Data driven decisions. Kwanini NALA wawe na HQ Kenya na sio Tanzania?

Data driven decisions. Kwanini NALA wawe na HQ Kenya na sio Tanzania?

Mkuu Tanzania ina mambo ya ajabu mkuu sana.
Kuna regulations sijui hata zinalisaidia nini taifa hili.
Mimi tu kila mwezi nikipokea ela less ni $500 kutoka nje na zote kwasababu Tanzania wana regulation zao za ajabu inabidi nizipitishe kenya. So flow iko hivi either paypal withdraw ni safaricom au skrill withdraw ni safaricom then safaricom to airtel money. Hapo anayehesabika kapokea hiyo pesa ni mkenya.
Na kuna zaidi ya watu hata 500 wanaotumia formula kama yangu hata humu wapo wengi.
Ukiwauliza paypal au upwork au skrill, jibh ni sheria za pesa Tanzania ndizo zinafanya mambo yawe hivyo.
Hili pia linafanya kuuza hata bidhaa kwenye platoforms za kimataifa kwa wajasi wadogo kuwa na changamoto. Wazungu wengi wanaiamini paypal linapokuja suala la malipo mtandaoni ila ndio tz paypal haipokei pesa.
Nchi ina mambo mengi ya ajabu na sijui wanafaidika nini kwa haya.
magufuli aliiharibu sana hii nchi
 
Regulations mbovu na zinazobadilika kila siku ni hoja ya msingi ila Remittances ni utumwa tu na kutafanya watu weusi Africa kuwa ni duni na tegemezi wa wazungu.
Utumwa kivipi?... yaani itokee fursa ya kufanya kazi nje ya nchi halafu ukatae, uendelee kuwa jobless huku bongo? Kisa kwamba ukienda US itachukuliwa kama ni utumwa???

Hapana mkuu, sikuungi mkono kabisaaa
 
Diaspora watanzania ni wachache mnoo na hii ya uraia pacha kutokukubalika ndio inafanya Mambo yawe magumu..

Kiasili watz sio aggressive kabisa maana linchi letu tu lenyewe lina fursa kila kona plus ujamaa wetu, mtu hata kama huna kipato cha uhakika Ila utakula na kulala hata kwa mashangazi

Hiyo akili ya kuhustle nje ya nchi unaipata wapi

Na sio kwamba nawasagia watu kunguni maana hata Mimi sio aggressive
True brother.... hatuko aggressive lakini pia inatokana na kutokujiamini. Na kutokujiamini hiyo inasababishwa na elimu finyu na kitokumudu lugha
 
Wazee wetu wako too outdated and too rigid in the world which needs the highest level of flexibility.

Mbaya zaidi, ndio wanaoamua kila kitu!
Nalubaliana.... hawa wazee wapo old school sanaaa... tena sanaaaa.. kisa tu wana Phd ila wana ushamba mwingi
 
Policy zetu zinatufanya tuwe stuck in the mud. World is moving fast and we cant catch up
Policy makers wenyewe ni old school... hilo nalo tatizo.

Unakuwa na mzee Prof amesoma miaka ya 80 huko, ukimuambia sijui paypal, skrill, crypto, anaona kama ni mashikolo mageni, anaamua kuyapiga pini, maana hayaelewi, anahisi labda ni kitisho fulani hivi, kumbe ni yeye tu haelewi.

Tatizo hilo
 
Ndio maana wabongo ukiwashinda hoja wanaanza kukuita wewe mkenya unajifanya unajua kilakitu...
 
Kiswahili has nothing to do with remittances.

Hatuna uraia pacha. Hatuna mwamko wa kwenda nje, hapo awali hakukua na sababu za msingi kwenda nje ya nchi plus ugumu wa kwenda nje kama kupata passport, hivyo Diaspora wa TZ ni wachache compared to wakenya.

Mazingira ya uwekezaji bongo bado sio rafiki.

Kenya remittances zimeongezeka maradufu mara baada ya kuruhusu uraia pacha. Bongo iige hili.
 
Kiswahili hakina faida zaidi ya ufahari

Wakenya waliachana na Ujamaa ndo maana Saudi kuna wakenya zaidi ya 50,000
Wameamua jilipua

Ukienda Sudan utawakuta wakenya wengi sana

English ni lugha ya dunia, leo hii Wachina wanajifunza Kiingeleza, wamebadili hadi vyuo vingine vinaanza fundisha kwa kiingeleza lengo ni kufanya biashara

Kenya hawakuachana na Ujamaa bali hawajawahi kuwa wajamaa kabisa.

Wakenya walianza kutoka zamani nje ya nchi sababu they had no other option. They had to. Social-political climate yao haikua rafiki. Kadhalika nchi zingine kama Nigeria nk. Sio sababu ya English tu au kwa kupenda kwao.

Umewahi kuwaona Namibians au waBotswana nje ya nchi zao permanently hata wakati nchi zao zinapitia wakati mgumu? Kwanini? Unadhani hawajui ngeli?
 
Kiswahili has nothing to do with remittances.

Hatuna uraia pacha. Hatuna mwamko wa kwenda nje, hapo awali hakukua na sababu za msingi kwenda nje ya nchi plus ugumu wa kwenda nje kama kupata passport, hivyo Diaspora wa TZ ni wachache compared to wakenya.

Mazingira ya uwekezaji bongo bado sio rafiki.

Kenya remittances zimeongezeka maradufu mara baada ya kuruhusu uraia pacha. Bongo iige hili.
Nothing to do with remittance?.... yaani utaenda nchi za ulaya na marekani na hujui kugha???
 
Nothing to do with remittance?.... yaani utaenda nchi za ulaya na marekani na hujui kugha???

Wamalawi hadi mmachinga anaongea kingereza kizuri tu japo kwa accent yao, nao wametuzidi remittances? Kwanini hawatoki nchini mwao?

Kuna more factors za watu kuzamia nje than just English.

Kukosekana kwa uraia pacha na mazingira mabovu ya biashara ndo maana watu hawatumi pesa za maana bongo.

Kenya remittances zime-triple mara baada ya kuruhusu uraia pacha.
 
Hahaa, mchakato wa kupata passport Tanzania, unaweza kuhisi labda unataka kununua figo!
 
Wamalawi hadi mmachinga anaongea kingereza kizuri tu japo kwa accent yao, nao wametuzidi remittances? Kwanini hawatoki nchini mwao?

Kuna more factors za watu kuzamia nje than just English.

Kukosekana kwa uraia pacha na mazingira mabovu ya biashara ndo maana watu hawatumi pesa za maana bongo.

Kenya remittances zime-triple mara baada ya kuruhusu uraia pacha.
According to data, sisi remittance kwa mwaka jana wao walikuwa USD 260 Million sisi tulikuwa USD 570 Million.

Ila Malawi population yao ni 20 million na Tanzania tupo 61 million.

Ukizichanga vizuri akili zako utagundua hata Malawi wanatuzidi remittance on relative terms.
 
Back
Top Bottom