisema David huku akimgusa begani mwanaume mmoja aliyekuwa amesimama pembeni karibu yake.
"Nambie" aliitika
"Unamuona yule msichana anachokifanya pale?"
"Msichana yupi?"
"Yule pale" David akanyoosha kidole katikati ya ule umati wa watu wanaokimbia
"Sasa watu wote wale nitajua ni mtu gani unamzungumzia" aliuliza yule mwanaume huku akimtazama David usoni kwa mshangao.
"Namaanisha yule Dada amevaa gauni jekundu kwani huoni anavyofanya katikati ya wale watu?"
"Eeh.. we jamaa mi sikuelewi bana" Alisema yule mwanaume huku akimuona David kama mwendawazimu, akazuga kama anapokea simu akaenda zake pembeni.

"Mbona anaonekana kwamba haoni nini pale?" David alijiuliza hukua akiamini kwa mtu mwenye macho yenye afya kamili kama yake asingeshindwa kumuona yule msichana mwenye gauni jekundu.

Wakati David akizidi kutazama mara ghafula akaona tukio lingine la ajabu. Kilishuka kitu cheusi kutoka juu angani kikaanguka chini katikati ya ule umati wa watu na baadae akasimama mtu mmoja aliyevalia mavazi meusi tii kuanzia juu hadi chini. Hata yeye alikuwa na ngozi nyeusi tii kama nguo zake. Alikuwa amevaa koti kubwa jeusi lenye kofia pana kichwani. Koti lake lilikuwa refu mno kiasi cha kugusa chini na kufanya miguu yake isionekane.
Mkononi alikuwa ameshikilia mkuki mrefu, akawa anatembea kumuelekea yule binti anayefanya kazi ya kuinua watu waliodondoka.
Yule mtu mwenye mavazi meusi naye alikuwa akipishana na watu pasipo kuonekana yaani alikuwa ni David pekee ndiye aliyekuwa akiwaona watu hao wa ajabu.
Yule mtu aliendelea kutembea akawa anamueleka yule binti, kwa bahati mbaya yule binti hakuwa amemuona kabisa na alipo mkaribia aliinua mkuki wake juu akiwa amedhamiria kuuzamisha kwenye mgongo wa yule binti aliyekuwa ameinama wakati huo.

David alishuhudia yote haya akiwa kwa mbali asielewe ni nini hasa kilikuwa kinaendelea. Alifumba macho kwa hofu asishuhudie tukio lile la kutisha. Kuna wakati alihisi kama yuko ndotoni lakini kila alipojaribu kuzinduka kutoka usingizini ndipo alipogundua kuwa haikuwa ni ndoto bali kila alichokiona na kukishuhudia kilikuwa ni kweli tupu.

Wakati yule mtu akiushusha kwa nguvu mkuki wake ghafula kufumba na kufumbua wakatokea wanawake wengine watano waliovaa mavazi mekundu sawa na alivyovaa yule binti. Mmoja kati yao akasimama mbele ya yule binti na wakati huo huo yule bwana mwenye mavazi meusi akausindilia mkuki wake kwenye mwili wa yule mwanamke aliyesimama mbele ya binti yule kumkinga, nikama mwanamke yule alikuwa amejitoa muhanga kuzuia mkuki usimpate yule binti na badala yake ukazama kwenye kifua chake na akatokea mgongoni.
David alipokuja kufumbua macho yake kuangalia kwa mara nyingine akakutana na tukio lingine la kutisha, aliona ule mkuki ukiwa umezama kwenye mwili wa mwanamke mwingine ambaye hakujua ametokea wapi huku wale wengine wanne wakiwa wamesimama imara kumzunguuka yule binti. David hakujua watu hawa wamefikaje fikaje mahali hapo na wametoka wapi. Kila alichokiona kilizidi kumchanganya na kumuacha mdomo wazi.
David alishuhudia yule mwanamke aliyechomwa mkuki akipukutika kama mchanga na baadae akawa moshi mweupe uliopotelea hewani. Wakati huo huo wale wanawake wanne waliosalia wakawa bado wamesimama kumzunguuka yule binti ambaye aliacha kufanya kile alichokuwa akikifanya sasa akawa anaelewa kuwa yuko hatarini kushambuliwa na yule mtu mwenye mavazi meusi.
Ajabu ni kwamba licha ya idada ya wale watu wa ajabu kuongezeka lakini bado ni David pekee ndiye aliyekuwa akiwaona. Watu wengine wote walikuwa bize na harakati za msiba wa Mheshimiwa Rais.

Yule binti alikuwa amesimama katikati huku akiwa amezinguukwa na wale wanawake wanne ambao kila mmoja alikuwa na kisu kidogo mkononi mwake kilichofungwa utepe mwekundu. Yule binti alipenya kati kati ya wale wanawake waliomzunguuka akapiga hatua kumsogelea yule mwanaume mwenye mavazi meusi.

"Tafadhali usimsogelee ni hatari" Aliongea mwanamke mmoja kati ya wale wanne.
"Acha niongee naye"
"Hapana Sasha anaweza kukudhuru" Yule mwanamke alisisitiza.
Naam, hilo ndilo jina halisi la binti huyo, aliitwa SASHA.
Wakati yote hayo yakiendelea David alikuwa kwa mbali akishuhudia. Alishangaa ni vipi anaona vitu ambavyo ama kwa hakika ni yeye pekee ndiye alikuwa na uwezo wa kuona lakini watu wengine hawakuelewa lolote. David hakujua ni vipi amepata uwezo huo, lakini mambo yalibadilika tangu pale alipoliokota lile boksi la SASHA akiwa ndani ya uwanja wa uhuru wakati ule wa kuuga mwili wa Mheshimiwa Rais.
 
Watu mwa roho mbaya nyie, yaani valentines ikapita hata mwaliko??[emoji23][emoji23][emoji23] Nime wamiss saaaaana[emoji76][emoji76][emoji76]
Ulipotea sana ukatuacha jangwani tulishawaza tuchonge ndama wa shaba labda atatufikisha Kaanani maana hatukujua yaliyokupata huko mlimani.

Tumefurahi kuona bado unapumua ngoja tuendelee na safari ya matumaini kufika tuendako 20 march 2023[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666]
 
Link ya uzi huo Tafadhali
 
Interesting,

RANGI ya Vazi analovaa mtu ktk Ulimwengu wa Roho kimwonekano linatambulisha mamlaka anayoitumikia mtu aliyevaa vazi Hilo.

Red and black ni RANGI za chini.

Malaika wa Nuru huvaa mavazi MEUPE. Ni utambulisho wa kule watokako.

Sometimes shetani naye huyavaa mavazi MEUPE Ili kutuhadaa bt Huwa tunamtambua usoni, Huwa kakunja NDITA sana,

Bt tangu kuumbwa Ulimwengu, Mungu hakuwahi mtuma mjumbe wake Kwa mwanadamu ktk mavazi mekundu au meusi.
 
Sio fix, nenda U-Tube, ushuhuda wa alioonyeshwa Adam Mbaya Kutoka congo, PROMOVER Tv. Part 36.

Ina TITLE: Nililiona Jina la OLD CEO likifanyiwa njama ktk kitengo Cha poison KUZIMU gizani.

Ulimwengu wa Roho hakuna Siri.

Proof ndo huwezi kuwa nayo kutestify ktk court za WANADAMU,

Hivyo inabaki kuwa tetesi.
 
Sio jina la new CEO ni la late CEO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…