Mkuu hapa ishu sio ulokole Wala udini hapa ni kile kinachosikika KATIKA Vinywa vya watumishi manabii sio Tanzania pekee Bali duniani kite!
Ishu ya kuangamia Kwa dar sio ya mtu mmoja Kuna vinywa vya manabii zaidi ya wawili Tena ndani na nje ya nchi!
Ishu ya kuibuka Kwa mtawala mtumishi au mchungaji TANZANIA imesemwa Sana na manabii ndani na nje ya nchi!!
Wakristo was kikatoliki na waislam ambao WAMEKUA VIONGOZI kiroho wanatumiaWanatumia NGUVU YA upande wa pili!!!
Mkuu bado natamani kumtambua kwa kina nabii Boniface Victor, huduma yake ya unabii, na mamlaka aliyonayo kutoa jumbe mbalimbali za kinabii. Nasema hivyo kwa sababu wito wa nabii wa kweli ni suala ambalo linatiliwa mkazo mkubwa sana katika maandiko matakatifu.
Hii ndiyo maana Neno la Mungu kutoka kinywani kwa Yesu Kristo mwenyewe linatupa tahadhari kuhusu kutokea kwa manabii wengi wa uongo katika siku za mwisho wa dunia, ambao yumkini wataweza kuwapotosha hata wateule wa Mungu.
Aidha, maandiko haya yanaweka wazi kuhusu jinsi mtu alivyokabidhiwa jukumu la kuwa nabii. Tunaona kuwa nabii hajitumi mwenyewe na kuanza kujishuhudia yeye mwenyewe, wala hatumwi na mtu mwingine, bali anatumwa na Mungu mwenyewe.
Maandiko matakatifu hujitetea yenyewe wala hayahitaji usaidizi wa hoja kutokana na falsafa ama simulizi za mapokeo ya kibinadamu. Kwa kuwa msingi wa Neno la Mungu hupatikanika kupitia katika Neno lenyewe, na pia hupatanishwa kupitia katika Neno hilo hilo.
Ukirejea katika Waebrania 8:1-13 tunaona kuwa Agano la Kale lilikuwa na mapungufu tena ni kuukuu ndiyo maana likaja Agano Jipya. Mimi nafikiri unabii uhusuo kizazi cha sasa unapaswa kujengwa ndani ya Agano Jipya ama nyakati za uwepo wa kanisa, na wala si kupitia Musa na manabii wa kale ambao ujumbe wao ulilenga zaidi kabila 12 za wana wa Israeli na kwa kipekee sana uliwalenga Wayahudi milki ya ufalme wa Yuda.
Baraka na laana zilizopo katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati Sura ya 28 ni za Agano la Kale, tena zenye kuwahusu watu wa kabila 12 za wana Israeli ambao waliishi kupitia matendo ya sheria. Hizo haziwahusu watu wa mataifa kwa kuwa kupitia Agano Jipya wao huishi kupitia rehema kutoka kwa Bwana Yesu Kristo, kwa hiyo basi hawafungwi na sheria hizo za torati na manabii wa kale.