Miaka 2,300, miaka 1335, miaka 1290 na miaka 1260, iliyotajwa kwenye kitabu cha nabii Daniel, yote inaishia mwaka 1798.
Yote ina anzia nyakati tofauti, lakini yote ina ishia mwaka 1798.
Miaka 2,300 ina anzia 503 BC.
503 BC + 2300 + 1 (tunaongeza mwaka 1, kutoka BC hadi AD, kwasababu, hakunaga 0 BC au 0 AD) = 1798 AD.
Miaka 1335 ina anzia 463 AD.
463 AD + 1335 years = 1798 AD.
Miaka 1290 ina anzia 508 AD.
508 AD + 1290 years = 1798 AD.
Miaka 1260 ina anzia 538 AD.
538 AD + 1260 years = 1798 AD.
Miaka 490 iliyotajwa kwenye kitabu cha Daniel (wiki 70, ambazo ni siku 490, ambazo ni, miaka 490) ina anzia 458 BC, kwenye decree/amri ya mfalme Artaxerxes wa himaya ya Uajemi, aliyompatia Ezra. Na ina ishia mwaka 33 AD, ambapo Stephen alipigwa mawe na wayahudi wasioamini injili ya Bwana Yesu Kristo. Na hivyo injili ya Bwana Yesu Kristo kuanza rasmi kupelekwa kwa mataifa.
458 BC + 490 years + 1 (tunaongeza mwaka 1, kutoka BC hadi AD, kwasababu, hakunaga 0 BC au 0 AD) = 33 AD.
Bwana Yesu Kristo, aliteswa, alisulubiwa, alikufa, alizikwa kaburini, alifufuka kutoka katika wafu, alipaa kwenda mbinguni, mwaka 30 AD. Roho Mtakatifu alishuka siku ya Pentekoste, mwaka 30 AD.
Mwaka 2030 AD, ni miaka 2000 ya injili kuhubiriwa kwa mataifa yote duniani, ikianzia Jerusalem.
Kwahiyo, adventists (na sda), walikosea pale waliposema kwamba mwaka 1844, ulikuwa mwaka wenye maana ya kinabii, kwasababu waliamini kimakosa kwamba miaka 2,300 ina ishia mwaka 1844.
Walikosea kwenye kupiga mahesabu ya miaka, na pia walikosea kwenye maana ya unabii wa kinachotokea mwishoni mwa hiyo miaka 2,300.
Mwaka 1844 haukuwa mwaka wenye maana ya kinabii. Na hivyo hawakutakiwa kutegemea tukio lolote la kinabii kutokea mwaka huo.
Mwaka 1798 AD ndio ulikuwa mwaka wenye maana ya kinabii. Kanisa huku duniani lilianza kusafishwa mwaka huo (unto 2,300 days, then shall the sanctuary be cleansed, here one day represents one year).
Pia wafaransa walimchukua mateka mnyama wa Ufunuo 13, mwaka 1798 AD (mnyama huyu alipata jeraha la mauti mwaka 1798 AD), na hivyo watakatifu, waliokolewa kutoka mikononi mwa mnyama huyo, mwaka huo, baada ya kuwa mikononi mwake kwa miaka 1,260. Mnyama ni ufalme wa kidini wa mpinga kristo.
Nguvu za ufalme wa mnyama, zinatarajiwa kurejea kikamilifu (jeraha lake la mauti linatarajiwa kupona kabisa) miaka kadhaa kutoka sasa. Probably in 2026 AD.
Bwana Yesu Kristo anatarajiwa kurudi baada ya mwaka 2030 AD.
Hatujui kama atarudi mwaka huo au miaka michache baada ya mwaka huo au miaka mingi baada ya mwaka huo.
Kwa kipindi cha miaka 3.5 kabla ya kurudi kwa Bwana Yesu Kristo; ushuhuda wa kweli wa Biblia utakuwa 'umekufa' (mashahidi wawili watakuwa wamekufa), baada ya kuwa umeshambuliwa na mnyama ambae atakuwa amepona jeraha la mauti (Ufunuo 11:7-10).
Na chapa ya mnyama itakuwa inatawala bila ushindani, kutoka kwa ushuhuda wa kweli wa Biblia ulio hai, kwenye kipindi hicho cha miaka 3.5.
Kwenye kipindi hicho cha miaka 3.5 hao mashahidi wawili watakuwa wamekufa, lakini ushuhuda wao utaendelea kukumbukwa, kwahiyo watakuwa bado wanashuhudia, ingawa watakuwa wamekufa.
Chapa ya mnyama ni mafundisho ya uongo ya kidini, ambayo yanadhaniwa kuwa ni mafundisho ya kweli ya kikristo, lakini kiukweli na kiuhalisia, yanapingana na injili ya kweli ya Bwana Yesu Kristo, na pia yanapingana na amri 10 za Mungu (Kutoka 20:1-17).
Mji wa kiroho wa Babeli, ulianza kuwepo duniani, toka pale Adam na Hawa, walipokula tunda la kujua mema na mabaya. Uliendelea kuwepo baada ya gharika ya Noah, pale Nimrod na wenzake walipoanza kujenga mnara wa Babeli. Mji wa kiroho wa Babeli utachomwa moto kabisa, pale Bwana Yesu Kristo atakaporudi mara ya pili, na pia dunia yote itachomwa moto wakati huo. Wakati huo, Bwana Yesu Kristo atawachukua watakatifu walio kufa (atawafufua wakati huo) na walio hai, na atawapeleka mbinguni, na kukaa nao mbinguni miaka 1,000.
Kwenye kipindi hicho cha miaka 1,000 dunia itakuwa imekaa katika hali ya kuharibika, baada ya kuchomwa moto na Bwana Yesu Kristo pale aliporudi mara ya pili.
Miaka 1,000, baada ya ujio wa pili wa Bwana Yesu Kristo, dhana ya mji wa kiroho wa Babeli (dhana ya mji wa kiroho, na sio mji wa kiroho wenyewe) itaharibiwa kabisa, na kupotea kabisa, na haitarudi tena. Ufufuo wa pili utakuwa umetokea kipindi hiki, watu waovu ndio watakao shiriki kwenye ufufuo wa pili, na waovu watachomwa moto na kuteketea kabisa kipindi hiki, baada ya kushiriki kwenye ufufuo wa pili, na baada ya hukumu, itakayotolewa kwenye ile siku kubwa ya mwisho ya hukumu.
Na Mungu ataumba mbingu mpya na dunia mpya, na Jerusalem mpya utashuka kuptoka mbingu mpya na kuja kwenye dunia mpya.
Note that, watakatifu 144,000 walitiwa muhuri wa kiroho wa Mungu wa kweli, kipindi cha Bwana Yesu Kristo na kipindi cha mitume (apostles) wa Bwana Yesu Kristo, na hawa wote 144,000 ni waisraeli (wa enzi zile) walioamini injili ya Bwana Yesu Kristo.
Wakristo kutoka mataifa (gentiles walio na wanao amini injili ya kweli ya Bwana Yesu Kristo), ambao sio waisraeli (wa enzi zile) nao pia wanapigwa muhuri wa kiroho wa Mungu wa kweli (mpaka pale dunia hii itakapoisha), lakini wao sio sehemu ya wale 144,000.
Kipindi hiki, hakuna apostles, kwasababu, apostles ni cheo cha juu kabisa ndani ya kanisa. Na pia, criteria ya kuwa apostle ni watu waliomwona Bwana Yesu tangu alipoanza kuhubiri injili, hadi alipopaa mbinguni. Na Bwana Yesu Kristo ndio aliwachagua kuwa apostles.
Paul ni exception, na huenda Paul pia aliwahi kumwona na kumsikia Bwana Yesu Kristo, wakati akiwa duniani, ingawa wakati huo Paul alikuwa haamini injili ya Bwana Yesu Kristo. Na pia apostle ni lazima ilikuwa awe ni muisraeli (wa enzi zile) alieamini injili ya Bwana Yesu Kristo.
Kwahiyo, ukisikia siku hizi, mtu au kiongozi wa kidini anajiita apostle (mtume) wa Bwana Yesu Kristo, ujue kuna uwezekano mkubwa sana kwamba anadanganya; kiukweli yeye sio apostle (mtume) wa Bwana Yesu Kristo.
Pia ukisikia, siku hizi, mtu anajiita yeye ni nabii wa Bwana Yesu Kristo, ujue kuna uwezekano mkubwa sana kwamba anadanganya; kiukweli yeye sio nabii (prophet) wa Bwana Yesu Kristo.
Nabii ni cheo kikubwa cha pili kwenye kanisa baada ya cheo cha apostle. Cheo cha apostle ni cheo cha kwanza, nabii ni cheo cha pili ndani ya kanisa.
Nabii anatakiwa aishike na kuifundisha injili ya kweli ya Bwana Yesu Kristo, pamoja na amri 10 za Mungu (pamoja na sabato ya siku ya saba). Pia nabii huwa anawasiliana na Roho Mtakatifu. Na kutokana na hili, nabii pia huwa anayajua vizuri sana sana maandiko matakatifu ya Biblia. (Note that mtu anaweza kuyajua vizuri sana sana maandiko matakatifu ya Biblia, bila ya kuwa nabii na bila ya kuwa mtume).
Pia Bwana Yesu Kristo na Roho Mtakatifu ndio wanaompa mtu hiko cheo cha unabii, au hiyo karama ya unabii. Na sio mtu husika kujiteua mwenyewe kuwa nabii.
Mkristo wa kweli (kutoka mataifa) ambae sio muisraeli (wa enzi zile) anaweza kuwa na cheo cha unabii au karama ya unabii.
Mama Ellen White (wa sda), hakuwa na cheo cha unabii, na hakuwa na karama ya unabii, kama alivyokuwa akisema. Alikuwa anavunja amri ya 9 (Usimshuhudie jirani yako uongo, ikimaanisha pia, usitoe ushuhuda wa uongo), na pia alikuwa anavunja amri ya 3 (Usilichukulie bure jina la BWANA Mungu wako, ikimaanisha mambo mengi, na pia ikimaanisha, usilitumie jina la BWANA Mungu wako, kutoa unabii wa uongo). Na pia kwenye baadhi ya mafundisho yake (na kwenye baadhi ya visions zake na dreams zake), amepingana na mafundisho ya kweli ya Biblia.