Mtanzania Tajiri
JF-Expert Member
- Aug 31, 2024
- 341
- 319
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPPC), David Kafulila, amesema tangu serikali ya Tanzania ifanye marekesho ya sheria na miongozo yake mbalimbali sasa kiwango cha wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania kimeongezeka.
Kafulila ameyasema hayo wakati akihitimisha siku ya kwanza ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaohusu Nishati unaofanyika kwa siku mbili nchi Tanzania kuanzia Januari 27 na 28, 2025 katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwl Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Aidha Kafulila ameongeza kuwa, serikali ya Tanzania itaendelea kufanya marekebisho ya sheria na miongozo ambayo bado inaleta changamoto kwa wawekezaji na hatimaye kutimiza ajenda M300 ya kuwafikishia nishati ya umeme waafrika milioni 300 ifikapo mwaka 2030.
Mhe Kafulila amesema ni lazima sekta binafsi Africa yote zihusishwe katika mchakato huo kwa sababu ndio wadau wakubwa wa maendeleo ulimwenguni kote.
Ameongeza kuwa ajenda hiyo haipaswi kuwa ya mipango pekee bali iwe ya kiutendaji zaidi na hatimaye iweze kuleta manufaa barani Afrika kwa waafrica.
Ukiacha Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kuhutubia mkutano huo wa M300 wengine ni Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko, Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba na Mhe David Kafulila Mkurugenzi wa kituo cha Ubia nchini PPPC.