Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, Daud Nyalamu amesema kutokana na utekelezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo wilayani humo, wao hawana deni kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, bali wanamhisi anawadai wao na wamejipanga kuhakikisha wanatiki mwezi Oktoba
Akizungumza leo katika mahojiano na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV, Nyalamu amesema
“Mama, sisi Halmashauri ya Wilaya ya Itilima hatumdai, bali sisi ndo anatudai. Tunamhakikishia Mama mwezi wa kumi tunatiki, na asiwe na wasiwasi kwa sababu miradi mingi ya kimkakati na ya maendeleo ambayo wananchi walikuwa wakihitaji, kwakweli ametekeleza”
Akitaja mafanikio hayo, Nyalamu amesema miradi mikubwa iliyotekelezwa ni pamoja na Ujenzi wa shule mpya tatu za sekondari, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, Ongezeko la huduma ya maji kutoka asilimia 30 hadi asilimia 87
Amesisitiza kuwa maendeleo hayo yameleta mabadiliko chnya kwa wananchi wa Itilima, na kwamba hali hiyo imejenga imani kubwa kwa serikali ya awamu ya sita
Source: CLOUDS TV