Msaidizi binafsi wa Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Tundu Lissu, David Djumbe, amefunguka kuhusu mazingira yaliyomfanya akimbie nchini Tanzania baada ya kupokea taarifa za siri kutoka ndani ya mfumo zilizomwonya kuwa alikuwa hatarini kutekwa na kuuawa ndani ya siku tatu.
Akizungumza katika mahojiano na Mwanzo TV Plus yaliyorushwa Agosti 7, 2026, Djumbe amesema watekaji hao walikuwa wakimsaka kwa lengo la kupata taarifa binafsi zinazomhusu Lissu na hivyo waliamini David kuwa na taarifa nyingi za Tundu Lissu
Ameeleza kuwa Novemba 27, 2025, alipigiwa simu na mtu ambaye yuko kwenye mfumo akimtaka akimbie haraka kuokoa maisha yake. Siku hiyo hiyo majira ya saa nane usiku, watu wasiojulikana wakiwa na gari jeupe walivamia nyumba yake, lakini walikimbia baada ya king'ora cha usalama (alarm) kulia.
Asubuhi iliyofuata ya tarehe 28 Novemba, Djumbe alilazimika kumwondoa mke wake na watoto na kwenda nao nje ya mji kwa ajili ya kuwaweka sawa kisikolojia na kuwaaga kabla ya kuanza safari ya kukimbia nchi.
Akiwa bado yuko nje ya mji, alipokea ujumbe kutoka kwa kijana anayeishi naye nyumbani akimfahamisha kuwa watu wenye silaha waliovalia nguo za uraia na kujitambulisha kama polisi walikuwa wameingia nyumbani kwake wakimtafuta.
Baadaye, mke wake aliporudi nyumbani hapo alikuta watu hao wameizingira nyumba. Walipomhoji kuhusu alipo mume wake, aliwaeleza kuwa amesafiri, lakini watu hao wakadai kuwa wao ni polisi kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay na walikuwa wakimhitaji Djumbe kwa mahojiano.