David Kafulila atolea ufafanuzi wa Adani kuwekeza katika Miundombinu ya Umeme kwa Ubia

Fursa iliyopo ni umeme wa jua au upepo...Tutashukuru sana wakija kuwekeza kwenye maeneo hayo
Kwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoendelea kuikumba Dunia nzima ni muhimu kuendelea kuwekeza katika vyanzo mbalimbali vya nishati hii kama ambavyo serikali yetu imekuwa ikifanya . Ndio maana tunaendelea kuwekeza katika umeme wa maji,gas,jua,upepo n.k.ili ikitokea tumekwama Sehemu basi Taifa lisiingie gizani.
 
Kwani alifanya kwa upendo au alifanya kwa sababu analipwa mshahara!?! Sio uzalendo! Anajua kuwa anapewa kibunda chake!
 


Tatizo na kukurupuka ni ujinga nchi kuwekeza kwenye usambazaji maana huwezi kufuta mikataba ya hivi . Uwekezaji ni kwenye uzalishaji ! Yaani mwekezaji akikuwekea waya kwenye kijiji bei haitaweza kushuka ni wizi ndiyo maana Tanesco inatakiwa kumiliki usambazaji na kuruhuru uwekezaji kwenye uzalishaji. Tusikubali huu uwekezaji hauna manufaa.
 
Na hii ndo shida ambayo viongozi wengi wanaiona ila hawataki kuionesha! Hapo tutegemee bei kuruka juu zaidi.
 
Ahh Mkuu kwamba unataka kusema ukitoa mshahara wake na pesa zingine bado atafanya kazi?! Au unamzungumzia Kafulila yupi!?
Ndio atafanya vyema kabisa bila shida wala kuhitaji malipo. Hivi unafahamu mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu iliyokuwa ikimpatia mshahara nakwenda kufanya kazi ya kujitolea kwa ajili ya kutafuta uhuru wa Nchi hii? Sasa huyo ndio role model wake
 
Na hii ndo shida ambayo viongozi wengi wanaiona ila hawataki kuionesha! Hapo tutegemee bei kuruka juu zaidi.
Hatuleti muwekezaji kama Taifa kuja kuongeza bei bali kuja kushusha bei na kurahisisha maisha ya watanzania, hususani kipindi hiki ambacho Mheshimiwa Rais anapambana kuhakikisha watanzania tunatumia nishati safi kwa ajili kupikia
 
Hapi hakuna bishara ni sawa na mtu kuomba kazi ambayo haipo jalafu unatoka hadharani kutangaza kuwa nafasi ya kazi fulani wameomba watu elfu 10 wakati hiyo kazi haipo!

Kafulila mjinga sana kwa hilo aweza iingiza serikali matatani kisheria

Kutangaza majina ya watu walioonyesha expression of interest huwa mchakato unakuwa umeshapitiwa na kamati mbalimbali na serikali kuridhia ndipo ubatoka hadharani kutamka

Biashara haipo halafu unatoka hadharani kutangaza kuwa fulani na fulani wameomba tenda ya biashara ambayo haipo kwa wakati huo nini hicho?
 
Ndio atafanya vyema kabisa bila shida wala kuhitaji malipo. Hivi unafahamu mwalimu Nyerere aliacha kazi ya ualimu iliyokuwa ikimpatia mshahara nakwenda kufanya kazi ya kujitokea kwa ajili ya kutafuta uhuru wa Nchi hii? Sasa huyo ndio role model wake
Duuh Mkuu! Mbona hapo maji marefu sana yaani Mwalimu ndo role model wa Kafulila!?? Serious kabsa
 
Hatuleti muwekezaji kama Taifa kuja kuongeza bei bali kuja kushusha bei na kurahisisha maisha ya watanzania, hususani kipindi hiki ambacho Mheshimiwa Rais anapambana kuhakikisha watanzania tunatumia nishati safi kwa ajili kupikia
Mapambio yaendelee!
 
Duuh Mkuu! Mbona hapo maji marefu sana yaani Mwalimu ndo role model wa Kafulila!?? Serious kabsa
Mheshimiwa Kafulila ni Mwanafunzi mtiifu wa Mwalimu Nyerere aliyewataka vijana kuwa waadilifu , wachapakazi na wazalendo kwa Taifa letu.
 
Acha matusi yako .kama hujasoma andiko na kuelewa ni bora ukaomba usomewe na ueleweshwe. Mheshimiwa Kafulila amefafanua vizuri sana na kwa hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…