Daudi Ballali's Death

Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
I AM BEGINING TO THINK he was a fool kukubali kuja kufanya kazi Tanzania, kama angebaki kulekule US huenda mauti yasingemkuta mapema namna hii.
 
Afariki Ijumaa, mpaka Jumanne hata nyumbani kwake hakuna hata dalili ya msiba? Mimi jamani siamini hili, hapa tunadanganywa.

Jiandaeni kutoa rambirambi kwenye gogo.

Huyu mkewe ana nguvu ya kutoa taarifa Ikulu na BOT lakini hakuna taarifa hata kwa familia yake Iringa.

Jamani nisaidieni, ni mimi tu ambaye naona kuna jmambo sio sawa?

Mkuu ES, mimi nakubaliana na data zako.


Mkuu, hii ndio inaitwa bongo. Maisha ujanjaujanja. Cha msingi watu waliopo Boston wasikose msiba. isitoshe ni wazi kwamba MKJJ anayajui mengi juu ya msiba huu wa kiaiana kuliko ikulu. Kwanza ikulu na BoT tayari wameshamkana!
 
huh!? Sasa matanga ya msiba huu yamewekwa wapi? au katika utamaduni wa akina Ballali hawaweki matanga? 😕

Nyumbani kwa Ballali mtaa wa Mahandu kitalu namba 347 Masaki, Dar es Salaam hakukuwa na dalili zozote za msiba. Gazeti hili lilifika nyumbani hapo na kumkuta kijana aliyejitambulisha kwa jina la Hassan, akieleza kuwa hajui chochote juu ya kifo cha bosi wake.

"Mimi kwa kweli sijui lolote, ni vyema mwende kule alikokuwa anafanyia kazi wanaweza kuwa na taarifa rasmi," alisema Hassan na kuongeza kuwa yupo peke yake na mlinzi na hakukuwa na mtu mwingine ndani.
 
I AM BEGINING TO THINK he was a fool kukubali kuja kufanya kazi Tanzania, kama angebaki kulekule US huenda mauti yasingemkuta mapema namna hii.

He was fool to compromise his principles. He should have stood firm. Instead, he accepted to be used and they ended up dumping him while they continue sipping what he helped them to reap ungraciously!
 
Tena hamna hata dalili ya msiba nyumbani na kijijini...wewe umeona kifo gani cha mtanzania yoyote hamna dalili za msiba? Hata iwe kabila gani...TUMEDANGANYWA.
 
Afariki Ijumaa, mpaka Jumanne hata nyumbani kwake hakuna hata dalili ya msiba? Mimi jamani siamini hili, hapa tunadanganywa.

Jiandaeni kutoa rambirambi kwenye gogo.

Huyu mkewe ana nguvu ya kutoa taarifa Ikulu na BOT lakini hakuna taarifa hata kwa familia yake Iringa.

Jamani nisaidieni, ni mimi tu ambaye naona kuna mambo sio sawa?

Mkuu ES, mimi nakubaliana na data zako, hapa tunadanganywa.

Mkewe pia anahusika katika ufisadi uliofanywa pale BoT. Hivyo 'kumuua" mumewe kwake haitakuwa shida ali mradi tu anajua ushahidi ambao angeutoa labda umgemuathiri huyo mama Anna Muganda hivyo 'kufa' kwa jamaa kunamuongezea imani landa anaweza kuponea chupu chupu kuingia lupango, maana katika mabilioni yaliyochotwa naye pia alinufaika. Huyu jama alikuwa mginjwa mahututi, je hospitali gani iliyoruhusu 'mgonjwa mahututi' atoke hospitali ili kafie nyumbani kwake Boston? Je, alitoka lini hospitali? alitoka kwa idhini ya madaktari? Je, tunaweza kupata majina ya hao madaktari walioruhusu Ballali kwenda 'kufia' nyumbani. Utata unazidi kuongezeka.
 
Mlioko Boston,Connecticut,Maryland , tafuteni County records za Death certificate...maana hata mbwa akifa marekani wana document.
 
Utaratibu wa ufanyajikazi kwetu ni mgumu mno!!!,Siku nzima ya jana baadhi ya watu walikuwa wanajaribu kufuatilia habari hii ya kifo cha Balali kwa ukaribu,lakini watu wa Ubalozi wetu DC walionekana wanasita kutoa habari wanayoifahamu,na kuelekeza watu waulize Ikulu kwa uthibitisho wa hilo,Kwa bahati nzuri watu wa Ikulu walipatikana kwa simu,na walidai kuwa Msemaji wa Ikulu hakuwepo Ofisini alikuwa busy kuandaa safari ya Mkuu kwenda Japan.

Mkuu huyo alipopatikana alidai kuwa "wanaowajibika kujua habari za Dr.Balali ni BOT kwa sababu Balali si muajiriwa wa serikali",au kama unahitaji lolote zaidi wasiliana na Jamaa za Balali huko US.

Baadaye Ndugu wa Mke wa Balali waliopo California na Boston walipatikana na kwa kifupi wakathibitisha habari hiyo kwa kifupi,na kwa maelezo yao,Sala(Swala) na Mazishi yatakuwa Ijumaa kwa watu wa karibu wa Marehemu.Kwa maana hiyo Ni KWELI Waungwana Kwamba Dr. Balali hatunae tena...Huko BOT Dar msiba huu umekwishatangazwa rasmi.

Cha kujiuliza hapa,ni kwa nini serikali haitaki kusema lolote kuhusu msiba huu mkubwa,ilhali ilituma baadhi ya watu kuja kufuatilia uwepo wa Dr hapa USA.Inaogopesha sana....
 
Mkuu,

Je mtu akifa inakuwaje? Hapa issue sio kuumwa na badala yake ni kifo, je sheria inasemaje?

Kama info inaweza kupatikana, basi tusaidie kututafutia hapo, tujue kama tumefungwa magoli na tujiandae kuzika gogo.

Msee,
kiufupi tu ni kuwa habari za Balali zipo well controlled, utadhani watu wamelishwa yamini ya kuficha hizi "siri"!!! kujibu swali lako ni kuwa Familia inaweza kuomba habari zake zisiwe public, na serikali ikafanya hivyo kama famili ilivyotaka!!!...........ni kama vile ndoa, ukikaa kimya unaweza kukutaja harusi yako gazetini(hasa ktk small towns) ukiomba iwe siri, yes inakuwa siri!!! SIMPO like that.

jana nilikuwa kwenye tail ya Sumaye kiana, lakini kumbe nilikuwa nimechelewa kwani jana hiyo ndio alikuwa anatinga Bongo kutokea hapa Boston!!! angekuwepo, wallahi ningepata nyeti!!
 
Sasa Matanga yatawekwa haraka haraka ili kutuzuga, lakini uwongo wao tumeshautengua. Kifo kitokee tangu Ijumaa, mama yake mzazi asiambiwe lakini wakaambiwe Ikulu na BoT!! Nyumbani kwa marehemu hakuna matanga hadi hii leo J'tano! Njooni na usanii mwingine, huu umeshavuja!
 
Ambacho nilikuwa sijui hivi kumbe hakuwa tena mfanyakazi wa serikali? Hii nilikuwa sijui kabisa. Mimi nilifikiri kuwa ameondolewa nafasi ya ugavana hila anabaki serikalini.
 
usanii unaendelea hapa

Kweli Balali kafariki!

2008-05-21 17:48:18
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, BOT, Dokta Daud Balali amefariki dunia. Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vyake nchini na huko Marekani, zimethibitisha kuwa Dk. Balali alifariki dunia Ijumaa iliyopita.

Vyanzo hivyo vimedai kuwa Dk. Balali alifariki baada ya mashine iliyokuwa ikimsaidia kupumua kuondolewa.

Aidha, vyanzo hivyo vimedai kuwa kabla ya kifo chake, Dk. Balali aliandaa ujumbe mzito, ambao ndani yake umeanika ukweli wote kuhusiana na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikielekezwa kwake, ikiwa ni pamoja na zile zinazohusiana na kashfa ya upotevu wa mabilioni ya pesa za nchi kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje, EPA.

Alasiri imeambiwa na vyanzo hivyo kuwa Dk. Balali alimkabidhi ujumbe huo wenye siri zote ndugu yake mmoja anayemuamini na kumpa maelekezo ya namna ya kuufikisha kunakohusika na hatimaye Watanzania kujua ukweli wa suala zima.

Hata hivyo, chanzo hicho kimedai kuwa hadi sasa haijafahamika ni ndugu yupi ameachiwa ujumbe huo.

Imedaiwa zaidi na chanzo hicho kuwa Dk. Balali aliamua kuandaa ujumbe huo wenye siri zote kwa vile hakutaka achafuliwe peke yake wakati wahusika wa sakata hilo wapo na anawafahamu.

Aidha, imedaiwa alikuwa akisema kuwa hakutaka aondoke na siri nzito kuhusiana na yote aliyokuwa akielekezewa kidole.

Dk. Balali alifukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete baada ya uchunguzi uliofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya Ernst &Young kubaini upotevu wa Shilingi Bilioni 133 zilikuwa zimechotwa BOT kupitia EPA wakati wa uongozi wake.

Dk. Balali alienguliwa nafasi ya ugavana na Rais wakati akiwa nje ya nchi kwa matibabu na tangu wakati huo, hakuwahi kurejea nchini mpaka umauti ulipomkuta.

Habari zinadai kuwa Dk. Balali anatarajiwa kuzikwa keshokutwa huko Jijini Washington DC, Marekani.


SOURCE: Alasiri
 
mara kafariki nyumbani kwake Boston, mara kafariki hospitali baada ya mashine iliyokuwa inamsadidia kupumua kuondolewa. Je, ni kwanini iliondolewa? Nani aliyetoa idhini ya mashine hiyo kuondolewa? Mkewe Anna Muganda, Ikulu, madaktari wake? 😕

Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, BOT, Dokta Daud Balali amefariki dunia. Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vyake nchini na huko Marekani, zimethibitisha kuwa Dk. Balali alifariki dunia Ijumaa iliyopita.

Vyanzo hivyo vimedai kuwa Dk. Balali alifariki baada ya mashine iliyokuwa ikimsaidia kupumua kuondolewa.
 
Afariki Ijumaa, mpaka Jumanne hata nyumbani kwake hakuna hata dalili ya msiba? Mimi jamani siamini hili, hapa tunadanganywa.

Jiandaeni kutoa rambirambi kwenye gogo.

Huyu mkewe ana nguvu ya kutoa taarifa Ikulu na BOT lakini hakuna taarifa hata kwa familia yake Iringa.

Jamani nisaidieni, ni mimi tu ambaye naona kuna mambo sio sawa?

Mkuu ES, mimi nakubaliana na data zako, hapa tunadanganywa.


jamani jamni mimi toka mwanzo nilisema BALALI HAJAFA, Anna uganda ni msanii tuu, kumbukeni naye yumo kwenye list, anawavuruga tu vichwa ili mumsahau mumuwe jamani watz tuamke jamani.......
 
Thanks invinsible.
Sisi tulioko mbali, tunasikia kuwa gazeti la alasiri limeandika kuwa Balali alikufa ijumaa na atazikwa Marekani.
Kama ni hivyo, hii si janja ya CCM na Mafisadi. Pengine ameshafanyiwa plastic surgery na sasa wanazika gogo tu! Ama kweli hii ndiyo 'scientific msukule' au 'ndondocha ya kisiasa'
Tujipe pole watz kwa kubambikiwa hilo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom