Wakati 'Tume Huru ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea Nchini Oktoba 29.2025 na siku zilizofuata' ikiendelea na majukumu yake, na wakati huu ambao inatajwa kwamba baadhi ya wawakilishi wa taasisi za kimataifa wamefika au wanatarajiwa kufika nchini kwaajili ya kuangaza matukio hayo, imeelezwa kuwa Tanzania haiwezi kushtakiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutokana na matukio ya Oktoba 29.2025 na siku zilizofuata
Imeelezwa kuwa ICC haiwezi kuanza kuwachukulia hatua viongozi wa Taifa lolote bila kufuata utaratibu, ambapo jambo la kwanza linalotazamwa ni endapo nchi husika haiko tayari kushughulikia jambo hilo au kama itaamua kushughulikia kuonekane uwepo wa dalili za upendeleo, jambo ambalo inaweza kuwa tofauti kwa Tanzania kutokana na Tume iliyoundwa, sambamba na kauli ya serikali kuwa inasubiri ripoti ya Time hiyo ili iweze kuchukua hatua
Hayo yamefafaniliwa na David Evance Komba ambaye ni Mbobevu wa Sheria za Kivita (International Humanitarian Law -IHL) alipokuwa akihojiwa na Jambo TV kupitia kipindi cha 'Jambo Asubuhi' leo, Jumatano Machi 11.2026.
Ili uweze kumshtaki Rais SSH lazima uweze kuthibitisha pasipo shaka uwepo wa mpango wa awali wa mauaji hayo. Lazima uweze kuweka wazi namna mpango mzima ulivyopangwa mpaka mauaji yakafanyika.Wakati 'Tume Huru ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea Nchini Oktoba 29.2025 na siku zilizofuata' ikiendelea na majukumu yake, na wakati huu ambao inatajwa kwamba baadhi ya wawakilishi wa taasisi za kimataifa wamefika au wanatarajiwa kufika nchini kwaajili ya kuangaza matukio hayo, imeelezwa kuwa Tanzania haiwezi kushtakiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutokana na matukio ya Oktoba 29.2025 na siku zilizofuata
Imeelezwa kuwa ICC haiwezi kuanza kuwachukulia hatua viongozi wa Taifa lolote bila kufuata utaratibu, ambapo jambo la kwanza linalotazamwa ni endapo nchi husika haiko tayari kushughulikia jambo hilo au kama itaamua kushughulikia kuonekane uwepo wa dalili za upendeleo, jambo ambalo inaweza kuwa tofauti kwa Tanzania kutokana na Tume iliyoundwa, sambamba na kauli ya serikali kuwa inasubiri ripoti ya Time hiyo ili iweze kuchukua hatua
Hayo yamefafaniliwa na David Evance Komba ambaye ni Mbobevu wa Sheria za Kivita (International Humanitarian Law -IHL) alipokuwa akihojiwa na Jambo TV kupitia kipindi cha 'Jambo Asubuhi' leo, Jumatano Machi 11.2026.
Hakuna kesi atakayopewa Samia, Lissu na Heche kwa zile kauli zao kabla ya uchaguzi mkuu wanaweza kutiwa hatiani watakapokuja ICC.Hakuna mtu anashitaki nchi anashitakiwa ni raisi fake Samia
Hapa kwetu kuna pande ngapi?Yuko sahihi kabisa. Mamlaka ya ndani kama ipo na ina uwezo wa kushughulikia ICC haiwezi kuingilia, 2008 Kenya kulikuwa na pande mbili ambazo zilikuwa zinashutumiana na wote walikuwa serikalini ndiyo maana Ocampo akalazimika kuingilia