David Kafulila alitetemesha Bunge na kupokelewa kifalme

David Kafulila alitetemesha Bunge na kupokelewa kifalme

Hivi mkuu huyo mama yako akimaliza mda wake , ndio utakuwa mwisho wako wa hizi siasa uchwara?
 
Chukua muda wako kusoma na kujifunza uwe updated na mambo yakisasa hizi propaganda unazofanya ni za kizamani sana ndio mana unatumia nguvu nyingi sana kama chawa ukiongeza maarifa hiki unachofanya kinaweza kubadili maisha yako ila ukiendelea hivi na content mfu unakua unaonekana kama crazy hivi na watu wanakuchoka hivyo soma sana ili ufanye hizi kazi za propaganda kwa tija
Hoja hujibiwa kwa hoja na siyo viroja
 
Hivi mkuu huyo mama yako akimaliza mda wake , ndio utakuwa mwisho wako wa hizi siasa uchwara?
Nitaendelea kuwa na Mheshimiwa Rais hata akistaafu hapo 2030 Nitaendelea kumkumbuka alama zake na yale aliyoyafanya kwa Taifa letu,kama ambavyo tunaendelea kumkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
 
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima
Hata ikishinda haina uwezo wa kufikisha 50%, na ndani ya chaguzi 2 ccm itakuwa chama Cha upinzani na kifo Moja kwa Moja. Ukiona haiko tayari kwa tume huru ya uchaguzi, ujue hofu Yao ni kwenye ukweli huu.
 
Itashinda kwa zaidi ya 90%
 
Hoja hujibiwa kwa hoja na siyo viroja
Kwasababu ya viroja ndio mana sisiemu inatumia Watu wa kaliba yako kwakuamini bado wananchi wa leo ni wale wa sera za ukomonisti kwenye Arusha declaration jifunzeni kilichowakuta ANC hawakubadilika na mahitaji ya wakati na walishupaza shingo kwakuamini watu wanawakubali, ndio mana hatushangai mnapolalamikia wapinzani ile hali mmekua madarakani zaidi ya miongo sita ila majority ya generation ya uongozi ni koo zile zile mlizozitengeneza na jamii ya wapambe walamba soli wanaoamini kupata nafasi kwakusifia lile tabaka lililojimilikisha nchi sasa bahati mbaya na wewe umeingia kwenye hili tabaka la pili la wapambe lakini unfortunately mnasahau kua generation inayoongozwa saa hii imebadilika kabisa bila ku allign nayo ni suala la muda tu kujizolea aibu.
 
Haitashinda, bali watatangazwa washindi na tume isiyo huru ya uchaguzi.
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.
 
Usiifananishe CCM na ANC,kwa kuwa CCM ipo mbele ya wakati na ni chaka kiongozi Barani Afrika na ndio maana vyama vingi sana huja hapa Nchini kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ndani ya CCM.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa David Kafulila Ameamsha hisia, kuwagusa waheshimiwa wabunge na kuwarejesha mbali sana kihisia. Chuma Kafulila kaliteka Bunge, kalitetemesha na kalitikisa kwelikweli. Hii ni baada ya kutambulishwa Bungeni kama Mkurugenzi wa PPP na Mheshimiwa Speaker Dkt Tulia Acksoni Mwansasu.

Ambapo Bunge zima na wabunge wote na kwa Umoja wao wamempatia heshima kubwa na ya kipekee sana utafikiri utambulisho wa Mfalme wa Uingereza ndani ya Bunge. Ambapo imeshuhudiwa meza zoootee za waheshimiwa Wabunge zikilindima kwa kishindoo cha makofi ya kumpigia na kumpatia heshima ya kipekee Mheshimiwa Kafulila.

Bila shaka waheshimiwa wabunge wote bado wana kumbukumbu vichwani mwao juu ya alama alizoziacha za kizalendo, alizoziacha mzalendo huyu na mchapakazi aliyetukuka wakati wa ubunge wake 2010-2015.ambapo ni yeye amewahi kuweka historia ya kulifanya Bunge likafanya na kuendelea na shughuli zake mpaka saa Tano usiku katika Historia ya Bunge letu wakati wa sakata la Escrow.

Imeonyesha bunge zima na waheshimiwa wabunge wote wana kiu kubwa sana na kumhitaji Mheshimiwa Kafulila ndani ya Bunge, wanatambua uwezo wake, mchango wake na sauti yake kuwa bado inahitajika sana Bungeni wanaona ni kama kuna kitu kimepungua Bungeni kwa kutokuwepo kwa Mwamba huyu wa kigoma David Kafulila.

Waheshimiwa wabunge wanaona kuwa mtu huyu asiye na makandokando, Mzalendo wa dhati, mpole, mtulivu, makini, jasiri, shupavu, hodari, Madhubuti, imara, mnyenyekevu na mwenye misimamo ya dhati katika kutetea Taifa letu bado mchango wake unahitajika ndani ya Bunge letu.

Waheshimiwa wabunge wanaona kuna kazi Mheshimiwa Kafulila anatakiwa akasaidiane nao ndani ya Bunge ndio sababu ya heshima kubwa walioweza kumpatia,ndio sababu ya mapokezi mazito walioweza mpatia,ndio sababu ya kuguswa kwa wabunge wengi baada ya utambulisho wake, ndio sababu ya kumshangilia na kumpigia makofi bila kukoma ,ndio sababu ya kumheshimisha na kumpa thamani yake.

Waheshimiwa wabunge waliokuwepo na ambao hawakuwepo wakati wa sakata la Escrow wanakumbuka na wanakumbukunbu nzuri juu ya kazi kubwa, ya kishujaa na kizalendo kwa Taifa letu iliyofanywa na mheshimiwa David Kafulila aliyekuwa amejitolea maisha yake kupigania Taifa letu bila kujali vitisho kutoka kwa mtu yeyote yule.

Waheshimiwa wabunge wametuma kwa Vitendo ujumbe mzito sana juu ya Hazina hii kwa Taifa letu kuwa Bado sauti ya Mheshimiwa David Kafulila inahitajika sana Bungeni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

View attachment 3017339
Hivi kuna vyuo vinatoa kozi za uchawa? Nahisi we jamaa una PHD kwenye hiyo kozi. Hizi sifa ungekuwa wazitoa kumtukuza Mola wako, basi pepo kwako ingekuwa wazi sana. Unaijua sana kazi yako ya kusifu na kupamba wanadamu. Wanakulipa kiasi gani?
 
Waheshimiwa wabunge wameguswa sana mpaka wengine wameshindwa kuficha hisia zao za upendo kwa Mheshimiwa Kafulila.nakujikuta wakipiga makofi kwa hisia kali sana huku macho yao yakiwa ni kama yanataka kutokwa na Machozi
Teh teh... Kupiga makofi kwa hisia kali!!? Duh.. hiyo kiboko. Umejua kuwasemea wabunge. Yaani umekuwa mbunge wa wabunge [emoji16]
 
Hivi kuna vyuo vinatoa kozi za uchawa? Nahisi we jamaa una PHD kwenye hiyo kozi. Hizi sifa ungekuwa wazitoa kumtukuza Mola wako, basi pepo kwako ingekuwa wazi sana. Unaijua sana kazi yako ya kusifu na kupamba wanadamu. Wanakulipa kiasi gani?
Mimi ni msema kweli na mzalendo kwa Taifa langu na siyo kwamba naandika kwa ajili ya kulipwa chochote kile.
 
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.
Haina uwezo huo, ingekuwa na uwezo huo ingekubali tume huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom