A VERY INTELLIGENT AND SIGNIFICANT SPEECH ON ASSORTED SOCIETAL ISSUES BY LATE MZEE MKAPA
Hiyo khotoba ina mengi ambayo yanaakili, mantiki na ufasaha wa muktadha wa uono na uchambuzi wake.
Labda mbali kuzidi wazungumzaji wengi--wazungumzaji katika majukwaa ya aina zile za makutano ya mafungamano ya (1) Washirika wa Maendeleo na (2) Wanajamii wanaobadilishana mashauri juu ya kadhia zao za 'Kimaendeleo ya Vitu/Upungufu wa Pesa za Kuendesha Miradi/Uhitaji'.
Dakika ya kumi (dk 10 - dk 15) ya hiyo media,
video, mzee Mkapa anazungumza jambo lenyewe khasa kuhusiana na dhamira na azma ya 'Maendeleo Endelevu' na mikingamano ijayo na urazini wenye kukosa fasaha ya ukweli khasa wa mambo; mambo ya uono wa juu juu wa mambo na kutengenezea mashauri mushkeli juu ya jitihada, mifumo na utendaji...
Mzee Mkapa, anatumia Uono na Ufikirifu Mifumo katika mashauri yake na uandishi wake wa Khotuba... Ni nadra sana kwa viongozi wengi katika jamii yetu kuwa mahiri katika Uono na Ufikififu mifumo; huu
huja na uzoefu na busara binafsi ya mtu katika ku-JUA mambo ilivyobora. Hii ndiyo inafanya Mzee Mkapa anaonekana ni mbora katika khotuba zake kwa kuwa 'Zina Akili Khasa'--namna ya hizo kuweza kuwa na 'Mbegu za u-JUA-ji' na siyo tu 'hoja shindanishi' ama vipi...
Kwa hivyo Mzee Mkapa, siku alipozungumza kwenye huo mualiko katika shule ya Siasa ya John F Kennedy, Septemba 15, 1999, alitoa khotuba iliyotayarishwa vizuri kwa mapana na marefu ya mbegu za u-JUA-ji na tena kwa mashauri yanayowasilishwa kwa haiba ya Uono na Ufikirifu Mifumo....
Kwa hivyo, yeye katika dakika ya kumi, kuzungumza kuhusu Azimio la Copenhagen,
Copenhagen Social Development Summit, kama kitovu cha 'Shauri Uono' kulandanishia 'Uono Mifumo' na basi kukazia Udhamirifu unaokwenda juu wa Upeo na Hadhi wa nia/matendo jamii ulio na
misingi ya Ukuu Kiroho, Maadili na Miiko... Halafu anachukua muktadha mushkeli wa tafsiri za mambo, "stereotyping"--mambo ya kubatizana majina na kasumba, kukontrasti mashauri yenye kuzingatia '
Utata' wa uono bora kwa mambo yanayopimika na mambo yasiyopimika kwa vigezo vya '
fedha za misaada'...
Mkutano wa Nishati Afrika M300, kiuono na ufikirifu mifumo,
mashauri yake mengi yaliyoibuka yamekuwa ni yenye kutabirika kwa mtu yeyote mwenye uono na ufikirifu mifumo. Majukwaa haya, kiufundi, ni
utundu wa kujenga ushawishi kwa muelekeo fulani wa mambo unaoweza kuwa umeshapangwa waziwazi ama isivyo waziwazi. Hili ndilo linaweza
kutoa viashirifu vya tathmini ya viongozi/uongozi na watendaji/utendaji wanaojifahamu ama wanaoicheza Sikinde ngoma ya Ukae...
Hmmm