Uchaguzi 2020 David Kafulila amjibu Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 David Kafulila amjibu Tundu Lissu

Mhoza

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2013
Posts
412
Reaction score
261
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kwasasa Jimbo la Uvinza amejibu hoja zilizotolewa jana na Mgombea kiti cha Urais wa JM !-

LISSU APANGULIWA HOJA 7 KWA MIKWAJU 7 YA TAKWIMU NA KAFULILA!

NIMEONA MATOBO 7 HOJA ZA LISSU!

Na David KAFULILA,
Agosti31, 2020.

Kwanza nashukuru sasa kuona ndugu yangu Tundu Lissu ameanza kuleta hoja zinazoweza kuanza kujadilika kama mgombea, tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa ni masimulizi ambayo kwakweli hayakuwa na lolote la kusaidia maamuzi ya mpiga kura.

Jana nilifuatilia hotuba yake iliyokosoa masuala kadhaa ambayo nimeona si busara ayatumie kupotosha Watanzania kufanya maamuzi katika misingi ya upotoshaji.

Ili kurahisisha, nimepanga mawazo yangu katika mafungu 7;

1. Lissu anasema Ripoti ya Benki ya Dunia ya Mwaka huu 2020 kuhusu urahisi wa kufanya Biashara( Easy of Doing Business Report 2020) imeishusha Tanzania kutokana na utawala wa JPM.

Asichokijua Lissu na wenzake wanaotumia hoja hiyo ni kwamba tayari Benki hiyo hiyo ya dunia (WB), katika taarifa yake ya tarehe ya juzi Agosti 27,2020, imeifuta tathimini hiyo ya Mwaka 2020 na ile ya 2018.

Benki ya Dunia imeleza wazi kuwa tathimini hizo zilikuwa na kasoro nyingi za kiuweledi na hivyo kukosa uhalisia. Kwa maelezo zaidi soma ....
Doing Business – Data Irregularities Statement

2. Lissu anashangaa inawezekanaje tuingie uchumi wa kati wakati tathimini ya taasisi ya MOODYS imeonesha Tanzania imeshuka daraja kutoka B1 Mwaka 2017 kwenda B2 Mwaka 2020 katika uwezo wa kukopa! ( credit rating).

# Hili ni suala la uelewa tu kwani, kwanza; hakuna uhusiano kati ya madaraja ya uchumi yanayopangwa na Benki ya dunia na madaraja ya uwezo wa kukopa yanayopangwa na taasisi zinazofanya tathimini hizo (GLOBAL CREDIT RATING AGENCIES) ikiwemo MOODYS.

#Ndio maana Mwaka 2017, Tanzania ilikuwa daraja la juu ( B1) kuliko Kenya (B2) kwenye ripoti za MOODY'S, ilhali Tanzania ilikuwa haijafuzu kuingia uchumi wa kati na Kenya ilikuwa tayari uchumi wa kati.

#Kujua kwamba Tanzania ilipewa daraja la juu kuliko Kenya Mwaka 2017, soma Gazeti la Daily Business la Kenya la Machi4,2017-link
US agency assigns Tanzania higher credit rating than Kenya

#Zaidi ni vema Lissu akafahamu kwamba kufuatia mtikisiko wa uchumi duniani uliosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa korona (COVID-19), nchi nyingi zimetikiswa kutokana na mtikisiko wa mnyororo wa biashara duniani (Global supply chain) ingawa ni kwa viwango tofauti.

# Ndio maana hata Kenya ambayo Mwaka 2017, taasisi ya MOODYS waliwapa daraja la B2 ikiwa na alama chanya (B2 with positive outlook), Mwaka huu 2020, imendelea kuwa na B2 lakini kwa alama hasi (B2 with negative outlook).

#Kiwango hicho ni chini ya Tanzania yenye daraja B2 chanya (B2 with positive outlook).

# Sijui kwa mtazamo wa Lissu huenda Kenya iliyopewa na MOODYS daraja chini ya Tanzania Mwaka huu angesema nayo ishushwe daraja kiuchumi kiasi gani kutoka uchumi wa kati.

# Pia ni vema ikafahamika kwamba serikali zinazoendeshwa kisasa duniani hutumia taasisi hizi kama MOODYS kufanyiwa tathimini. Na kwa Tanzania, kwa mara ya kwanza tumefanyiwa tahimini Mwaka 2017, chini ya JPM.

#.Hii ni kwasababu JPM anaamini katika usasa wa ukweli (real modernization) tofauti na Lissu anayedhani kuendesha uchumi kisasa ni kutozibana kampuni za madini kulipa kodi stahiki.

3.Hoja kwamba deni la Taifa wakati JK anaondoka lilikuwa trilioni 20 na kwamba katika awamu ya tano limeongezeka kufikia trilioni 40.

# Hili nalo ni suala la ufahamu kwani ingawa kweli deni limeongezeka lakini takwimu hizo sio za kweli. Wakati Lissu anasema JK aliacha deni la Trilioni 20, ukweli ni kwamba deni la nje peke yake Mwaka 2015....lilikuwa zaidi ya dola Billioni 16.4 au zaidi ya Trilioni 30TZS wakati huo, achilia mbali deni la ndani ambalo lilikuwa zaidi ya Trilioni 8.7TZS. (Chanzo- BoT Monthly Economic review).

# Usahihi wa takwimu na taarifa sahihi ni jambo muhimu sana hasa kwa Kiongozi anayetafuta kuaminika. Sijui Lissu hizi takwimu za trilioni 20 kazitoa vyanzo gani?

4.Lissu anasema uwezo wetu wa kuhimili deni umeshuka kwasababu deni limezidi kuwa kubwa.

# Labda nitoe ufahamu wa jumla tu kwamba tatizo la deni kwenye uchumi wowote linapimwa kwa vigezo zaidi ya ukubwa wa deni, bali vigezo vya uhimilivu (debt sustainability).

# Na dalili za wazi ambazo mtu wa kawaida anaweza kuzitumia kujua tuna tatizo la deni au lah!, ni kiwango cha riba unachotozwa kukopa.

#Serikali inapokuwa na hali mbaya kiuchumi (desperate) inakopa kwa riba kubwa kuliko Serikali yenye hali nzuri kiuchumi.

#Ndio sababu Mwaka 2015 kipindi ambacho serikali ilibidi kukopa ili kulipa mshahara watumishi, ilikopa soko la ndani kwa riba ya mpaka asilimia 17% kwa hatifungani za siku 365 Mwaka 2015, kulinganisha na kipindi cha JPM, ambapo Serikali inakopa kwa riba ya asilimia 4.8% kwa hatifungani za siku 365.

# Hiyo ni hali ya kawaida hata kwa maisha binafsi, kwamba ukiwa hoi kiuchumi (desperate) hutojali ukubwa wa riba unapotaka mkopo, lakini ukiwa vizuri kiuchumi huwezi kuchukua mkopo kwa riba kandamizi.

#Ninachojaribu kusisitiza ni kwamba afya yetu kiuchumi kumudu kukopa bado ni kubwa kwa vigezo vyote ndio maana Serikali inakopa kwa riba chini katika rekodi ya zaidi ya miaka10, na kwa vigezo vya tathimini za MOODY'S hakuna anayetuzidi afya hiyo ukanda huu.

5.Lissu anahoji umakini wa Serikali ya JPM kusimamia biashara na Sekta binafsi.

# Kifupi JPM amerejesha biashara na sekta binafsi kwenye reli, kutoka biashara za mishentaun kwenda biashara halisi. Bahati mbaya kila nikiwasikiliza Lissu na Membe naona fikra zao ni turudi uchumi wa 'mishemishe'

# Lissu anataka kupotosha Watanzania kama alivojaribu kwenye sekta ya madini wakati Rais alipoamua kuchukua hatua thabiti. Lissu alisema maamuzi ya madini yangeua sekta ya madini, lakini cha kushangaza mauzo ya dhahabu tu nje ( export) yameongezeka kutoka dola bilioni 1.3 mwaka 2015 mpaka dola bilioni 2.1 mwaka 2019.( BoT-MER)

# Lissu anapotosha Watanzania kuwa biashara chini ya JPM tunafanya vibaya kuliko kabla, nimkumbushe tu kwamba namba hazidanganyi. Mauzo ya Tanzania nje ya nchi Mwaka 2015 yalikuwa dola bilioni 8.9 kulinganisha na dola bilioni 9.7Mwaka 2019.

6. Lissu anahoji uamuzi wa kununua ndege kwamba haukupitishwa na Bunge.

# Labda hili lieleweke tu kwamba uamuzi wa kununua ndege haukupitishwa na upinzani bungeni sio bunge ingawa ilikuwa hoja ya upinzani mabunge yote kabla ya awamu ya tano kuingia na ilikuwa sehemu ya Ilani ya Chadema ya mwaka 2015 (rejea Ukurasa wa 40 Ilani ya Chadema).

#Ukweli kauli ya Lissu kwamba Bunge halikuhusjshwa ununuzi wa ndege ni ya kusikitisha mno kutolewa na mgombea nafasi ya juu kabisa ya nchi.

#Nasema hivi kwasababu bajeti ya ununuzi wa ndege kwa mara ya kwanza imepitishwa katika Bunge la Bajeti la 2016/17 ambapo ilitengwa na kupitishwa kiasi cha Trilioni 1.49TZS

# Naomba ifike wakati ieleweke na tuweke kumbukumbu sawa kwamba tumetoka zama ambazo tulikodi ndege mbovu kwa dola milioni 43 mpaka zama za kununua ndege mpya bombardier kwa dola milioni 32...( Ripoti ya CAG , Aprili 2020).

#Tumetoka zama za kujadili Taifa kukosa ndege mpaka zama za Taifa la kujadili namna ya kununua ndege (kwamba kununua kwa taslimu au kukopa). Huko nyuma hata uwezo wa kukopa hatukuwa nao.

7.Mwisho nihitimishe kwa kujadili hoja ya Lissu kuhusu Bima ya Afya nchini;

# Labda niseme kwamba nilipokuwa Songwe kama Katibu Tawala Mkoa, wananchi vijijini walionesha mwitikio mkubwa sana kuhusu bima ya afya hata ile ya chini kwa maana ya CHF.

# Songwe ulikuwa mkoa wa kwanza kwa kaya zenye bima ambapo asilimia76% walikuwa na bima hiyo.

# Mwitikio wa wananchi kwa bima ni kitu halisi hasa baada ya Serikali kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. ( kutoka kutengewa billioni 31 mpaka billioni 270).

# Ndio maana idadi ya Watanzania wanaotumia bima iliongezeka kutoka takribani wanufaika milioni 9.8 Mwaka 2015 mpaka zaidi ya milioni 16.7 mwaka 2019..

#Nimshauri Ndugu yangu Lissu awe anafanya tafiti ya anayolishwa na wenzake kabla hajayamwaga majukwaani. Moja ya sifa za kiongozi bora ni kujiridhisha na taarifa kabla ya kuziweka hewani.
 
Pumba tupu hivi ya maisha tuliyonayo hapa Tz hali ya duni ya uchumi inajionesha wazi haina hata haja ya hao wadau hadi waseme,yaani huyo kafulila anaingea as if anaishi rwanda hayupo Tanzania.

hivi hii hali ya uchumi wa watu na biashara ndogo hadi kubwa kuanguka tunaziona kwa macho yetu mnadanganya danganya ili iweje,ni muda wa kumwambia magufuli atatue changamoto za kiuchumi.

hata rate ya watu kufa imeongozeka kutokana na chumi mbovu za watu.
 
Napenda Critics..., kwa kuwa critical ndio tunaona makosa na kujenga..., swali langu ni kwamba hawa critics hawaoni mapungufu ya pande zile (hususan huyu aliyekuwa mpinzani thus ideology yake haiendani na Chama Tawala) Je kweli yote yanayofanyika huko ni Kosher ?, au ndio kujitoa ufahamu na kujivika u- Cheer Leader....
 
Huenda akakumbukwa kwenye teuzi baada ya uchaguzi, uzuri anafahamika na wenye nchi.
Akiendeleza juhudi zake kama hivi watamkumbuka tu mkuu.

Bora Makonda yeye hajui kubishana mambo ya uchumi,yeye baada ya kupigwa chini na wajumbe ameamua bora tu awe anapost khs kupata watoto mapacha basi.
 
Duuh hapa naona blah blah za kufukia shimo!Kafulila anatumia ujinga wa watanzania kuwahadaa na hoja nyepesi!
Hoja pekee ya kiuchumi zenye mashiko na kuweza kueleweka na Watanzania ni unafuu ktk kuendesha maisha ya kila siku kupitia vipato vyao, unafuu wa kodi na maduhuli yalipwayo serikalini, fursa zaidi za kiuchumi za mzawa kuweza kuwekeza na pua za kupata ajira ya uhakika nchini.

Zaidi ya hapo itakuwa ni kutuletea porojo tupu ili kujipendekeza kwa mtu fulani. Kafulila tafuta kazi nyingine ya kufanya, simamia kweli na uungane na vijana wengine ambao wanapigika kutokana na sera mbovu za CCM.
 
Hivi huyu kafulila alishawahi hata kuhoji ni nani alipanga kumtoa roho Lissu?

Njaa zake tu?

Haya basi subiria uteuzi.
 
Pumba tupu hivi ya maisha tuliyonayo hapa Tz hali ya duni ya uchumi inajionesha wazi haina hata haja ya hao wadau hadi waseme,yaani huyo kafulila anaingea as if anaishi rwanda hayupo Tanzania.

hivi hii hali ya uchumi wa watu na biashara ndogo hadi kubwa kuanguka tunaziona kwa macho yetu mnadanganya danganya ili iweje,ni muda wa kumwambia magufuli atatue changamoto za kiuchumi.

hata rate ya watu kufa imeongozeka kutokana na chumi mbovu za watu.
Kwa Hiyo Hata Kufa Watu ni Kosa LA Magufuri Hahaha Jibuni Hoja kwa Hoja Mshaumbuliwa Hapo Achokijibu Jamaa Upotoshajii Wa Lissu Kajibiwa Kwa Reference Yani Nyinyi Bana
 
Napenda Critics..., kwa kuwa critical ndio tunaona makosa na kujenga..., swali langu ni kwamba hawa critics hawaoni mapungufu ya pande zile (hususan huyu aliyekuwa mpinzani thus ideology yake haiendani na Chama Tawala) Je kweli yote yanayofanyika huko ni Kosher ?, au ndio kujitoa ufahamu na kujivika u- Cheer Leader....
MKUU HOJA HUJIBIWA KWAA HOJAA. JIBU HOJA, VINGINEVYO NAA WEWE UNAONEKANA POYOYO TU
 
Hoja pekee ya kiuchumi zenye mashiko na kuweza kueleweka na Watanzania ni unafuu ktk kuendesha maisha ya kila siku kupitia vipato vyao, unafuu wa kodi na maduhuli yalipwayo serikalini, fursa zaidi za kiuchumi za mzawa kuweza kuwekeza na pua za kupata ajira ya uhakika nchini.

Zaidi ya hapo itakuwa ni kutuletea porojo tupu ili kujipendekeza kwa mtu fulani. Kafulila tafuta kazi nyingine ya kufanya, simamia kweli na uungane na vijana wengine ambao wanapigika kutokana na sera mbovu za CCM.
VIJANA WENZANGU HAKUNA MAISHA RAHISI KWENYE NCHI ZINAZOENDELEA NI WAPUUZII PEKEE WANAOFIKILI KUBADALISHA VIONGOZI WA KISIASA KUTABADILISHA MAISHA YAO KATIKA UTAWALA HUU HUU WA MAGU VIJANA TUMEJIAJILI KWENYE UFUGAJI KILIMO NA BIASHARA NDOGONDOGO TUNAISHI MAISHA MAZURI KWANINI SISI TUWEZE NYINYI MSHINDWE SABABU NI UVIVU NA AKILI TEGEMEZE NA KUSUBILI SERIKALI IWAFANYIE KILA KITU VIJANA AMKENI MJITUME MAISHA NI HATUA WACHA KABISA
 
Kwa Hiyo Hata Kufa Watu ni Kosa LA Magufuri Hahaha Jibuni Hoja kwa Hoja Mshaumbuliwa Hapo Achokijibu Jamaa Upotoshajii Wa Lissu Kajibiwa Kwa Reference Yani Nyinyi Bana
Lissu alijichanganya mwenyewe akatolewa mfano, bila hivyo mkoloni acacia alitukalia vibaya, baada ya demo ya Lissu Blady hakurudi tena aka resign na kazini
 
Ni ujinga hali anajuwa watumishi wa umma hadi vyama vyao viliwatelekeza miaka 5 hii.
 
Back
Top Bottom