Dark days 17/03/20...

Mkuu unaandika ukiwa nchini tz au nje ya nchi? Au unatumia hisia za kisiasa au uhalisia wa matendo?
 
Soma vizuri kwa Yoga. Utaona why projects za JPM zinaendelea.
Yaani umuue mtu sababu kaleta mradi wa kukuharibia ulaji. Alafu ameshakufa Bado tu unaendeleza mradi huo huo uliosababisha uue mtu?

Basi hao wauaji kwenye hii riwaya wamesingiziwa. nilitegemea alivyokufa tu na mradi ungetelekezwa Ili waendelee kupiga Hela!!
 
zitto junior anafanya spinning kwa vichwa maji wengi humu. Sisi acha tuendelee kuwa wapenzi wasomaji lakini bongo zetu zina chujio [emoji851]
Wala hakuna spinning ni reasoning ya kawaida tu. Tatizo wengi wanapenda conspiracy theories. Mfano mtu anakomaa eti JPM alikua haumwi ila kapewa sumu, Sasa namuuliza kivipi kampeni alishindwa kufanya au alikua ameshapigwa sumu? Pia nimeuliza huko nyuma aliwahi dondoka Pemba and later Ruangwa na alipotea kama wiki mbili kabisa Hadi kina Zitto wakapost bendera nusu mlingoti..... Baadae akazinduka.

Miaka yote hiyo haikuwa sumu ila 2021 ndio sumu? Je asingezinduka baada ya kutoka Ruangwa nayo wangesema sumu?

Embu tuache conspiracy, ni ngumu sana kumuua Rais wa nchi maana sio kwa ulinzi ule wa kimwili na Roho. Anaweza kufa only when the deep state decides so and it cant be by polonium and taarifa zisingevuja kabisa.
 
Kilichomuua late CEO ni hawa wazee wa bismillah. Walikasirika baada ya yeye awamu hii kuselect baraza la mawaziri lililojaa wakristo wengi hii iliwakera. Bila kujua wakamtanguliza mbele ya haki R.I.P[emoji854]
Kwani ni Rais yup toka nchi imepata uhuru aliwahi kuteua mawaziri waislam wakawa na uwiano walau unaokaribia sawa na wakristo? Kwann hao huko nyuma hawakuuliwa?
 
Hakuna cha kuanguka Zanzibar wala hiyo issue ya kusini uzuri ilikuwa live hiyo watu walitumia invisible power kutaka kumwondosha ndo maana kila aliyekuwa anaangalia ule mkutano aliuone ule moshi na maneno aliyoyasema.

Sema kuna nguvu kubwa inayumika kulazimisha mwamba aonekana alikuwa na hitilafu ya moyo ila hiyo ilitumika tu kama gia ya kuwaaminisha watu. Sidhani kama mtu mwenye pace maker anaweza kupiga push up au kuendesha zaidi ya mikutano mitano kwa siku. Lakini pia akiwa ikulu ya chamwino kuna kipindi alionekana anaruka kwenye mawe sasa kwa mtu wa pace maker sidhani kama anaweza kufanya vile.

Sema watu wamefanikisha yao acha nchi itafunwe na mchwa. Kuna yule ceo wa nne yeye alikuwa anaanguka mara kadhaa majukwaani mbona mpaka leo yupo.
 
We jamaa mwongo sana. Yule mzee alikuwa na tamaa ya madaraka kuliko fisi akiona mzoga.

Tumwombee Mungu amrehemu madhambi yake lakini kwenye hili hana utetezi wowote.
Ni lini alitangaza kuwa anataka kujiongezea muda, unajua hata kama hatumpendi mtu ebu tujaribu kutomlisha maneno
 
Kuna yule ceo wa nne yeye alikuwa anaanguka mara kadhaa majukwaani mbona mpaka leo yupo
CEO wa 4 alikiri ni mgonjwa na amewahi Hadi fanyiwa operation kuondoa saratani ya tezi dume. Sasa Cha ajabu mnachokataa kwa JPM haumwi ni Nini? Mtu kampeni hakufanya zaidi ya 60% ya ratiba aliyopangiwa.
Christian Eriksen nyota wa Manchester United mbona anavaa pacemaker na anacheza Mpira kama kawa. Imagine Mpira mnavyokimbizana na hajawahi pata shida uwanjani ndio sembuse JPM push up 5 zile?
Hakuna cha kuanguka Zanzibar wala hiyo issue ya kusini uzuri ilikuwa live hiyo watu walitumia invisible power kutaka kumwondosha ndo maana kila aliyekuwa anaangalia ule mkutano aliuone ule moshi na maneno aliyoyasema.
Kama ni invisible power mbona hakufa? Au Nini kilizuia asife kwa invisible power aje kufa kwa visible power?
 
Hahahaha, kwakwel napenda unavojibu kwa hoja, hapo kweny hoja ya pace maker ndo umemaliza kabisa, salute mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…