Data driven decisions. Kwanini NALA wawe na HQ Kenya na sio Tanzania?

Yap mkuu well noted.

So hapa mchawi wetu haswa nia

1. Lugha - Watanzania wengi hawajui lugha ya malkia kwahiyo hawavuki maji.

2. Regulations - hiyo issue ya paypal na system nyingine kupigwa pini Tanzania nia kwasababu ya ile sheria yetu kandamizi ya anti money laundering ndo imeweka kofuli kwenye miamala inayotoka nje
 

nakataa sio lugha.
mbona kuna kampuni zimeenda nchi ambazo lugha zipo zaidi ya 8 zinatumika.
tatizo ni serikali kuwa itabiriki na siasa zake .mfano wa magufuli tu unaweza kuleta muwekezaji ambaye afahamu kesho kuna kichaa gani
 
Regulations za Kenya pia ziko friendly especially kwenye miamala ya kuingia na kutoka nje.

Tanzania kuna ile sheria ya anti money laundering ilisainiwa na Prof. Mpango, yaani ni mwiba mkali kwenye miamala inayoingia nchini
Hii nchi yetu kua tajiri ni kosa. Regulations za kimasikini, zinatungwa na watu wenye akili za kimasikini, ili kuhakikisha tunabaki kua masikini.

Mlolongo wa kupokea dola elf kumi tu kutoka nje ya nchi, unatosha kukufanya ujutie kua mtanzania!
 
Ni kweli mkuu, hata 'investment security'....usalama wa mali au miundombinu ya uwekezaji Kenya wamejitahidi mno nadhani wana uelewa mkubwa mno wa dunia ya utandawazi unavyofanya kazi kuliko watunga sera wetu...........hapa Tanzania lolote kwa muda wowote linaweza kutokea kuathiri mali za wawekezaji.
 
Kinachotukwamisha Tanzania kinaanzia kwenye sera
 
Wazee wetu wako too outdated and too rigid in the world which needs the highest level of flexibility.

Mbaya zaidi, ndio wanaoamua kila kitu!
 
Yes, yaani i wish tungekuwa tunafanya utafiti issue kubwa ni kwamba lugha inawapa wakenya kujiamini na kwenda kusaka fursa nje ya nchi
Kiswahili hakina faida zaidi ya ufahari

Wakenya waliachana na Ujamaa ndo maana Saudi kuna wakenya zaidi ya 50,000
Wameamua jilipua

Ukienda Sudan utawakuta wakenya wengi sana

English ni lugha ya dunia, leo hii Wachina wanajifunza Kiingeleza, wamebadili hadi vyuo vingine vinaanza fundisha kwa kiingeleza lengo ni kufanya biashara
 
Some tyme unaweza ukajiumiza akili kuwaza kwann tunabaki nyuma ya kenya au blahblah.

Lakini tusijue malengo ya viongozi wetu mm nahisi hawapo kucompete na kenya zaidi wapo kuifanya Tanzania iwe kama Tanzania and not kenya.

Last month Kuna kiongozi mmoja mkubwa wa wizara level ya kutoa maamuzi nilikuwa nadiscuss nae kuhusu mambo afya basi nikamwambia unaona private huduma zao ni bora kuliko serikali akanikatisha na kusema serikali haipo kwaajili ya kucompete ila private ndio wanatakiwa kuiga serikali maana serikali ndio mkubwa...Nilichoka!
 
Regulations mbovu na zinazobadilika kila siku ni hoja ya msingi ila Remittances ni utumwa tu na kutafanya watu weusi Africa kuwa ni duni na tegemezi wa wazungu.
 
Hii kauli ya Museveni kwa waganda ipo related kabisa na watanzania.

Even fools survive in Tanzania, But in other parts of the world they can die....
 
Regulations mbovu na zinazobadilika kila siku ni hoja ya msingi ila Remittances ni utumwa tu na kutafanya watu weusi Africa kuwa ni duni na tegemezi wa wazungu.
Hapa ni lugha tu tofauti imetumiwa. Serikali wakifanya wao inaitwa mikopo na misaada isiyo na masharti (loans and grants), wananchi wa kawaida inaitwa remittances. Hakuna hata mmoja aliyeweza kujitegemea kwa asilimia 100. Wote ni tegemezi tu.
 
Ungemnasa kibao

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 

Policy zetu zinatufanya tuwe stuck in the mud. World is moving fast and we cant catch up
 
Yaani unafungua thread kabisa kuongelea $5m ya mtu wakati mafisadi kila siku yanapora mabilioni ya miradi tumekaa kimya🏃🏃🏃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…