Darren Jason Watkins JR (ishow speed) kijana aliyeifungua macho ya dunia kuhusu China

Darren Jason Watkins JR (ishow speed) kijana aliyeifungua macho ya dunia kuhusu China

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Katika umri mdogo ambao wengi hujifunza tu kuhusu dunia kupitia vitabu na mitandao, Darren Jason Watkins Jr, maarufu kama IShowSpeed, amevuka mipaka na kufanya historia kwa macho yake mwenyewe.
images - 2025-04-15T210024.609.jpeg
Akiwa kijana mwenye ushawishi mkubwa mtandaoni, Ishow Speed amepata kulitembelea taifa la China na kuonesha ulimwengu sura halisi ya taifa hilo—sura ambayo mara nyingi hufunikwa na propaganda za vyombo vya habari kutoka Magharibi.
hq720 (2).jpg

Ni huyu kijana amepata kuonesha uwazi wa picha wa namna taifa la China lilivyopiga hatua kubwa kwenye maendeleo, ameonesha picha zisizo na ubaguzi, achana na BBC, CNN na VOA, Ishow Speed amewaonesha watu namna maendeleo ya China yalivyo katika kiwango cha juu.
images - 2025-04-15T205950.767.jpeg

Kupitia mitandao ya kijamii, Darren hupendelea kurusha matangazo ya moja kwa moja akiwa mitaani, akionyesha maisha ya kawaida ya Wachina, mila, teknolojia, vyakula na ukarimu wao wa ajabu. Safari yake haikuwa tu burudani, bali somo kwa dunia linalofunua undani wa jamii ambayo wengi hawajaifahamu kwa karibu.
IShowSpeed-1.png

Kwa safari yake ya kihistoria nchini China, Ishow Speed ameonesha unafiki ambao mara kadhaa tumekuwa tukioutazama kwenye vituo vya habari vya kimataifa. Ni wazi kuwa Ishow Speed amewakera wazungu kwa kiasi kikubwa kwa kuonesha unafiki wao nje nje.
images - 2025-04-15T205912.643.jpeg

Kuna kiasi kikubwa sana cha watu walikuwa wakiamini kuwa Miundombinu ya China ni ya kawaida. Ila bwana mdogo ameionesha dunia utamaduni wa China pasipo upendeleo.
images - 2025-04-15T210024.609.jpeg

Kitu cha msingi sana kwa bwana mdogo ni kujiwekea usalama mkubwa sana maana anaweza kufanyiwa jambo baya lolote ili asiendelee na safari zake hizo. Tusione ajabu kuwa dogo ana ndoto ya kwenda Cuba, Korea Kaskazini pamoja na Urusi kuonesha maisha ya mataifa hayo.
 
Hata bongo kuna sehemu nzuri sana, pia kuna slums.
 
Anayesema China ni duni na masikini ni nani?.

Kwa sasa USA pekee ndiye anayemzidi pato la Taifa Duniani pote, sasa Taifa namba mbili kwa pato Duniani litakuwaje masikini na duni kimaisha?.

Hapo pande zote mnatufanyia propaganda
 
Back
Top Bottom