Wakuu mimi siamini kuwa Balali amekufa, kwa sababu:-
1. kwa wale msiojua ni kwamba katika mji wa State ya Boston, habari za wagonjwa kulazwa hospitali na wagonjwa kufariki wakiwa kwenye hospitali za State hiyo ni open to the public, yaani unaweza kwa kupitia internent kupata info za mgonjwa yoyote aliyelazwa au kufariki huko Boston,
2. Boston, ina wakazi wengi sana wa kutoka bongo, ambao pia wengine wamebobea kwenye sekta ya Medicine kwenye hospital za huko na tunawafahamu kwa karibu, sasa haiwezekani kuwa wote hawajui kwamba Balali aliwahi kulazwa hospitali gani huko!
3. Haiwezekani Balali ambaye mpaka magazeti ya Boston, kama Globe ambayo yanajua kuwa huyu ni mtu of special interest kwa taifa letu na kwa waa-Afrika wengi wanaoishi Boston, afariki dunia wao wasijue kabisaa, lakini gazeti la Tanzania Daima, likajua that is a big joke!
4. Mke wa sasa Balali, ni dada wa mume wa dada wa mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima, ambalo ndilo limekuwa la kwanza kusema hizi habari, now kweli this is just your usual another death annoucemment, au?
5. Ni kwa nini wa-Tanzania kwa maelfu wanaoshi Boston, hawajui Balali alipokuwa amelazwa au hata habari za msiba? Angalau hata the big star Hashimu, the basketballer angekuwa amejulishwa na wazungu somehow kuwa kuna mbongo mwenzio hospital amelazwa au amekufa, lakini hata yeye hajui na ni mwenyeji huko Boston!
Sasa kulikoni na hii habari? Naiona haijakaa sawa hii!