David Kafulila anakumbukwa na wakulima wa Simiyu kwa kupaisha bei ya Pamba kufikia Tsh. 2200 kwa kilo katika historia ya Taifa letu alipokuwa RC

Fuatilia kilichokuwa kinaendelea kabla, wakati na baada ya kutumbuliwa kwa Kafulila.
Kafulila alitumbuliwa na kutolewa kuwa RC wa Simayu, akawekwa benchi, akasugua makalio, akaanza uchawa mitandaoni, akakumbukwa na kupewa cheo cha mchongo kwenye uwekezaji. Ni kacheo fulani hivi ka ovyo, sasa jamaa naona hajaridhika nako maana hakampi upigaji wa kingedere, ndio maana kaswaga machawa kibao hapa JF wakumpa promo ili kuboost uteuzi mwingine.
 
Nenda hata leo kule Simiyu halafu tamka neno Kafulila au mama Samia kama hutatukanwa.

Lakini fika hapo hapo Simiyu halafu tamko Magufuli au Mtaka uone namna utakavyoshangiliwa.

Kwa wana Simiyu, kwa sasa Kafulila ni neno la kulaaniwa.
 
Tumia akili zako zote. Kwa akili yako unadhani yeye alizinunua? Au soko la duniaa aliliagiza kupandisha bei? Badala uongelee kushusha pembejeo ili hata soko la dunia lisiwaarithiri unajadili vitu viko nje ya uwezo wake. Rubbish
 
Nenda hata leo kule Simaye halafu tamko neno Kafulila au mama Samia kama hutatukanwa.

Lakini fika hapo hapo Simiyu halafu tamko Magufuli au Mtaka uone namna utakavyoshangiliwa.

Kwa wana Simiyu, kwa sasa Kafulila ni neno la kulaaniwa.
Kumbe hata wewe hauko Simiyu daaah,

ILA nimekuuliza nijibu swali langu,

Wananchi wa Simiyu Wanamchukia Kafulila Kwa sababu alisimamia wakauza Pamba yao kwa TZS 2,200 badala ya TZS 800?

Au kuna sababu nyingine.

Au Wanaomchukia ni wanunuzi na wachuuzi wa Pamba za Wakulima?

Mwambie huyo Mtakatifu aache kupotosha Viongozi Rais anapendwa sana Simiyu pengine kuliko sehemu yoyote ile ya nchi hii.

Kafulila hajawahi kuwa na mchezo na Wezi na Mafisadi andika hii pembeni itakusaidia katika hoja zako.

Haya hebu niambie kwanini walijinyonga kumkwepa Kafulila?

Mbona hawakujinyonga wakati wa Mtakatifu?
 
Kwanza tambua tu Mimi binafsi sijawahi kukaa hivi na Kafulila Wala namba yake Sina ila napenda sana Vijana Wazalendo aina yake.

Ogopa sana Mtu anakataa Fedha za Kitanzania zaidi ya TZS 2.8bl ogopa sana nasema ogopa nguvu ya pesa.

Sasa Kafulila kama ni Mkurugenzi Mkuu wa PPP unadhani anatamani kweli Uteuzi tena? Be serious.

Ila hatuwezi mzuia Rais kama atataka kumsaidia zaidi kwani nia yake ni njema sana kwa Taifa tangu akiwa kijana mdogo.
 
Tumia akili zako zote. Kwa akili yako unadhani yeye alizinunua? Au soko la duniaa aliliagiza kupandisha bei? Badala uongelee kushusha pembejeo ili hata soko la dunia lisiwaarithiri unajadili vitu viko nje ya uwezo wake. Rubbish
Soma hii itakusaidia,
👇👇👇

Kafulila alianzisha kitu kinaitwa "Simiyu model" .

Nia ya hii Model ni kutaka Ushirika kushindana na watu binafsi katika ununuzi wa Pamba.

Lakini pia Kafulila alianzisha kamati za pamba kudhibiti Kila hujuma ya walanguzi wa Pamba.

Matokeo ndio hayo bei ikafika mpaka 2200 wakati miaka yote bei ya pamba haijawahi kuzidi 1,200 kwa mkulima.

Ndio Wapo watu kama wewe mnaoweza kusema sababu ni kupanda kwa bei ya pamba katika soko la dunia dine,

Ukweli ni kwamba haukuwa mwaka wa kwanza bei kupanda katika soko la dunia na bado bei haikuzidi 1200/.

Mfano wa miaka ambayo Pamba ilipanda sana katika Soko la dunia ni Mwaka 2011, 2012, 2018 katika miaka hii bei ya pamba katika soko la dunia ilipanda na bado mkulima hakupata zaidi ya 1200/=.

Sasa huyu Kafulila alidhibiti chain ya wapigaji eneo la pamba ndani ya Mkoa mpaka kwenye mfumo wa wanunuzi.

Mimi naombeni watu waje wafanye utafiti alichofanya Kafulila na kilichotokea kwenye bei ya pamba ili kitumike kama mwongozo wa Serikali Kwa manufaa ya Sasa na kizazi kijacho.

Ukiongea na wazee wa pamba hapa Simiyu au mchambuzi wa miaka kama Mzee Joseph Mihangwa watakwambia yule kijana alikata mtandao wote wanaokula jasho la mkulima wa pamba.

Tunaweza kuzungumza mengi lakini Kafulila bado ni mtu mwenye uthubutu na ujasiri mkubwa wa kiuongozi.
 
Kilichomwondoa Kafulila sio Pamba,
Kilichomwondoa ni Kumnyanga'nya MNEC na Mbunge Soko na madini Simiyu na kulirudisha Serikalini haya mengine ni porojo tu.
 
Kilichomwondoa Kafulila sio Pamba,
Kilichomwondoa ni Kumnyanga'nya MNEC na Mbunge Soko na madini Simiyu na kulirudisha Serikalini haya mengine ni porojo tu.
Acha uzushi.
Mama akimzawadia Kafulila uRC wa Simiyu kwenda kuendelea kuwaunganisha wakulima wa Pamba kazi ambayo Mtaka alikuwa amekwisha kuifanya kwa 100%. Kilikuwa ni kipimo cha kwanza kabla ya kuja kumhamishia mkoa mkubwa kama Arusha nk. Lakini Kafulila akafeli kwa 100% akaishia kutumbuliwa usiku usiku.

Kafulila aliharibu mnooo kule Simiyu, akawagawa wananchi na kumkosanisha mama Samia na wanachi wa Simiyu, leo Samia anatukanwa ovyo na wanaSimiyu kwa kumuondoa Mtaka na kuleta kile Kibuyu cha kiha kutoka Kigoma.
 
Hongera wewe kijana nakukubali sana
Naona machawa mnapongezana.
Bora hata ile misukule ya Lumumba iliyokuwa inalipwa buku mbili na bundle kuja kupost upupu, kuliko hii michawa ya sasa.
Poor CCM.
 
Uchawa unaharibu hadi Akili.
Yaani Kafulila kakugeuza hadi umekuwa ndondocha wale, unaandika tu huku ukidhani kila mtu ni mjinga hapa JF. Ngoja tukupe shule.

Eti Kafulila ni mkurugenzi mkuu wa PPP? Nani kakwambia?
Unaandika kitu hata hukijui.
Kafulila aliteuliwa kuwa kamishna wa ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma (PPP). Kafulila sio mkurugenzi wa PPP ,na PPP sio kitengo kinachojitegemea hapa Tanzania.
Fahamu tu, PPP ni kiidara kidogo kimojawapo ndani ya wizara ya fedha na kiko chini ya naibu katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango.
 
Nakumbuka tangazo lilipotolewa kuwa Kafulila sio Mkuu wa Mkoa wa Simiyu tena,

Kulikuwa na mnada pale Sakasaka watu walipiga mwano utafikili wamefiwa kisa Kafulila.
Simiyu madalali wa Pamba wanamchukia sana Kafulila aliwatia hasara wakanunua Pamba kwa 2200 badala 1000 au mia nae.
Ila nasikia hahongeki huyu muha ndio maana anapigwaga vita sana sio mtu ya dili.
 
Duuuh PPP kwa sasa ni idara Kamili kama ilivyo TIC inawatumishi kibao na bajeti ni yake sio Fedha.
 
Duuuh PPP kwa sasa ni idara Kamili kama ilivyo TIC inawatumishi kibao na bajeti ni yake sio Fedha.
Acha blah blah wewe.
PPP ni idara ndogo (wala sio kitengo) ndani ya wizara ya fedha na iko chini ya ofisi ya naibu katibu mkuu wizara ya fedha.

Kama TRA ni kitengo ndani ya wizarq ya fedha, vipi kuhusu kiidara kidogo kama PPP?

Kama TIC ni kitengo ndani ya wizara ya uwekezaji, vipi kuhusu PPP ambayo ni kiidara kidogo?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…