BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Kuanzia November 16; taarifa za watumiaji hao zimevuja na zinauzwa mtandaoni. Taarifa hizi zikiwemo namba za simu, majina (kwa wanaoweka majina yao kwenye akaunti zao) na profile picture zimekusanywa na kuuzwa kwenye Dark Markets.
Hakuna chats zilizovuja; data zinazouzwa ni namba za simu za watu: ambapo wanunuzi wanaweza kutumia katika kutuma spams na scams.
Taarifa za watumiaji wa nchi takribani 84 zipo wazi;
🔘 watumiaji Milioni 32 ni wa Marekani,
🔘 Millioni 11 wanatoka Uingereza, na
🔘 Egypt - taarifa za watumiaji Milioni 45
🔘 Italy - taarifa za watumiaji Milioni 35
🔘 Saudi Arabia - taarifa za watumiaji Milioni 29
🔘 Ufaransa - taarifa za watumiaji Milioni 20
🔘 Turkey - taarifa za watumiaji Milioni 20
🔘 na Urusi taarifa za watumiaji Milioni 10.
🔘 na wengine ni nchi nyingine zilizobaki
Bei za data zinatofautiana na nchi, kwa wastani data za Marekani zinauzwa kwa dola 7,000 na data za watumiaji wa Uingereza zinauzwa kwa kuanzia Dola 2,500.
Mtandao wa Cybernews, TechRadar Pro na analyst wa kiusalama wanasema data hizo asilimia kubwa ni za watumiaji wa WhatsApp GB na WhatsApp nyingine ambazo sio Official. Meta imegoma kuelezea kinachoendelea lakini lawama kubwa imeonekana kwenye app feki ambazo sio official.
Taarifa hii mpya ambayo imeanza kusambaa, inaonyesha madhara makubwa ya kutumia app ambazo sio official.
Lakini inawezekana ni watu tu wanatishia watu. 🤷🏽♂️
Credit: Swahili.Tek