David Kafulila: Ajabu ni ipi Tanzania yenye ziada ya umeme kununua umeme?

David Kafulila: Ajabu ni ipi Tanzania yenye ziada ya umeme kununua umeme?

YAY

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
362
Reaction score
381
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila hivi ndivyo alivyoandika baada ya baadhi ya Watanzania kushangaa kauli ya Rais Samia Suluhu kuhusu Tanzània kununua Umeme nje ya nchi, Ethiopia.

Mkurugenzi Kafulila anasema pamoja na kwamba nchi kubwa na tajiri duniani kama Marekani ( USA ), Ujerumani, Norway, Sweden au Australia wanaumeme mwingi kiasi Cha kuuza nje ya nchi zao bado na wao kwa Upande mwingine wa nchi zao wananunua umeme kutoka nje ya nchi zao.

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Kafulila anasema kuwa baadhi ya maeneo ya nchi yetu hasa maeneo ya mipakani gharama ya kuzalisha, kusafirisha na kufikisha umeme maeneo hayo ni kubwa pengine kuliko gharama ya kuuvuta na kuununua umeme toka nchi za jirani.

IMG-20250311-WA0000.jpg
 
Ulifika sababu ethiopia alikuwa anampelekea umeme mteja wake anaempa mahela.

Ethiopia kafikisha umeme namanga sababu anauuza nchi nyingii..

Hajaupeleka kwa ajili ya kuhudumia mkoa mmoj
Tanzania itaweza kuuza umeme nje?
Kila pembezoni mwa mikoa kanunua nje, yeye atamuuzia nani?

Ajabu ninkua umeme wa nje mfn uganda haukatikagi ila maumeme ya tanzania kila mwezi mgao

Ujinga mtupu
 
Tanzania itaweza kuuza umeme nje?
Kila pembezoni mwa mikoa kanunua nje, yeye atamuuzia nani?

Ajabu ninkua umeme wa nje mfn uganda haukatikagi ila maumeme ya tanzania kila mwezi mgao

Ujinga mtupu

Hapana sio kila pembezoni.. njia ya zambia mbeya.. Tanzania inakamilishwa. Hivyo Tanzania atamuuzia Zambia

Pia zanzibar na yeye anauziwa na Tanesco.
 
Kafulila yupo sahihi.. ni ujinga kusafirisha umeme kutoka rufiji mpaka kagera. Maelfu ya kilometa.

Huku ukiwa kagera unaweza kununua umeme uganda ukafika kagera kwa urahisi maana pafupi sana
Yupo sahihi Kabisa
 
Nilikuwa natazama TBC, nikawa nafatilia Maoni na hoja za engenier mmoja aliyekuwepo studio.

Maengiener Uchwara wa bongo,

Vituko TU,

Serikali ya CCM ikisema 2+2=5.

Basi wachambuzi na Wasomii Uchwara wanajaribu njia zote kutafafanulia kwa nini Jawabu ni Tano .

CCM inageuza Taifa kuwa la hovyo sana na zaidii.

Hoja za kufulila, ati Hata bwana flani anafanya, kwanini iwe ajabu.

Duuuh hii ni hatari.

Wacha nisikie zangu wimbo wa Tanzania.

Tazama Ramani utaona Nchi zuri,
Yenye mito na mabonde mengi yanafaka.,
Nasema kwa kinywa harafu kwa kufikiri,
Nchii iliyo mashuhuri huitwa Tanzania.
 
View attachment 3266167

==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila hivi ndivyo alivyoandika baada ya baadhi ya Watanzania kushangaa kauli ya Rais Samia Suluhu kuhusu Tanzània kununua Umeme nje ya nchi, Ethiopia.

Mkurugenzi Kafulila anasema pamoja na kwamba nchi kubwa na tajiri duniani kama Marekani ( USA ), Ujerumani, Norway, Sweden au Australia wanaumeme mwingi kiasi Cha kuuza nje ya nchi zao bado na wao kwa Upande mwingine wa nchi zao wananunua umeme kutoka nje ya nchi zao.

Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini

Kafulila anasema kuwa baadhi ya maeneo ya nchi yetu hasa maeneo ya mipakani gharama ya kuzalisha, kusafirisha na kufikisha umeme maeneo hayo ni kubwa pengine kuliko gharama ya kuuvuta na kuununua umeme toka nchi za jirani.

===
Hili zwazwa linasema wanazalisha umeme wa ziada. Je sisi tunazalisha hata wa msingi? Hili likafulia sijui kama ni zima upstair au lina kaugonjwa ka licesiasis aka uchawa.
 
Back
Top Bottom