Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) umetangaza marufuku kwa Watoa Huduma Binafsi kujihusisha na utoaji wa taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu utekelezaji wa michakato mbalimbali ya Mradi wa BRT ikiwemo suala la mikataba na mipango.
Taarifa kwa Vyombo vya Habari, Agosti 4, 2025 iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa DART, Dkt. Athumani J. Kihamia imesisitizwa kwamba taarifa zozote kuhusu masuala ya kiutendaji, ununuzi wa mabasi, sera au mipango ya waendeshaji wenzao zitatolewa na DART pekee na sio vinginevyo.
“Mawasiliano yoyote ya umma kuhusu utekelezaji wa Miradi ya BRT, Sera au Mipango rasmi lazima yatoke kupitia DART pekee. Hakuna mtoa huduma anayeruhusiwa kuzungumza na Vyombo vya Habari,” amesema Dkt. Kihamia.
Aidha, ameongeza kuwa kumekuwa na taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na baadhi ya watoa huduma binafsi zikihusisha majukumu ya usimamizi, ununuzi wa mabasi na shughuli za waendeshaji wenzao.
Dkt. Kihamia alifafanua kuwa taarifa hizo ni batili na zinakiuka taratibu rasmi za mawasiliano zilizowekwa na DART. Amesema hakuna mtoa huduma yeyote anayeruhusiwa kuzungumza na Vyombo vya Habari kuhusu masuala ya kifedha, mikataba ya ununuzi wa mabasi, au mipango ya waendeshaji wenzao.
DART imesisitiza kuwa inaendelea kujitahidi kuhakikisha utekelezaji wa Mradi wa BRT unafanyika kwa weledi, huku wakitoa wito kwa watoa huduma kuheshimu majukumu yao bila kuingilia mamlaka ya msimamizi.
Aidha, Dkt. Kihamia alibainisha kuwa katikati ya mwezi huu (Agosti 2025) wanatarajia kuanza kutoa huduma kupitia Mradi wa BRT Awamu ya Pili – Mbagala, ameongeza kuwa kwa kuunganisha Awamu ya Kwanza na ya Pili, hadi kufikia Oktoba, wanatarajia kuwa na zaidi ya mabasi 930 ambayo yataletwa na wawekezaji.
Ikumbukwe kuwa mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), ambapo tayari wawekezaji kadhaa wamepewa mikataba kupitia mashirikiano hayo.