Duuuh kumbe hata anavyoandikaga kumuhusu Rais Samia ni Rais huyu anamlisha hayo maneno?
Lucas Mwashambwa yeye ametoa sababu kwanini anavutiwa na Kafulila,
Wewe kama unasababu ambazo unaamini sifa anazopewa Kafulila ni za uongo pia zilete hapa,
Ila Mimi kwa kuwa niko field acha nikusaidie kidogo.
👇👇👇
Kafulila alianzisha kitu kinaitwa Simiyu model.
Nia ya hii Model ni kutaka Ushirika kushindana na watu binafsi katika ununuzi wa Pamba.
Lakini pia Kafulila alianzisha kamati za pamba kudhibiti Kila hujuma ya walanguzi wa Pamba.
Matokeo ndio hayo bei ikafika mpaka 2200 wakati miaka yote bei ya pamba haijawahi kuzidi 1,200 kwa mkulima.
Ndio Wapo watu kama wewe mnaoweza kusema sababu ni kupanda kwa bei ya pamba katika soko la dunia dine,
Ukweli ni kwamba haukuwa mwaka wa kwanza bei kupanda katika soko la dunia na bado bei haikuzidi 1200/.
Mfano wa miaka ambayo Pamba ilipanda sana katika Soko la dunia ni Mwaka 2011, 2012, 2018 katika miaka hii bei ya pamba katika soko la dunia ilipanda na bado mkulima hakupata zaidi ya 1200/=.
Sasa huyu Kafulila alidhibiti chain ya wapigaji eneo la pamba ndani ya Mkoa mpaka kwenye mfumo wa wanunuzi.
Mimi naombeni watu wakafanye utafiti alichofanya Kafulila na kilichotokea kwenye bei ya pamba ili kitumike kama mwongozo wa Serikali Kwa manufaa ya Sasa na kizazi kijacho.
Ukiongea na wazee wa pamba hapa Simiyu au mchambuzi wa miaka kama Mzee Joseph Mihangwa watakwambia yule kijana alikata mtandao wote wanaokula jasho la mkulima wa pamba.
Tunaweza kuzungumza mengi lakini Kafulila bado ni mtu mwenye uthubutu na ujasiri mkubwa wa kiuongozi.