David Kafulila anakumbukwa na wakulima wa Simiyu kwa kupaisha bei ya Pamba kufikia Tsh. 2200 kwa kilo katika historia ya Taifa letu alipokuwa RC

Embu acha porojo zako wewe .nani alikwambia kuwa alitumbuliwa kwa hasira? Kwanini alipewa tena uteuzi? Unajuwa Mhessimiwa Rais anaweza kukutoa mahali popote pale na kukupeleka mahali popote pale kwa wakati wowote na muda wowote ule?

Unafahamu mbinu alizotumia Mhessimiwa Kafulila kupandisha bei ya pamba mkoani Simiyu?
Fuatilia kilichokuwa kinaendelea kabla, wakati na baada ya kutumbuliwa kwa Kafulila.
Kafulila alitumbuliwa na kutolewa kuwa RC wa Simayu, akawekwa benchi, akasugua makalio, akaanza uchawa mitandaoni, akakumbukwa na kupewa cheo cha mchongo kwenye uwekezaji. Ni kacheo fulani hivi ka ovyo, sasa jamaa naona hajaridhika nako maana hakampi upigaji wa kingedere, ndio maana kaswaga machawa kibao hapa JF wakumpa promo ili kuboost uteuzi mwingine.
 
Crde mbona umekuwa duni kiasi hiki?

1. Unasema Wananchi wa Simiyu wanamchukia Samia kwa sababu ya Kafulila fine,

Swali,

a). Kama Kafulila na Rais Samia waliwapa bei ya TZS 2,200 na wanamchukia Rais Samia kama unavyosemaga humu fine,

Vipi kabla na baada ya Kafulila walipopewa bei ya TZS 1,000 wamempenda zaidi Rais au RC aliyeko au huyo Mtakatifu Unayemtaja taja hapa?

Wewe huna akili,

Wananchi wamchukiaeje Kafulila aliyewapa bei NoNo ya 2,200 waje wampende wa 1,000,???!!!

Sikia Crde ,

Hakuna kipindi Rais Samia na Serikali yake na Chama chetu tulifurahiwa na Wanasimiyu kama wakati wa Kafulila achana na majungu ya hao Watakatifu unaowataja taja hapa.

Kafulila aliingia Simiyu 2021 na akauza Pamba yake 2022 kwa TZS 2,200.

Then akaondolewa kwa hasira kama unavyosema wewe.

Kumbe hasira hizi mlizichochea ninyi kwa masilahi yenu.

Simiyu huwezi kuzungumzia Pamba ya TZS 2,200 bila kumtaja Kafulila na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mwisho niweke sawa hili.

Mkoa wa Simiyu tunampenda sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hata kama kura ikipigwa Leo atapata kura zaidi ya 85% so wait and see 2025.
Nenda hata leo kule Simiyu halafu tamka neno Kafulila au mama Samia kama hutatukanwa.

Lakini fika hapo hapo Simiyu halafu tamko Magufuli au Mtaka uone namna utakavyoshangiliwa.

Kwa wana Simiyu, kwa sasa Kafulila ni neno la kulaaniwa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Uongozi ni kuacha alama zinazoishi katika Maisha na mioyo ya watu,ni kuacha kitu kitakacho simuliwa vizazi kwa vizazi,ni kuacha rekodi ambayo itaimbwa na kuzungumzwa na watu kwa miaka mingi hata kama wewe utakuwa haupo uongozini au Duniani lakini utaendelea kuishi na watu japo hupo Duniani au madarakani.

Uongozi siyo habari ya umeongoza miaka mingapi au umekaa miaka mingapi. kinachomfanya mtu akakumbukwa na watu ni kazi alizozifanya kwa muda alipokuwa na madaraka au hai na faida ya uhai wake kwa watu na uongozi wake ulivyogusa maisha ya watu.

Ndio maana leo hii viongozi na watu kama John F Kennedy ,Dr Martin Luther King Junior,BoB Marely ,Abraham Lincolin wanaendelea kukumbukwa na watu wengi sana Duniani kwote licha ya kwamba walikufa miaka mingi na waliishi miaka michache Duniani kabla ya kufikia uzee wao. Ndio maana pia viongozi kama Edward Moringe Sokoine wanakumbukwa na Taifa letu japo walikaa madarakani kwa Muda mfupi lakini historia zao na majina yao yameganda na kunasa katika mioyo ya watanzania kutokana na mikono yao na kazi zao kugusa maisha ya watu na kuleta matokeo Chanya.

Hii maana yake nini? Unaweza kuongoza kwa miaka mingi,kukaa madarakani au kwenye cheo fulani kwa miaka mingi na bado usikumbukwe na yeyote yule pale ambapo utaondoka leo.unaweza kuondoka leo kwenye ukuu wa mkoa au uwaziri au uwaziri mkuu au uspika au ukurugenzi wa taasisi fulani halafu kesho watu wakasahau kabisa kama ulikuwepo kwenye nafasi fulani.kwanini? Kwa sababu uongozi wako na uwepo wako kwenye kiti haukugusa wala kubadilisha maisha ya watu au mtu yeyote yule.kwa hiyo ulikuwa kama mvuke au moshi tu ambao umekuja na kupita.

Mheshimiwa David Kafulila licha ya kukaa katika nafasi ya Ukuu wa mkoa Wa Simiyu kwa muda mfupi lakini bado anaendelea kukumbukwa na wana Simiyu kama mkuu wa mkoa aliyeleta tabasamu,furaha, matumaini na kuwainua kiuchumi kwa kupaisha Bei ya pamba yao ambayo kwa karibu 70% ya pamba yote Tanzania inatokea Simiyu kufikia bei ya 2200 kwa kilo, bei ambayo haikuwa kutokea tangia Nchi yetu ipate uhuru.leo anakumbukwa na kusemwa kuwa hapa Simiyu kilipita na kulipita CHUMA David Kafulila aliyeleta Nuru kwa wakulima na maendeleo kwa kaya za wanasimiyu.

Jiulize wewe kiongozi uliyepo kwenye cheo fulani au wadhifa fulani ukiondoka leo kwenye nafasi uliyopo watu watakukumbuka kwa lipi? Umegusa maisha ya watu wangapi? Umeleta tabasamu kwa kaya ngapi? Wangapi wamepata nuru kutoka gizani? wangapi wamepata matumaini kupitia mikono yako? Wangapi wanatamani urejee au urudishwe au uongezewe muda au kukuombea dua na maombi mema ya kurejea au kupata cheo kikubwa au nafasi fulani? Utakumbukwa kwa lipi ndugu yangu? Au unaisha na kufanya kazi ilimradi tu watoto wako wapate ugali mezani? Umebadilisha maisha ya wangapi?

Wangapi wanaona uwepo wako hapo ulipo ni baraka na mlango wa wao kutokea kimaisha na kuinuka kiuchumi? Wangapi wanakukumbuka kwa mema?

Gusa maisha ya watu, Leta tabasamu kwa watu,washa taa kwenye mioyo ya watu,inua watu,shika mikono ya watu uwainue juu,wape matumaini watu ili siku moja Ukumbukwe kama ilivyo kwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere,Nelson Mandela,kwame Nkrumah, Keneth Kaunda, Winnie Mandela na wengine wengi sana. Lakini pia ukifanya vyema utaungwa mkono ukiwa bado hai kama ilivyo kwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Tumia akili zako zote. Kwa akili yako unadhani yeye alizinunua? Au soko la duniaa aliliagiza kupandisha bei? Badala uongelee kushusha pembejeo ili hata soko la dunia lisiwaarithiri unajadili vitu viko nje ya uwezo wake. Rubbish
 
Nenda hata leo kule Simaye halafu tamko neno Kafulila au mama Samia kama hutatukanwa.

Lakini fika hapo hapo Simiyu halafu tamko Magufuli au Mtaka uone namna utakavyoshangiliwa.

Kwa wana Simiyu, kwa sasa Kafulila ni neno la kulaaniwa.
Kumbe hata wewe hauko Simiyu daaah,

ILA nimekuuliza nijibu swali langu,

Wananchi wa Simiyu Wanamchukia Kafulila Kwa sababu alisimamia wakauza Pamba yao kwa TZS 2,200 badala ya TZS 800?

Au kuna sababu nyingine.

Au Wanaomchukia ni wanunuzi na wachuuzi wa Pamba za Wakulima?

Mwambie huyo Mtakatifu aache kupotosha Viongozi Rais anapendwa sana Simiyu pengine kuliko sehemu yoyote ile ya nchi hii.

Kafulila hajawahi kuwa na mchezo na Wezi na Mafisadi andika hii pembeni itakusaidia katika hoja zako.

Haya hebu niambie kwanini walijinyonga kumkwepa Kafulila?

Mbona hawakujinyonga wakati wa Mtakatifu?
 
Fuatilia kilichokuwa kinaendelea kabla, wakati na baada ya kutumbuliwa kwa Kafulila.
Kafulila alitumbuliwa na kutolewa kuwa RC wa Simayu, akawekwa benchi, akasugua makalio, akaanza uchawa mitandaoni, akakumbukwa na kupewa cheo cha mchongo kwenye uwekezaji. Ni kacheo fulani hivi ka ovyo, sasa jamaa naona hajaridhika nako maana hakampi upigaji wa kingedere, ndio maana kaswaga machawa kibao hapa JF wakumpa promo ili kuboost uteuzi mwingine.
Kwanza tambua tu Mimi binafsi sijawahi kukaa hivi na Kafulila Wala namba yake Sina ila napenda sana Vijana Wazalendo aina yake.

Ogopa sana Mtu anakataa Fedha za Kitanzania zaidi ya TZS 2.8bl ogopa sana nasema ogopa nguvu ya pesa.

Sasa Kafulila kama ni Mkurugenzi Mkuu wa PPP unadhani anatamani kweli Uteuzi tena? Be serious.

Ila hatuwezi mzuia Rais kama atataka kumsaidia zaidi kwani nia yake ni njema sana kwa Taifa tangu akiwa kijana mdogo.
 
Tumia akili zako zote. Kwa akili yako unadhani yeye alizinunua? Au soko la duniaa aliliagiza kupandisha bei? Badala uongelee kushusha pembejeo ili hata soko la dunia lisiwaarithiri unajadili vitu viko nje ya uwezo wake. Rubbish
Soma hii itakusaidia,
👇👇👇

Kafulila alianzisha kitu kinaitwa "Simiyu model" .

Nia ya hii Model ni kutaka Ushirika kushindana na watu binafsi katika ununuzi wa Pamba.

Lakini pia Kafulila alianzisha kamati za pamba kudhibiti Kila hujuma ya walanguzi wa Pamba.

Matokeo ndio hayo bei ikafika mpaka 2200 wakati miaka yote bei ya pamba haijawahi kuzidi 1,200 kwa mkulima.

Ndio Wapo watu kama wewe mnaoweza kusema sababu ni kupanda kwa bei ya pamba katika soko la dunia dine,

Ukweli ni kwamba haukuwa mwaka wa kwanza bei kupanda katika soko la dunia na bado bei haikuzidi 1200/.

Mfano wa miaka ambayo Pamba ilipanda sana katika Soko la dunia ni Mwaka 2011, 2012, 2018 katika miaka hii bei ya pamba katika soko la dunia ilipanda na bado mkulima hakupata zaidi ya 1200/=.

Sasa huyu Kafulila alidhibiti chain ya wapigaji eneo la pamba ndani ya Mkoa mpaka kwenye mfumo wa wanunuzi.

Mimi naombeni watu waje wafanye utafiti alichofanya Kafulila na kilichotokea kwenye bei ya pamba ili kitumike kama mwongozo wa Serikali Kwa manufaa ya Sasa na kizazi kijacho.

Ukiongea na wazee wa pamba hapa Simiyu au mchambuzi wa miaka kama Mzee Joseph Mihangwa watakwambia yule kijana alikata mtandao wote wanaokula jasho la mkulima wa pamba.

Tunaweza kuzungumza mengi lakini Kafulila bado ni mtu mwenye uthubutu na ujasiri mkubwa wa kiuongozi.
 
Mleta mada kama hujui tu, kilichomuondoa Kafulila Simiyu ni kitendo chake kwenda kuua kilimo cha Pamba.
Juhudi zote za kuifufua Pamba kule Simiyu zilizofanywa na Anthony Mtaka kwa miaka kadhaa, Kafulila alikuja kuziua kabisa.
Kinachoendelea leo kule Simiyu ni matokeo ya kiburi na upuuzi wa Kafulila. Leo hii Kafulila akija Simiyu anaweza kupopolewa mawe.
Kilichomwondoa Kafulila sio Pamba,
Kilichomwondoa ni Kumnyanga'nya MNEC na Mbunge Soko na madini Simiyu na kulirudisha Serikalini haya mengine ni porojo tu.
 
Acha uzushi.
Mama akimzawadia Kafulila uRC wa Simiyu kwenda kuendelea kuwaunganisha wakulima wa Pamba kazi ambayo Mtaka alikuwa amekwisha kuifanya kwa 100%. Kilikuwa ni kipimo cha kwanza kabla ya kuja kumhamishia mkoa mkubwa kama Arusha nk. Lakini Kafulila akafeli kwa 100% akaishia kutumbuliwa usiku usiku.

Kafulila aliharibu mnooo kule Simiyu, akawagawa wananchi na kumkosanisha mama Samia na wanachi wa Simiyu, leo Samia anatukanwa ovyo na wanaSimiyu kwa kumuondoa Mtaka na kuleta kile Kibuyu cha kiha kutoka Kigoma.
 
Hongera wewe kijana nakukubali sana
Naona machawa mnapongezana.
Bora hata ile misukule ya Lumumba iliyokuwa inalipwa buku mbili na bundle kuja kupost upupu, kuliko hii michawa ya sasa.
Poor CCM.
 
Kwanza tambua tu Mimi binafsi sijawahi kukaa hivi na Kafulila Wala namba yake Sina ila napenda sana Vijana Wazalendo aina yake.

Ogopa sana Mtu anakataa Fedha za Kitanzania zaidi ya TZS 2.8bl ogopa sana nasema ogopa nguvu ya pesa.

Sasa Kafulila kama ni Mkurugenzi Mkuu wa PPP unadhani anatamani kweli Uteuzi tena? Be serious.

Ila hatuwezi mzuia Rais kama atataka kumsaidia zaidi kwani nia yake ni njema sana kwa Taifa tangu akiwa kijana mdogo.
Uchawa unaharibu hadi Akili.
Yaani Kafulila kakugeuza hadi umekuwa ndondocha wale, unaandika tu huku ukidhani kila mtu ni mjinga hapa JF. Ngoja tukupe shule.

Eti Kafulila ni mkurugenzi mkuu wa PPP? Nani kakwambia?
Unaandika kitu hata hukijui.
Kafulila aliteuliwa kuwa kamishna wa ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma (PPP). Kafulila sio mkurugenzi wa PPP ,na PPP sio kitengo kinachojitegemea hapa Tanzania.
Fahamu tu, PPP ni kiidara kidogo kimojawapo ndani ya wizara ya fedha na kiko chini ya naibu katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango.
 
Nakumbuka tangazo lilipotolewa kuwa Kafulila sio Mkuu wa Mkoa wa Simiyu tena,

Kulikuwa na mnada pale Sakasaka watu walipiga mwano utafikili wamefiwa kisa Kafulila.
Simiyu madalali wa Pamba wanamchukia sana Kafulila aliwatia hasara wakanunua Pamba kwa 2200 badala 1000 au mia nae.
Ila nasikia hahongeki huyu muha ndio maana anapigwaga vita sana sio mtu ya dili.
 
Uchawa unaharibu hadi Akili.
Yaani Kafulila kakugeuza hadi umekuwa ndondocha wale, unaandika tu huku ukidhani kila mtu ni mjinga hapa JF. Ngoja tukupe shule.

Eti Kafulila ni mkurugenzi mkuu wa PPP? Nani kakwambia?
Unaandika kitu hata hukijui.
Kafulila aliteuliwa kuwa kamishna wa ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma (PPP). Kafulila sio mkurugenzi wa PPP ,na PPP sio kitengo kinachojitegemea hapa Tanzania.
Fahamu tu, PPP ni kiidara kidogo kimojawapo ndani ya wizara ya fedha na kiko chini ya naibu katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango.
Duuuh PPP kwa sasa ni idara Kamili kama ilivyo TIC inawatumishi kibao na bajeti ni yake sio Fedha.
 
Acha blah blah wewe.
PPP ni idara ndogo (wala sio kitengo) ndani ya wizara ya fedha na iko chini ya ofisi ya naibu katibu mkuu wizara ya fedha.

Kama TRA ni kitengo ndani ya wizarq ya fedha, vipi kuhusu kiidara kidogo kama PPP?

Kama TIC ni kitengo ndani ya wizara ya uwekezaji, vipi kuhusu PPP ambayo ni kiidara kidogo?
 
Back
Top Bottom