Hizi Mwendokasi safari zake hazikupangwa kutokana na mahitaji. Wamenakili vituo vya daladala na wao wakapita humohumo. Ingekuwa suluhisho kama wangenakili vituo vya kuanzia au kuishia au kugeuzia vilivyotumika kabla daladala hazijapakwa mikanda ya njia.
Mfano huku kwetu Dar Barabara ya Nyerere, kuna daladala zilikuwa zinaanzia/zinaishia/zinageukia Vingunguti, Uwanja wa Ndege, Banana, Mombasa na Gongo la Mboto. Hizi terminal za kuanzia/kuishia/kugeukia ndizo zilipaswa kutambulishwa kwenye Mwendokasi. Nina maana Mwendokasi zilipaswa kuanzia/kuishia/kugeukia vituo hivyo nilivyotaja. Kusingekuwa na vurugu vituoni