Alexander Lukashenko
JF-Expert Member
- Sep 9, 2017
- 4,140
- 9,667
Shukrani !!Niuruhusu nipitie hoja zako kwa mandiko tofauti
Consistency ni suala la kulielewa jambo na Watanganyika wachache walielewa hili.
Wengi hawakujali sMuungano, waliwakubali Wazanzibar kama Watanzania licha ya Ubaguzi wa Wazanzibar
Watanganyika walikatazwa kujadili Muungano ''taboo' wakiambiwa ni 'Muungano pekee, ni Tunu, n.k.' na kuujadili ilikuwa kama ''Uhaini' Lengo wasijue kwamba wamebeba mzigo peke yao.
Mjadala wa Muungano unajulikana vizuri kwa Wazee kama Warioba, Msekwa, Jenerali kwa uchache wa kuwataja.
Watanganyika wakipigwa marufuku kuujadili kama ilivyoonekana kwa tukio la Mh Mbowe, Wazanzibar waliachwa waseme watakavyo. Siku za nyuma walikuwa na 'slogan' '' kama hamfanyi abcd' tunavunja Muungano.
Wazanzibar wakaeneza uongo kwa kuifanya Zanzibar kama mhanga 'Victim' wa Muungano na si 'mfaidika' Beneficiary. Ikaonekana Zanzibar inaonewa, inanyimwa , inapigwa vita na kauli nyingi za kipuuzi kama hizo.
Kwa mfano, kuundwa kwa tume ya pamoja ya Fedha ilionekana Tanganyika inaficha kitu.
Rais Mwinyi kaweka ukweli waziii akisema mfuko wa pamoja utailazimu Zanzibar kuchangia, itaumia .
Mh Mwinyi alikuwa anamjibu VP OMO wa ACT anayeeneza uongo huo katika mikutano bila aibu! kwa miaka mingi
Kuna Uzi JF wa Zitto (ACT) wa July 2019 ukisema 'eti account ya pamoja' ni ya kugawana mafao ya Muungano.
Zitto anasema tunapaswa kuwalipa Zanzibar Trilioni 7. Uongo mtupu! fedha za Watanganyika ndio mafao ya Muungano? Ni kama vile ARDHI ya Tanganyika imegeuzwa ya Muungano. Zitto hakusema Zanzibar inachangia nini katika mafao ya JMT.
Taratibu tumebomoa uongo wao si kwa uongo bali kwa 'facts' na siku hizi hutawasikia wakisema hovyo .
Lengo la TRA NI kukusanya fedha zote za nchi (JMT) halafu kufanya 'remittance' kule Zanzibar kwa kuwa ina 'status' Pili, kurahisha biashara kwamba mzigo ukilipiwa Zanzibar unaingia bara kwa maana ya ku 'harmonise' shughuli na kuondoa viwango tofauti kati ya Bara na Zanzibar.
Wazanzibar wakakataa na kuanzisha ZRB, hilo likaongeza mzigo wa kodi. Kilichofanyika ni kuacha mapato ya TRA yabaki . Hili likaleta ugumu wa biashara ambao Zanzibar walilamika kwamba nchi moja kwanini bidhaa zilipiwe kodi mara mbili.
Marais wote na hasa JPM alikataa bidhaa kutoka Zanzibar zisiingie bila kodi kwasababu Zanzibar kuna tax evasion kubwa na viwango vya tax ni vidogo sana ukilinganisha na Bara, na inatumika kama uchochoro.
Kwa maana kwamba kontena linaloshushwa Dar es Salaam linalipiwa zaidi kuliko kushushwa Zanzibar.
Kama unakumbuka clip ya Mbunge Ali Kessy alisema ' kontena' la pikipiki ni 40Milioni Dar , kule Zanzibar ni 5 Milioni. Kuna taarifa baada ya JPM utartaibu wa kupitisha bidhaa kutoka Zanzibar umerudishwa tena, kufuta kero
Hakuna tatizo TRA kuacha mapato Zanzibar ikiwa Zanzibar watachangia Muungano kwa njia nyingine.
Pili, hakuna bidhaa zitakazoingia kutoka Zanzibar bila kulipiwa kodi kwa kisingizio cha nchi moja wakati Mtanganyika ataumia kwa kodi zaidi TRA isipopata mapato ya kutosha.
Lakini pia kuna kituko cha Muungano.
Wafanyakazi wa TRA Zanzibar wanalipwa na TRA JMT ingawa mapato yanabaki kwa SMZ.
Ni sawa na kituko cha Wafanyakazi wa Uhamiaji kulipwa na JMT mapato yanatokana na Uhamiaji ni mali ya SMZ.
Nikisema nimeelewa moja kwa moja Nitakuwa muongo, ila umenifungua Njia wapi pa Kugusa kama nitataka kutafiti kuhusu hili. Nadhani nitalitumia Andiko lako kama "Checklist" wakati najielimisha na Kudigest kila neno.
Kwa uelewa wangu ni Kuwa Muungano upo hadi leo kwa kuwa CCM wanataka uwepo, Wakiuchoka wao basi utakufa.
Je wanapata nini ambacho sie hatukioni?
As siku Zinaenda CCM inapoteza Nguvu kama taasisi na Kuzalisha "chawa" wa Mwenyekiti. Hivyo atakachowaza mwenyekiti ndio final.
Je tutarajie atakuja tokea "Mwehu" asiyejali legacy za watangulizi wake na kuvunja?