Dark days 17/03/20...

Mkuu fafanua hp kidgo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu fafanua hp kidgo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu

Katika zama hizi za mpinga kristo anapoenda kushika hatamu Duniani kote,IPO nchi Moja iliyoteuliwa ambayo Mungu atamsimamisha mtumishi wake ili kusimamia utawala was kimungu katika nchi hiyo!

Yaani nchi hiyo ndio pekee mpinga kristo atashindwa kuitawala ikiwa na mamlaka ya kiungu,ndipo watakatifu wote wa Dunia wamwabuduo mungu katika roho na kweli watakimbilia ndio nchi hii ambayo Mungu anaenda kusimika utawala wake!!

Ataenda kusimama mtumishi was mungu kama kiongozi katika nchi hii nae ataitengeneza kuwa makusanyo ya watakatifu wote kabla ya kanisa kunyakuliwa!!

Duru za maandishi na kinabii kwasasa zinasomeka hivyo!mvurugano utakaojitokeza utamuibua mtumishi kuwa kiongozi!ngoja mnyukano kwanza uendelee!!
 
Halijawashinda, just watch and enjoy the game.
 
Hii ni kweli Mkuu kuna Manabii nawaheshimu sana, walizungumza juu ya unabii wa Tanzania kuongozwa na mtumishi wa Mungu na madhabau ya kuzimu itaondolewa rasmi Ikulu ya Tanzania na Mungu atasimika madhabau takatifu juu ya taifa la Tanzania.
Lakini pia Kenya wana madhabau ya kuzimu ambayo itakuja kuondolewa na Rais Mwanamke!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Yaani +255?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa hapa!

Hebu nenda Temeke pile,kamuone yule Benedict victor atakupa mchongo hapo The rupture ministry,kanisa la unyakuo!!

Ana madini kiasi msikilizie tuone!

YouTube unyakuo TV!
Nimekaa temeke miaka 5 now nimehama mkuu mitaa yangu ilikuwa ni pale chuo cha bandari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Master NAMBA MOJA AJAYE NCHINI hivi member wa Ds sheria za nchi zinamgusa?
Kwamba akifanya kosa sheria zinaweza kumwajibisha na kumfunga kweli?
 
Mkuu itakuwa rahisi Ds iliyo chini Lucifer kukubali kuachia utawala na utawala wa juu kuweza kumiliki?
 
Mkuu itakuwa rahisi Ds iliyo chini Lucifer kukubali kuachia utawala na utawala wa juu kuweza kumiliki?
Hebu ingia kwanza unyakuo Tv,Kuna videos nyingi sana za kifo Cha mungu wa Tz yaani Dragon ambae alikua anaweka utawala!na sasa kiroho eti nchi Haina kiongozi hadi sasa!!

Zote ni nadharia lakini tusongapo mbeleni tutakuja kuona pole pole!

Vita vya dragon kuachia kiti haikua rahisi!

Ngoja tusubiri!2025 tutaanza kupata majibu!
 

Sawa baada ya mwaka mpya kuanza nitafanya hivyo kiongozi
 
Mkuu hivi nabii kuhusu hatma ya uongozi Tanzania zinatoka katika chanzo kipi cha habari? Nini kuhusu uhakika wa chanzo hiki? Ikulu ya Tanzania imekuwa ikikaliwa na marais wa madhehebu ya Kikatoliki upande wa Wakristo na Kishia upande wa Waislamu. Je! Hawa wote wana nadhiri ya madhabahu ya kuzimu? Hii lugha ya madhabahu huongelewa sana na walokole.

Jamani naomba mniwie radhi kwa kuwa kama Thomaso aliyetia mashaka kuhusu habari za ufufuo wa Yesu Kristo. Napata mashaka makubwa kuhusu unabii kuhusu majanga yatakayolikuta Jiji la Dar es Salaam ifikapo mwezi Mei mwaka 2024 na kuinuliwa kwa rais ambaye atakuwa mlokole (kwa lugha ambayo ni rahisi kueleweka).
 
Kiongozi The MoNA kwenye hii Ds ndani ya Ds layer ipi yenye nguvu kushinda layer nyingine?

Ds yote ina nguvu lkn yupo ds mkuu. Ulimwengu unaongozwa na energy mbili (positive or negative) positive is more powerful and peaceful energy unlike negative energy.

Hii positive energy (God the most highest one) ndiye mwenye mamlaka kamili. Hivyo ulimwengu wake ndio wenye nguvu japo mwenye ulimwengu negative amepewa mamlaka ya hapa duniani.
Kwa hiyo Ds zipo zenye mamlaka kutoka (positive or negative). Ila tulipo sasa ds negative inatawala dunia na kwa mamlaka waliyopewa kazi yao ni uharibifu mtupu.

Negative energy tuite (mamlaka ya chini) wanataasis zao za kuongoza dunia, inatumia watu kufanikisha mambo yake. Kwa hiyo mamlaka ya chini ndiyo ina nguvu na huwatumia watu kupitia watu ndio wanaanzisha ds ndani ya ds ili kufikia walio wengi
 
Mkuu The MoNA shukurani sana
 
Master NAMBA MOJA AJAYE NCHINI hivi member wa Ds sheria za nchi zinamgusa?
Kwamba akifanya kosa sheria zinaweza kumwajibisha na kumfunga kweli?
Wanasheria zaona viwango vikali zaidi katika operation zao!

Wakiwa uraiani watashatakiwa kama raia wakivunja sheria,lakini kwenye ujasusi was kidola utendaji wake haufuati Sheria za kawaida za kitaifa,wanatenda bila sheria za ndani!!
 
Mkuu hapa ishu sio ulokole Wala udini hapa ni kile kinachosikika KATIKA Vinywa vya watumishi manabii sio Tanzania pekee Bali duniani kite!

Ishu ya kuangamia Kwa dar sio ya mtu mmoja Kuna vinywa vya manabii zaidi ya wawili Tena ndani na nje ya nchi!

Ishu ya kuibuka Kwa mtawala mtumishi au mchungaji TANZANIA imesemwa Sana na manabii ndani na nje ya nchi!!

Wakristo was kikatoliki na waislam ambao WAMEKUA VIONGOZI kiroho wanatumiaWanatumia NGUVU YA upande wa pili!!!
 
Amewahi kutoa unabii wowote wa kitaifa ukatimia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mtumishi,

Hupaswi kuishi Kwa dhana.

Roho mtakatifu yupo, Muulize atakujibu ikiwa ni Kweli Dar itaangamia au la!!

Mimi niliuliza na nikajibiwa. Nasubiri kusikia Kutoka kwako pia.
 
Mkuu bado natamani kumtambua kwa kina nabii Boniface Victor, huduma yake ya unabii, na mamlaka aliyonayo kutoa jumbe mbalimbali za kinabii. Nasema hivyo kwa sababu wito wa nabii wa kweli ni suala ambalo linatiliwa mkazo mkubwa sana katika maandiko matakatifu.

Hii ndiyo maana Neno la Mungu kutoka kinywani kwa Yesu Kristo mwenyewe linatupa tahadhari kuhusu kutokea kwa manabii wengi wa uongo katika siku za mwisho wa dunia, ambao yumkini wataweza kuwapotosha hata wateule wa Mungu.

Aidha, maandiko haya yanaweka wazi kuhusu jinsi mtu alivyokabidhiwa jukumu la kuwa nabii. Tunaona kuwa nabii hajitumi mwenyewe na kuanza kujishuhudia yeye mwenyewe, wala hatumwi na mtu mwingine, bali anatumwa na Mungu mwenyewe.

Maandiko matakatifu hujitetea yenyewe wala hayahitaji usaidizi wa hoja kutokana na falsafa ama simulizi za mapokeo ya kibinadamu. Kwa kuwa msingi wa Neno la Mungu hupatikanika kupitia katika Neno lenyewe, na pia hupatanishwa kupitia katika Neno hilo hilo.

Ukirejea katika Waebrania 8:1-13 tunaona kuwa Agano la Kale lilikuwa na mapungufu tena ni kuukuu ndiyo maana likaja Agano Jipya. Mimi nafikiri unabii uhusuo kizazi cha sasa unapaswa kujengwa ndani ya Agano Jipya ama nyakati za uwepo wa kanisa, na wala si kupitia Musa na manabii wa kale ambao ujumbe wao ulilenga zaidi kabila 12 za wana wa Israeli na kwa kipekee sana uliwalenga Wayahudi milki ya ufalme wa Yuda.

Baraka na laana zilizopo katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati Sura ya 28 ni za Agano la Kale, tena zenye kuwahusu watu wa kabila 12 za wana Israeli ambao waliishi kupitia matendo ya sheria. Hizo haziwahusu watu wa mataifa kwa kuwa kupitia Agano Jipya wao huishi kupitia rehema kutoka kwa Bwana Yesu Kristo, kwa hiyo basi hawafungwi na sheria hizo za torati na manabii wa kale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…