Dark days 17/03/20...

Dark days 17/03/20...

Smartkahn kuhusu Rwanda kama kuna ukweli fulani, namna ambavyo anaipelekesha Congo hadi unashangaa kabisa.
Kagame ni kikaragosi cha Marekani katika maslahi yake pale Kongo.

Juzi, mkuu wa kurugenzi ya intelijensia ya USA ameenda kuwapatanisha Kagame na Tshekedi.

Kwamba jeshi la Kongo liache kushirikiana na FDLR kwasababu ni tishio kwa Kagame na utawala wake pale Kigali.

Kwa akili ya kawaida tu, sitarajii Tshekedi kuafikiana na pendekezo hili.

Ni sawa na kupendekeza, Kagame awaondoe wapiganaji wa 'March 23 Movement' ndani ya Kongo.

Kwa maana hiyo, pendekezo linamlinda Kagame kuliko Tshekedi.
 
Mkuu Peaceforever , utakuwa hunijui, mimi ni mmoja wa watu pisi sana humu JF, kwanza huwezi nisikia nikitukana mtu, pili hata nikitukanwa najibu kwa asante sana na ubarikiwe!. Mimi sio mkorofi kabisa!, ni mtu poa sana!.
P
Unatumia aliki ya kiutuuzima kuvumilia tusi lakini mkuu unaumia kwa ndani.

Tusi la kisiasa linauma sana mkuu.
 
Tuna mpaka mrefu sana na Kenya katika nchi tunazopakana. Tuna mpaka na Msumbiji, Congo, na nchi nyingine
Tushawishi kwanini unadhani Zanzibar imekaa vibaya. Ni kwa usalama upi
Kwanza Economic Intelligence specifically kwenye bandari ikijumuisha mnyororo mzima wa biashara, usafiri na usafilishaji;
_20231123_230808.JPG

Screenshot_20231123-232522~2.png

Geographical location ya zanzibar imeji-position sehemu mbaya ukilinganisha na pwani ya tanganyika huku,
hasa ukizingatia routes za usafilishaji na miundombinu yake, ukiachilia mbali kua bandari muhimu, kubwa na shindani ukanda huu zipo karibu na zanzibar lakini pia ndio eneo pekee lililokaa kimkakati katika kuhakikisha mizigo ya majirani zetu inawafikia kwa wakati, huku ukizingatia ushindani na majirani zetu Kenya, msumbiji hata Angola kule.

Pili vitisho vya kigaidi, yanaweza yakaibuka makundi ya kigaidi yenye itikadi kali za kidini ikawa ngome yao kule, wakatuletea shida bara huku Kwakua tutakua tumekosa udhibiti wa moja kwa moja.
Tulioishi wakati wa ' frontline states' na mapigano ya kudai Uhuru kwa nchi za kusini mwa Africa hatuoni tishio lolote la nchi jirani. Hata hivyo nakubaliana nawe kwamba 'Intelligence' tuliokuwa nayo si hii ya sasa hivyo kuwa vulnerable na nchi yoyote ni kitu possible. Hapa si suala la mipaka ni suala la 'Intelligence'
Kuhusu intelligence hapo no dought naunga mkono kwa huu mfumo, huu ndio msingi mzima wa usalama kwa yeyote, hali yoyote, wakati wowote na mahali popote pale, kwasababu kama utakua na uwezo wa kung'amua/kutambua hatari iliyopo mbele na namna sahihi ya kukabiliana nayo, utakua imara no matter how vulnerable you are. Tuchukulie mfano taifa la Israel walikua katikati lakini wanaendelea ku-survive hadi leo.
Lakini pia unaweza kua safe kwa maana kwamba una jeshi imara, geographically well positioned na technology kubwa lakini maadui wakiamua hawawezi wakakosa uzaifu wako, tena kupitia humohumo ambamo wewe unaona upo vizuri, hivyo basi kua na intelligence iliyotukuka ndio jambo la msingi zaidi. Chukulia mfano shambulio la September 11(world trade center) kule USA na hili la juzi hapo Israel.
Hoja ya ulinzi na usalama kama sababu za Muungano, ilikuwepo, HAIPO kwasasa. Dunia imebadilika sana
Ni kama hoja ya kuwa na makao Makuu Dodoma kwasababu za usalama, si kweli!
Mkuu mimi naona bado kigezo cha usalama kinanguvu kwasababu kama ulivyosema kwasasa hakipo, je? Vipi kesho na keshokutwa, Kwakua dunia haipo static inaenda inabadilika, basi tutegemee lolote linaweza kutokea, Mkuu mimi nahisi mbeleni huko kama tutakua tishio kwa namna moja ama nyingine hii zanzibar itatutumika kimkakati kitu-destabilize kidiplomasia kama ilivyo;
China kwa Hong Kong,
China kwaTaiwan,
China kwa Philippine,
Russia kwa Ukraine, na pia....
Cuba kwa USA.

Kitu ambacho Nimeki-note intelligence tulionayo si haba ila tatizo liko kwa watendaji/utekelezaji hauna ufanisi wakutosha sometimes wanapuuzia... nahisi labda yawezekana...
=kuto kukamilika kwa ushahidi,
=hawana uhakika na chanzo cha taarifa,
=wanatathimini ghalama,
=vitendea kazi duni,
=miundo mbinu hafifu.
 
Unatumia aliki ya kiutuuzima kuvumilia tusi lakini mkuu unaumia kwa ndani.

Tusi la kisiasa linauma sana mkuu.
Kwanza sio kila tukano ni tusi!, neno mkorofi sio tusi! na wala sio tukano!, ila pia ni kweli kuna members humu wana midomo michafu, na kuna watu humu tuna ngozi ngumu Kobe utasubiri! hivyo tunavumilia yote!.
P
 
Nakuelewa mkuu, badala ya ukorofi isomeke "uchokozi" au "uchochezi"?!😄
Duh...!, sasa nimekuwa mkorofi!, labda kwa vile kuna watu wanawajua watu kuliko wanavyo jijua wenyewe, labda unieleze nina ukorofi gani?.

Ila hii ya uchochezi ni kubwa kuliko! kwasababu uchochezi ni kosa la jinai!, nimefanya uchochezi gani?.
P
 
Kwanza Economic Intelligence specifically kwenye bandari ikijumuisha mnyororo mzima wa biashara, usafiri na usafilishaji;
Geographical location ya zanzibar imeji-position sehemu mbaya ukilinganisha na pwani ya tanganyika huku,
hasa ukizingatia routes za usafilishaji na miundombinu yake, ukiachilia mbali kua bandari muhimu, kubwa na shindani ukanda huu zipo karibu na zanzibar lakini pia ndio eneo pekee lililokaa kimkakati katika kuhakikisha mizigo ya majirani zetu inawafikia kwa wakati, huku ukizingatia ushindani na majirani zetu Kenya, msumbiji hata Angola kule.
Sijui unataka kueleza nini, kwamba, Majirani watatumia bandari za Zanzibar kuliko za Tanganyika!!
Jiografia ipi inakueleza hivyo! Ironically, bila Tanganyika , Zanzibar inawafikia vipi Majirani zetu?
Bandari za Beira, Lamu, Mombasa ndio washindani kwasababu zina access na 'inland' siyo Zanzibar
Hakuna hoja!


Pili vitisho vya kigaidi, yanaweza yakaibuka makundi ya kigaidi yenye itikadi kali za kidini ikawa ngome yao kule, wakatuletea shida bara huku Kwakua tutakua tumekosa udhibiti wa moja kwa moja.
Haya ni madai ya kukaririshwa tu. Kenya inashambuliwa na Al Shabab kama ilivyo Uganda. Msumbuji yapo makundi ya kigaidi kama ilivyo Congo na Rwanda. Hili la kusema Zanzibar kuna siasa kali ni hoja za kukaririshwa. Kwani Dini ipo Zanzibar peke yake? Yaani hayo makundi ya siasa kali hayawezi kutokea Mombasa au Kado Delgado ni lazima yatokee Zanzibar. Na ugaidi hasa ni kitu gani!. Please hizi ni hoja za kukaririshwa, ziache
Mkuu mimi naona bado kigezo cha usalama kinanguvu kwasababu kama ulivyosema kwasasa hakipo, je? Vipi kesho na keshokutwa, Kwakua dunia haipo static inaenda inabadilika, basi tutegemee lolote linaweza kutokea, Mkuu mimi nahisi mbeleni huko kama tutakua tishio kwa namna moja ama nyingine hii zanzibar itatutumika kimkakati kitu-destabilize kidiplomasia kam
Hakuna kitu ni hoja tu za kukaririshwa toka enzi hizo kuhusu Usalama.
 
Kwanza sio kila tukano ni tusi!, neno mkorofi sio tusi! na wala sio tukano!, ila pia ni kweli kuna members humu wana midomo michafu, na kuna watu humu tuna ngozi ngumu Kobe utasubiri! hivyo tunavumilia yote!.
P
Hahaa mkuu, umesema wewe nimtu poa, kuwaambia watu humu wanamidomo michafu ni ukorofi pia.
 
Hahaa mkuu, umesema wewe nimtu poa, kuwaambia watu humu wanamidomo michafu ni ukorofi pia.
Mkuu Liwagu japo ni kweli mimi ni mtu poa sana ila simaanishi mimi ni malaika!, na mimi ni binadamu tuu, I'm only a human being na nina madhaifu yangu kama binadamu mwingine yeyote, na moja ya dhaifu langu kubwa ni kuusema ukweli no matter what, bila kujali ukweli huu utamfurahisha nani au utamuudhi nani!, as long as ni ukweli nitausema. Sasa kama kwa kuwaambia watu ukweli nitatafsiriwa ni mkorofi, then mimi ni mkorofi.
P
 
Kagame ni kikaragosi cha Marekani katika maslahi yake pale Kongo.

Juzi, mkuu wa kurugenzi ya intelijensia ya USA ameenda kuwapatanisha Kagame na Tshekedi.

Kwamba jeshi la Kongo liache kushirikiana na FDLR kwasababu ni tishio kwa utawala wa Kagame na utawala wake pale Kigali.

Kwa akili ya kawaida tu, sitarajii Tshekedi kuafikiana na pendekezo hilo.

Ni sawa na kupendekeza, Kagame awaondoe wapiganaji wa 'March 23 Movement' ndani ya Kongo.

Kwa maana hiyo, pendekezo linamlinda Kagame kuliko Tshekedi.
Shukurani sana mkuu msakaa jr ila nafikiri Rais Tsheked akiamua kuwa na urafiki na Urusi pamoja na kundi la Wagnar group Mmarekani na vibaraka vyao hapo Congo anakalishwa chini.
 
Sijui unataka kueleza nini, kwamba, Majirani watatumia bandari za Zanzibar kuliko za Tanganyika!!
Hapa nililenga mipaka ya zanzibar hasa baharini kama tukitengana, haiwezi ku-interfere shughuli zetu za bandari.

Wasiwasi wangu ndio ulikua hapo, ila kama tukitengana na bado tukawa na mlango wa bahari unaojitegemea bila kukatiza territory ya visiwani basi sioni shida yoyote.
 
Mkuu Liwagu japo ni kweli mimi ni mtu poa sana ila simaanishi mimi ni malaika!, I'm only a human being na nina madhaifu yangu, na moja ya dhaifu langu kubwa ni kuusema ukweli no matter ukweli huu utamfurahisha nani au utamuudhi nani!, as long as ni ukweli nitausema. Sasa kama kwa kuwaambia watu ukweli nitatafsiriwa ni mkorofi, then mimi ni mkorofi.
P
"Sasa kama kwa kuwaambia watu ukweli nitatafsiriwa ni mkorofi, then mimi ni mkorofi."
P

Ndio,wewe ni mkorofi,
Mimi ni mmoja wa members wengi wanao soma sana madazako humu.
Wewe nimkorofi kama ulivyo sema hapo.
Rejea bandiko lako linalo husu DP world kwamba sasa tumegundua tuna wanasheria wa ainagani, nikama unajaribu kuwaweka utupu wa watu humu.
 
Katika mjadala huu kuna wanaoamini kwamba muundo wa sasa wa Muungano ni mzuri bila kutueleza ni kwanini.
Tuangaze haraka tu kwa baadhi ya mambo yanayochanganya.

Kuna Waziri Mkuu wa JMT anayependekezwa na Rais na kuthibitishwa na Bunge la JMT. Ndani ya Bunge kuna Wabunge wa kuteuliwa na Rais kutoka Zanzibar, Wabunge 5 kutoka Baraza la Wawakilishi na Wabunge takribani 70 wa kuchaguliwa.

Waziri Mkuu wa Tanzania anayechaguliwa na Wabunge wa pande zote hana mamlaka katika jambo lolote linalohusu Zanzibar. Kwa mantiki , huyu ni Waziri Mkuu wa Tanganyika ingawa anachaguliwa na Wazanzibar pia. Kituko # 1

Katiba ya 1977 inasema ikiwa Rais au Makamu wa Rais hawapo , Waziri mkuu wa JMT atendesha kikao cha Baraza la Mawaziri (Cabinet). Ndani ya Baraza la Mawaziri yupo Rais wa Zanzibar kama Mjumbe. Kikao hicho kikiendelea Mkuu atakuwa Waziri Mkuu wa JMT, si Rais wa Zanzibar . Kituko #2

Rais SSH ameamuru kujengwe Ofisi ya Waziri mkuu wa JMT na Makamu wa Rais wa JMT Zanzibar.
Waziri mkuu hana mamlaka Zanzibar, Ofisi ya nini ? Makamu wa Rais ni mfungua makongamano hana mamlaka Zanzibar Ofisi ya nini. Ofisi hizo zimejengwa kwa kodi za Tanganyika! Kituko# 3

Wabunge wa Zanzibar ndani ya Bunge la JMT wapo katika kamati za kisekta zinazohusu mambo ya Tanganyika.
Utawaona wakishiriki ukaguzi wa shughuli za Utalii, Tamisemi, Kilimo na ufugaji, elimu, Afya, n.k. mambo yasiyo ya Muungano. Hutaona Wabunge wa JMT katika kamati za kisekta wakienda kukagua shughuli Zanzibar! Kituko#4

Zanzibar wanakusanya pesa za 'VISA' za watalii na kubaki huko. Wafanyakazi waUhamiaji wameajiriwa na Serikali ya JMT ambayo mapato yake ni ya Tanganyika. Kwamba, Tanganyika ina gharama za Mishahara ya Wafanyakazi wa Uhamiaji Zanzibar ili wakusanye mapato ya SMZ! Kituko # 5

Bidhaa yenye idhini kutoka shirika la Viwango Tanzania (TBS) haiwezi kutumika Zanzibar hadi iidhinishe na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS). Bidhaa yenye kuidhinishwa na ZBS inaingia Tanganyika na kutumika bila idhini ya TBS. Kituko# 6

Orodha ni ndefu sana, inaendelea. Karibuni mtetee hoja
 
Back
Top Bottom