Dark days 17/03/20...

Dark days 17/03/20...

Niuruhusu nipitie hoja zako kwa mandiko tofauti

Consistency ni suala la kulielewa jambo na Watanganyika wachache walielewa hili.
Wengi hawakujali sMuungano, waliwakubali Wazanzibar kama Watanzania licha ya Ubaguzi wa Wazanzibar

Watanganyika walikatazwa kujadili Muungano ''taboo' wakiambiwa ni 'Muungano pekee, ni Tunu, n.k.' na kuujadili ilikuwa kama ''Uhaini' Lengo wasijue kwamba wamebeba mzigo peke yao.

Mjadala wa Muungano unajulikana vizuri kwa Wazee kama Warioba, Msekwa, Jenerali kwa uchache wa kuwataja.

Watanganyika wakipigwa marufuku kuujadili kama ilivyoonekana kwa tukio la Mh Mbowe, Wazanzibar waliachwa waseme watakavyo. Siku za nyuma walikuwa na 'slogan' '' kama hamfanyi abcd' tunavunja Muungano.

Wazanzibar wakaeneza uongo kwa kuifanya Zanzibar kama mhanga 'Victim' wa Muungano na si 'mfaidika' Beneficiary. Ikaonekana Zanzibar inaonewa, inanyimwa , inapigwa vita na kauli nyingi za kipuuzi kama hizo.

Kwa mfano, kuundwa kwa tume ya pamoja ya Fedha ilionekana Tanganyika inaficha kitu.
Rais Mwinyi kaweka ukweli waziii akisema mfuko wa pamoja utailazimu Zanzibar kuchangia, itaumia .

Mh Mwinyi alikuwa anamjibu VP OMO wa ACT anayeeneza uongo huo katika mikutano bila aibu! kwa miaka mingi

Kuna Uzi JF wa Zitto (ACT) wa July 2019 ukisema 'eti account ya pamoja' ni ya kugawana mafao ya Muungano.

Zitto anasema tunapaswa kuwalipa Zanzibar Trilioni 7. Uongo mtupu! fedha za Watanganyika ndio mafao ya Muungano? Ni kama vile ARDHI ya Tanganyika imegeuzwa ya Muungano. Zitto hakusema Zanzibar inachangia nini katika mafao ya JMT.

Taratibu tumebomoa uongo wao si kwa uongo bali kwa 'facts' na siku hizi hutawasikia wakisema hovyo .


Lengo la TRA NI kukusanya fedha zote za nchi (JMT) halafu kufanya 'remittance' kule Zanzibar kwa kuwa ina 'status' Pili, kurahisha biashara kwamba mzigo ukilipiwa Zanzibar unaingia bara kwa maana ya ku 'harmonise' shughuli na kuondoa viwango tofauti kati ya Bara na Zanzibar.

Wazanzibar wakakataa na kuanzisha ZRB, hilo likaongeza mzigo wa kodi. Kilichofanyika ni kuacha mapato ya TRA yabaki . Hili likaleta ugumu wa biashara ambao Zanzibar walilamika kwamba nchi moja kwanini bidhaa zilipiwe kodi mara mbili.

Marais wote na hasa JPM alikataa bidhaa kutoka Zanzibar zisiingie bila kodi kwasababu Zanzibar kuna tax evasion kubwa na viwango vya tax ni vidogo sana ukilinganisha na Bara, na inatumika kama uchochoro.

Kwa maana kwamba kontena linaloshushwa Dar es Salaam linalipiwa zaidi kuliko kushushwa Zanzibar.

Kama unakumbuka clip ya Mbunge Ali Kessy alisema ' kontena' la pikipiki ni 40Milioni Dar , kule Zanzibar ni 5 Milioni. Kuna taarifa baada ya JPM utartaibu wa kupitisha bidhaa kutoka Zanzibar umerudishwa tena, kufuta kero

Hakuna tatizo TRA kuacha mapato Zanzibar ikiwa Zanzibar watachangia Muungano kwa njia nyingine.
Pili, hakuna bidhaa zitakazoingia kutoka Zanzibar bila kulipiwa kodi kwa kisingizio cha nchi moja wakati Mtanganyika ataumia kwa kodi zaidi TRA isipopata mapato ya kutosha.

Lakini pia kuna kituko cha Muungano.
Wafanyakazi wa TRA Zanzibar wanalipwa na TRA JMT ingawa mapato yanabaki kwa SMZ.
Ni sawa na kituko cha Wafanyakazi wa Uhamiaji kulipwa na JMT mapato yanatokana na Uhamiaji ni mali ya SMZ.
Shukrani !!
Nikisema nimeelewa moja kwa moja Nitakuwa muongo, ila umenifungua Njia wapi pa Kugusa kama nitataka kutafiti kuhusu hili. Nadhani nitalitumia Andiko lako kama "Checklist" wakati najielimisha na Kudigest kila neno.

Kwa uelewa wangu ni Kuwa Muungano upo hadi leo kwa kuwa CCM wanataka uwepo, Wakiuchoka wao basi utakufa.
Je wanapata nini ambacho sie hatukioni?

As siku Zinaenda CCM inapoteza Nguvu kama taasisi na Kuzalisha "chawa" wa Mwenyekiti. Hivyo atakachowaza mwenyekiti ndio final.
Je tutarajie atakuja tokea "Mwehu" asiyejali legacy za watangulizi wake na kuvunja?
 
Kabla ya Uchaguzi boss alitaka amuweke mrithi wake kwenye kampuni yake, mrithi anayemtaka yeye. Ila kutokana na upinzani mkubwa ndani ya kampuni maamuzi magumu ilibidi yafanyike

Baada ya Uchaguzi kuna mtu alipata uongozi accidentally. Hakuwa chaguo la boss, alipewa sababu ya kuua kambi!

Big boss anayemaliza muda alifanya maamuzi hayo akiamini ataweza kum-control kwakuwa file lake analo na anamjua na amempa ili kunusuru mkatiko mkali kwenye kampuni.

Alijua ataleta umoja ndani ya kampuni. Mambo yalibadilika baada ya new boss kupewa kijiti na kukabidhiwa ofisi!

Alichofanya ni kutengeneza timu yake na kuondoa timu yote ya mtoa kijiti! Akaenda mbele zaidi kupitia files na kuanza kutindua maslahi ya mtoa kijiti kwenye kampuni!

Mbaya zaidi, akamfukuza mwenye kijiti, au the old boss kwenye kampuni anayoamini ni ya kwake na bila yeye haiendi!

The New Boss alipewa notification na maelekezo kuhusu mambo kadhaa mara kadhaa, ila aliskika akijibu, yeye ndio mwenye kijiti na hakuna wa kumpangia! Hataki maelekezo na kwanza haelekezeki!

Alijibu hivyo hadharani bila woga wala hofu! Kwakuwa alimjua adui ni nani! Alianza mpaka kutangaza kuwa kampuni ile sasa ni yake na chini yake inafanya makubwa sana, na wale wa zamani walikuwa wanaifilisi!

Haikuwa habari njema saaaana kwa mwenye kijiti kabla ya uchaguzi na backup system yake! Discussion zilifanywa mara kadhaaa kumjadili new big boss in town kumbe the new boss alikuwa anawarecord all the time!

Alichokifanya ni kuvujisha badhi ya convos za washirika wa adui mkuu kum-notify ironically kuwa anajua wanachomjadili na anajua hawampendi! Na amejipanga au ameji-sacrifise yupo tayari kwa lolote!

Shida ikaanza, after a discover kuwa deal za the old big boss zinazimwa na zinachukuliwa kwa nguvu na stakeholders wapya chini ya maelekezo ya the new big boss na stakeholders wa zamani wanatupwa nje ya ukuta!

Ikatisha zaidi baada ya boss mpya kutaka kuwa CEO wa milele! Na akapanga watu wa kuhakikisha hilo linakamilika!

The old boss akakaa chini, akafikiria akaona kama huyu 4 years tu kanifanya hivi je 20 years to come?

Muda ukaenda, the old boss played dead! But came up with a plan, involving the closest friend and the system in the company kama tunavyojua, the old the wine...... the fine it becomes!

The new Big boss kajichanganya during campaings za kuusaka u-CEO tena, akapigwa tukio, after Uchaguzi wa pili wa kampuni only three months akatema ndoano!

Msaidizi wake akaitwa chemba, maelekezo akapewa achukue kijiti, afanye reform mambo kwabu yanapaswa kurudi kama zamani!

Msaidizi kuangalia hali ilivyo, akaanza kurudisha the old structure kwenye kampuni! The only difference ni yeye ndio CEO but behind the scene there is another CEO!!

Let see will the new boss stick to the plan? or...


Itaendelea.......


Guess the company!??

Muendelezo Soma Dark days 17/03/20.…...

Angalizo: Story hii haihusiani na chochote Dark days 17/03/20...
Haya Series ya Dec 1
 
Tatizo la Muungano linasababishwa na mambo mengi ikiwemo 'taboo' yaani mwiko kuuongelea
Muungano hautetewi kwa hoja bali vihoja na viroja. Ni wa pekee, ni tunu, ni muhali n.k.

Watanganyika wakapigwa marufuku kuuongelea kama tulivyoona sakata la Mbowe lililoleta kelele zisizo na kichwa wala miguu. Wazanzibar kama kawaida wakapewa 'free ride' ya kutukana kama tunavyowasikia akina Masoud Othman, Jussa, Duni n.k.

Tunapoonyesha matundu ya Muungano wenye akili timamu watajifunza, wenye uelewe katika umbali wa pua hawatatuelewa. Bila kuuongelea Muungano na yaliyojificha chini ya kapeti ipo siku Muungano utakuwa 'glass' na ikianguka ni kuvunjika papo hapo.

Kituko cha Muungano cha leo.
Wazanzibar wanasema mambo ya Muungano yabaki 11 ya mkataba wa awali.

Ndani ya Bunge kuna Wabunge 393 akiwemo AG. Ukimuondoa AG wanabaki 392 na ukiondoa 80 wa Zanzibar wanabaki 312 wa Tanganyika.

Ikiwa Bajeti ya Kilimo, Mifugo , Afya au Elimu itapigiwa kura na kufungana 156/156 kati ya Watanganyika wa YES na NO, watakaoamua bajeti hizo ni Wazanzibar 80, wale wale wasiotaka mambo ya Muungano yaongezwe.

Wabunge wa Zanzibar wapo kamati za BUNGE za mambo yanayohusu Tanganyika.
Katika kamati hizo Wazanzibar hao wana maamuzi yanayogusa masilahi ya Watanganyika.

Wakirudi Zanzibar wanadai hawataki mambo ya Muungano yaongezwe , mambo yale yale waliyokuwa wanayasimamia katika kamati huko Nkasi, Nyamagana, Kadewele, Isevya na Handeni kusiko wahusu.
Yaani issue sana
 
Back
Top Bottom