Darsa ya Ramadhan 1 (2022): Mke na Mume hawaruhusiwi kukutana kimwili, haswa katika mchana wa mwezi wa Ramadhan

Darsa ya Ramadhan 1 (2022): Mke na Mume hawaruhusiwi kukutana kimwili, haswa katika mchana wa mwezi wa Ramadhan

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
Assalam alaikum

Katika darsa letu la leo tuta tazama baadhi ya hukumu nyeti zinazo ambatana na usiku wa mwezi wa Ramadhan. Tukizijua hukumu hizi swaumu zetu zitakuwa katika njia iliyo nyooka. Na kama hatutazijua hukumu hizi basi swaumu zetu zita haribika, itatubidi kulipa deni pamoja na kulipa kafara. Jambo ambalo ni kubwa sana!

Hebu na tutazame kwa ukaribu aya inayo ambatana na hukumu za usiku wa mwezi wa Ramadhan.

Mwenyezi Mungu anasema katika sura al Baqara, sura ya pili aya 187 kama ifuatavyo;

“Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate kumcha”

Katika dini ya Kiislamu hairuhusiwi kuwa na maingiliano kati ya mwanamume na mwanamke bila ya kuoana. Endapo watu wataamua kuwa na maingiliano hayo bila ya ndoa, hiyo ita itwa uzinifu au zinaa.

Na zinaa ni kitendo kibaya kabisa mtu kukifanya kwani kinaleta ufisadi wa hali ya juu katika jamii zetu. Madhara yake ni mengi na husababisha maafa makubwa. Na la muhimu zaidi ni kuwa zinaa inamchukiza sana Mwenyezi Mungu na Mtume wake Muhammad (swallallahu alaihi wa aalihi wa sallam).

Maingiliano ya kijinsia kati ya mume na mke yanaruhusiwa baada ya ndoa, na yanaruhusiwa katika nyakati zote. Kuna wakati mke na mume hawaruhusiwi kukutana kimwili, haswa katika mchana wa mwezi wa Ramadhan.

Ama maingiliano hayo yameruhusiwa na Mola Mtukufu katika usiku wa Mwezi wa Ramadhan. Ruhusa hii imo ndani ya Qur’an.

Mwenyezi Mungu anasema;

أُحِلَّ لَكُمْ لَيْلَةَ الصِّيَامِ الرَّفَثُ إِلَىٰ نِسَائِكُمْ ۚ هُنَّ لِبَاسٌ لَكُمْ وَأَنْتُمْ لِبَاسٌ لَهُنَّ ۗ عَلِمَ اللَّهُ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَخْتَانُونَ أَنْفُسَكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ وَعَفَا عَنْكُمْ ۖ

“Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni”


83b10cc0270c4d118f04b81f51434f3b.jpg
 
Ramadhan is prescribed for you and those before you so may achieve Taqwa 'the fear and remembrance of Allah'
AllahuAkbar Tabarakallah

InshaaAllah Mwenyezi apokee sala zetu Amin🙏🏽
Allahuma Barik
 
Watoto hutafutwa usiku.
Hawa wa mchana ndo huwa yanakuaga hayana akili kabisa.
Unafanya ndoa mchana. Subiria uzae toto la ajabu.
 
Ngoja waje kuchukua miongozo...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom